Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Jana asubuhi nilimtuma mtoto na shillingi 8,400 kununua sukari kilo tatu nikifahamu mteja wangu huwa ananiuzia sukari Tshs. 2,800 kwa kilo.

Mtoto alirudi mikono mitupu akanieleza kuwa sukari imepanda bei na sasa kilo moja ni Tsh. 3,500. Nilishtuka sana na mpaka sasa sijaamini.

Nina maswali yafuatayo kwa Serikali:

1. Ongezeko hili limesababishwa na nini?

2. Je, kama Serikali mlitoa taarifa kwa wananchi kuhusu ongezeko hili?

3. Je, mnajua wananchi wengi hawataimudu bei hii?

4. Je, Serikali haijui kuwa Wananchi tunakosa imani na Serikali yetu?

Ninaomba majibu ya maswali yangu.
 
Eti ulimtuma akanunue kwa mteja wako...
Hii ndo Kiswahili gani ss
 
Acheni kuitumia wenyewe watashusha bei
Mwenzako baharia hapa sukari syo mtumiaji sana kg 1 naweza kaa nayo mpaka miezi 3

Ova
 
Hoja zizingatiwe ndugu zangu naona mashambulizi yanaenda kwa mleta uzi
 
Acheni kuitumia wenyewe watashusha bei
Mwenzako baharia hapa sukari syo mtumiaji sana kg 1 naweza kaa nayo mpaka miezi 3

Ova
Sukari inatumika kwenye viwanda vya vinywaji tofaut tofauti, vitafunwa, Bia pia nadhani sasa wewe sukari unawezaje kuikwepa.
 
Mdogo mdogo, Bagamoyo sukari inaanza kurudisha mtaji wake kwa lazima.

Mafuta, ilikuwa hivi hivi, mshazoea...

Ngoja tuone kama wataandamana...
 
We bana unatupiga fix tu hapa. Kama ulitaka kusema habari za sukari kupanda bei ungesema tu sio kuanza la listori la kutunga.

We tangu sukari imepanda bei hujanunua sukari? Imepanda lini kwani na imelalamikiwa mara ngapi humu
 
Mtoto wako angeenda na kadi yako ya CCM angeuziwa kwa Bei ya 2,800.
Huu Ni muda muafaka wa kujiunga na CCM.
 
Sukari inatumika kwenye viwanda vya vinywaji tofaut tofauti, vitafunwa, Bia pia nadhani sasa wewe sukari unawezaje kuikwepa.
Hapo sasa ndiyo utumwa wa mbongo
Siku mbongo akigomea basi hao wapandishaji wataelewa nao

Ova
 
Back
Top Bottom