Sugu ana nguvu mara 100% kuliko Tulia na sababu ni moja tu - USA!

Nimecheka sana .. sasa hiyo nguvu ya USA si akogombee huko USA??
Sisi watu wa Mbeya tunajua kiasi gani Tulia kagusa mioyo yetu
 
Iwe jua, iwe mvua Kamanda Sugu atashinda kwa kura nyingi sana. Mwananchi wa kawaida wa Mbeya Mjini hawezi kujua IPU ni nini na inampa faida gani.
 
Unaposema Sugu ni CIA unamaanisha ni mtumishi wao? Sugu anaweza kuwa chawa wa USA lakini hawezi kuwa mtumishi wa CIA

Kumbuka Marekani hawana rafiki wala adui wa kudumu rejea Sadam Hussein na Iraq yake alikuwa kipenzi cha Marekani lakini baadaye wakamfanyia kitu mbaya

Ni kweli kuwa Sugu ananguvu kubwa Mbeya mjini na mtaji wa kupendwa na watu lakini kusipokuwa na mizania sawa ya uchaguzi Sugu hawezi kutoboa jimbo la Mbeya regardless anaungwa mkono na USA
 
Ila kuwa mbunge kutoka chama cha upinzani moja ya faida yake ni kutoangaliwa nini umefanya katika jimbo lako yani upinzani unakubeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…