Subaru vs Vanguard

Kitakachoibeba c200 na 320i ni uwezo wa kuvuka 180kph ila kwa zone za 0-180kph utashangazwa na Crown au Mark X hasa dereva akiwa jasiri.
Yes... Kwenye acceleration c200 na 320i sio wazuri kutokana na design ya gearbox...yaan zipo fixed gear ratio ambayo inafanya gear box i shoft from one gear to another..maana yake kila muda gear shifting inapotokea kuna deceleration inatokea before another gear kua picked up...hichi kitu hakipo kwa gari yenye CVT transmission (yaan continuous variable transmission) yaan muda wote transmission inakua connected to engine while varying gear ratios (through pulleys and belt)(no power cut from engine to tires) hapa utaona tu gar ina accelerate very fast to top speed (180). Baaada ya hapo sasa mzungu ndo anaanza kukunyanyasa kwenda 180+ mpaka...hapa hata Volkswagen polo ya zaman yenye cc 1300 anakuwashia indicator ya kuomba site akupite unabaki unamfukuza na usimpate tena.
 
Asee naona kuna watu hawajui spec nyingi za engine..kuna cc, kuna horse power na kuna kitu kinaitwa torque..sasa nguvu ipo kwenye torque... power multiplication ya cc na horse power..ntatoa mfano unakua kuna mlorry wa mchina una horse power 380 lakini kacheck torque yake....

Kuhusu Brevis na LC 200..brevis anaweza achwa na lc 200 mkuu tena mbali..kwakua lc ina torque kubwa sana.. pia ina top speed kubwa (260) wakati brevis ana 180..tena high way brevis hafati kabisa.
 
Wale wakiwa kwenye msafara wanatembea speed inayoweza kua attained na gari yenye top speed ndogo..mfano unakuta kwenye masafara unagari nyingi zikiwemo hardtop land cruiser..sasa land cruiser hardtop hata kufika tu 180 nyingi hazifiki hata kama ni mpya...so wanatembea mwendo ule ili ku accomodate gari yenye speed ndogo but zikiwa zenyewe tu lc 200 au lc 300 mkuu hukamati.
 
Hapo weight to body ratio ndio ita dictate mzee. Crown gari ya tani moja na nusu kiuzito ni nusu ya uzito wa hio LC.

Kwenye Drag Race Crown itatangulia mbele na itamaliza 180 kama ni long stretch kisha ndio Cruiser yenye zaidi ya 180 itafungua mapafu na kuanza kuivuta taratibu hadi kuikata.

Ila kwa Crown za chinese model zenye 260kph ipo kazi. Ukute ni 2GR ile ya 3500cc ni balaa zito.
 
Iki kicarina nikauze tu haiwezekani kisahani kinasoma 140kph lakini nakuja kupitwa na sauli kirahisi hivi kama nimesimama?
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 CARINA sidhani hata kama itamaliza 180KPH zote ikiwa ishachoka.
 
Crown inatulia kama Yatch inavyoelea kwenye bahari ya Hindi. Hio yako inayokupa presha labda kama umefunga shockup za Koroma au Jinbo 🤣🤣🤣
 
Yani Dualis kagari ka horsepower 140 ushindanishe na gari ya horsepower 170 tena yenye gear 7? Vanguard nyingi nimekutana nazo highway na zina kichaa kweli kweli!
 
Vp hao mapacha wa3( mark x , Crown na Brevis) wakikutana na C200 Kompressor au 320i nani atamezwa hapo mkuu kwa uzoefu wako?
Hapo wajerumani wote wanalamba mchanga. Huwezi amini ila ndio ukweli na hio ni until Crown akimaliza kazi yake then ndio watakuja kumpita past 180KPH.

Crown 0-100kph inatumia sekunde 6 tu wakati BMW ni 8.9 na benz ni 9.4! Tayari kwenye takeoff wanakuwa washaachwa.
 
Nataka tofauti ya specs za Crown Majesta, Athlete na Royal Saloon.
Majesta ana 345HP V8 engine High-End luxury. Huyu ndo babalao

Royal Saloon ni Luxury ila ianshea engine sawa na Athlete. Tofauti zake moja ina Sport suspensions (Athlete) na ingine ina Soft suspension kwa burudani zaidi (Royal Saloon)
 
Labda dereva awe mwoga
Wewe uje upunguze spidi kupanda tuta mwenzako keshalivuka yuko mbele yako
 
Una uhakika walikuwa wanakimbizana na wewe?
 
Mkuu hao ndiyo wabongo wanaitwa huyo jamaa hajawahi kuendesha crown wala kupewa lift kwenye LC200..
Hapa jukwaaani kuna story nyingi za kwenye kahawa hii ndiyo shida nimesoma comments nyingi kule juu nimeshangaa Sana
Kama ingekuwa hivyo serikali ingenunua Crown.

VX V8 ni dude haswaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…