"Wenye nyumba tuna mbinu nyingi, ukitutoka katika umeme tutakupata tu hata katika maji, ukizidi sana tunaona umepapenda kwetu halafu mjanja mjanja tuna mitoto yetu mikorofi itakuibia.😀
Ukiendelea kukomaa tutapandisha bei za vitu vya ajabu ajabu kama vile usafi, tutawakumbusha wazawa wenzetu kukukomalia pesa ya ulinzi na usafi wa jiji tuwapokelee ili uwe haupumui, mida ya utulivu na mkeo ndio tunagonga mlango kukukumbusha 😀
Ukiwa mwema, mwema tutakuwa tunakupiga piga mizinga na kukopa kopa, yani kwa kifupi sera ni mpangaji asi relax ajenge haraka, au akodi nyumba nzima. Ukikaa na sisi wewe ni familia yetu kwa manufaa yetu, shda zetu zinakuhusu ila zako inategemea
Mkitubana sana kwa sababu ni ya urithi tutauza,tunaenda kukuza tena mji pembezoni na kuendelea kuwabana"
NATANIA ILA INAKUJA KUJA HIVIIII KAMA KWELI
😀