Eti Sugu nae sasa ( siku hizi ) anaitwa Bilionea. Najua kuwa Sugu ana Hela ( GENTAMYCINE simfikii ng'o ) ila bado hana Hadhi ya Kuitwa Bilionea unless labda hatujui maana ya Bilionea au tunahitaji Msaada wa Kiufafanuzi kutoka BAKITA na BOT juu ya maana na dhana nzima ya neno Bilionea na Mtu Kuitwa Bilionea.
Kwangu Mimi Sugu akiitwa Mfanyabiashara au Mjasiriamali mwenye Mafanikio nitakubali tena kwa 100% ila leo hii kumuita Sugu Bilionea ni Kulidharau neno husika na Kuwadharau wale Mabilionea hasa kama akina Bakhressa, Mo Dewji, Rostam, GSM na wengineo baadhi.