Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hali ya uzalishaji wa sukari katika viwanda saba nchini imeshuka hadi kufikia tani 1,000 kwa siku kutokana na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa kauli ya serikali leo Jumamosi kuhusu hali ya sukari nchini, Bashe amesema katika kukabiliana na uhaba wa sukari ambao sasa umefikia tani 30,000, serikali imetoa kibali kwa wenye viwanda kuagiza sukari tani 100,000 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 23 - 24 Januari mwaka huu.

“Uzalishaji wa sukari katika taifa kwa kipindi cha miaka mitatu uliendelea kuongezeka kiasi kwamba sugar gap kwa mwaka jana ilishuka mpaka kufika wastani wa tani 30,000 na mwaka huu tulitarajia kumaliza kabisa gap ya sukari katika Taifa letu.

Hata hivyo amesema kutokana na hatua zilizochukuliwa anaamini ifikapo katikati ya Februari hali ya upatikanaji wa sukari itaanza kurejea katika hali ya kawaida na kutokuwa na madhara yoyote.

Source - EATV
na iwe hivyo. maana hii imekuwa kero.

Miwa tunazalisha ya kutosha.
Viwanda tunavyo vingi.
1. BAGAMOYO SUGAR
2. KAGERA SUGAR
3.MTIBWA SUGAR
nk
Sasa kwanini sukari iwe bei juu??!

Usimamizi na ufuatiliaji ni jambo muhimu
 
MNAWAENDEKEZA TU HAO WAZALISHAJI WA NDANI, LENGO LAO NI KUSHUSHA UZALISHAJI ILI KUPANDISHA BEI.

NINGEKUWA RAISI WANANCHI WANGU ASINGEPATA TABU, BORA TUAGIZE NJE KULIKO KUTESA WANANCHI WANGU.
 
Moja ya sekta imefaidi nchi awamu ya sita ni SUKARI

Kwa nini sukari ya Zambia inazuiwa wakati hatuna uwezo wa uzalishaji kiasi kamba mnakomoa raia kwa kigezo cha kulinda bidhaa zetu huku wafanyabiashara wajanja wanfaidika kwa huo mpango kwa kuumiza raia?

Wakiamka wanajikuna kisha wanataja bei wanayotaka inakuwa hivyo.

Nchi zote zinazotuzunguka kilo ya sukari ni chini ya sh 3000 sisi tunakimbilia 5000

Mama amefungua nchi kwa ma cartel wa sukari

Kipi CCM wamefanya cha maana ktkmTaifa hili

Toka mama aingie kila kitu kimepanda maradufu ila hali nchi haipo ktk vita yoyote

Umeme nao ni anasa na hakuna juhudi yoyote ya kiongozi wa Taifa kuonesha yupo bega kwa bega na wananchi ndio kwanza anasema yeye yupo kimya

Watanzania katiba mpya ni muhimu kupata viomgozi bora watakaowajibika kwa wananchi na sio viongozi wanaowajibika kwenye chama.

20240121_081037.jpg
 
Miaka nenda miaka rudi bei ya Sukari inachezewa Tanzania mara utasikia sijui viwanda wamesimamisha uzalishaji watoe vibali mara utasikia Mvua nyingi ili mradi sarakasi zao zikubalike tu wakati Nakonde na Kasumulu sukari ni Tsh 2500...
Sukari Tanzania ni biashara ingine ya Madawa ya kulevya iliyojificha kwenye Vibali...
 
nchi kuongozwa na mwanamke, tena hapa africa, wa kiislamu (uislamu hauruhusu haya mambo ya mwanamke kuwa kichwa cha nyumba, ni watu wa chumbani , pambo la mume, not otherwise)
 
Ndio anakuongoza na huna lolote la kufanya kubadili hilo.
 
Moja ya sekta imefaidi nchi awamu ya sita ni SUKARI

Kwa nini sukari ya Zambia inazuiwa wakati hatuna uwezo wa uzalishaji kiasi kamba mnakomoa raia kwa kigezo cha kulinda bidhaa zetu huku wafanyabiashara wajanja wanfaidika kwa huo mpango kwa kuumiza raia?

Wakiamka wanajikuna kisha wanataja bei wanayotaka inakuwa hivyo.

Nchi zote zinazotuzunguka kilo ya sukari ni chini ya sh 3000 sisi tunakimbilia 5000

Mama amefungua nchi kwa ma cartel wa sukari

Kipi CCM wamefanya cha maana ktkmTaifa hili

Toka mama aingie kila kitu kimepanda maradufu ila hali nchi haipo ktk vita yoyote

Umeme nao ni anasa na hakuna juhudi yoyote ya kiongozi wa Taifa kuonesha yupo bega kwa bega na wananchi ndio kwanza anasema yeye yupo kimya

Watanzania katiba mpya ni muhimu kupata viomgozi bora watakaowajibika kwa wananchi na sio viongozi wanaowajibika kwenye chama.

View attachment 2878038
Umekosea sana kuweka Hilo lipicha hapo.
 
Mpaka mseme,bado hamjasema. Nchi imefunguka.
 
Lakini hizo nchi jirani haziongozwi na serikali ya JMT chini ya Chama cha Mapinduzi na wananchi wa huko sio watanzania.

Ni muda sasa wa wananchi kujiweka wenyewe ndani ya mzani, isijekuwa hata ‘stamina’ yetu katika kupata huduma zetu za msingi na haki iko chini ama pengine hatuna kabisa.

Siku zote mja hupata anachostahiki na sio anachotaka pekee.
 
Hussein,

Tanzania inaagiza kutoka nje ya nchi sukari, mafuta ya kula, mchele, ngano, mbogamboga, matunda, maziwa, nyama na samaki. Unajisifia nini Hussein?

Tanzania mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 710,000 kwa mwaka. Lakini zaidi ya Tani 420,000 ya sukari Tanzania inaagiza kutoka nje ya nchi. Tatizo.

Mahitaji ya mafuta ya kula Tanzania ni tani 570,000 wakati uzalishaji wa mafuta ya kula ni tani 250,000. Hivyo tani 320,000 tunaagiza nje. Tatizo kubwa.

Tanzania inanunua tani 863,000 za ngano kutoka nje ya nchi huku uzalishaji wa ndani wa zao la ngano ukiwa chini ya tani 100,000. Waziri wa kilimo upo tu?

Tanzania inaagiza kutoka nje mbolea zaidi ya tani 700,000. Wakati ambao mahitaji ya mbolea kwa mwaka Tanzania ni wastani wa tani 500,000.

Zaidi ya 99% mbolea Tanzania inaagizwa kutoka nje ya nchi, siyo za kutengeneza ndani. Hii inaathiri msimu wa uzalishaji kwa wakulima. Waziri hujui?

Tanzania ina ukubwa wa 947,303 km². Eneo lenye maji ni 6.4% ya ardhi yote. 46% ya ardhi yote Tanzania inafaa kwa kilimo (arable land).

Eneo ambalo limetumika kwa kilimo ni 24% ya eneo lote la ardhi ya. Tanzania inatumia zaidi ya TZS 1.3 trilioni kuagiza chakula kwa mwaka. Uzembe.

Miaka mitano (2014 hadi 2019) Tanzania iliagiza chakula kutoka nje chenye thamani ya TZS 7.74 trilioni. Ngano ikiwa ni 53.3%. Wahuni madarakani.

Nchi namba 30 kwa ukubwa wa ardhi Duniani (12 kwa ukubwa wa ardhi Afrika) inatumia TZS 1.3 trilioni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi? Hushangai?

75% ya mbegu Tanzania zinatoka nje ya nchi hasa mbegu za chakula kikubwa kwa watanzania wengi, mahindi. Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza.

Wizara ya Kilimo, wekezeni katika utafiti katika masuala ya bioteknolojia (biotech) na vituo 17 vya Utafiti wa Kilimo Tanzania, vipewe umuhimu.

Wizara ya Kilimo ilitenga Sh8 bolioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika vituo 17 vya TARI katika hekta 854. Vilijengwa?

Mbegu za mbogamboga zote 90% zinatoka nje ya nchi. Unajiuliza kazi ya Agricultural Seed Agency (ASA) ni nini? Kweli fedha za bajeti zinafika?

Wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) wanayo mashamba, kwanini hawazalishi mbegu ya msingi (foundation seed)?

Kwanini wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) waagaize mbegu za kilimo kutoka nje? Waziri upo ofisini tu? Unajiona sawa?

Haya ni mambo ya kufanyia kazi hapo Wizara ya Kilimo. Hiyo ni wizara yenye uti wa mgongo wa watanzania. Siyo wizara ya kufanyia mchezo.

Brigedia Mtikila, MMM.
 
Ndo maana vyuo vikuu tanzania matokeo ya wahitimu ni kama sifuri tu. Chuo cha kilimo kipo lakini hakuna matokeo kabisa
 
Awamu hii kufeli kumaanzia juu kabisa.

Chimbuko la tatizo ni huyo alie juu yao.
 
Kilimo sio kuuza magazeti
Tuna shahada za kilimo sio za propaganda
Huwezi kutuambia ati sukari ime pande bei kwa sababu ya mvua.
Kwani hii mvua ime nyesha muda gani?
Kama nchi ina jali watu wake kwanini serikali haikujihami kuagiza sukari nje ya nchi?
Huu ni mkakati wa juwaumiza wananchi kama kawaida ya Ccm.
 
Mimi ni mpenzi sana wa ITV habari

Bei ilipoanza waligonga hodi bodi ya sukari walipoulizwa mbona bei panda ovyo watu wameficha sukari?
wakajibu hakuna kama hicho ni shida ya uzalishaji na soon litarekebishika.

Hivi majuzi yuleyule mwenyekiti anaulizwa anasema wamefuatilia na wamedhihirisha kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wameficha sukari ili ipande bei wanayoona

Sasa unawaonya watu tushaumia. Natoka Shinyanga kg 6000sh sijui Mei watanunua sh ngapi Mungu wangu.

Embu kiongozi mmoja wa juu aseme neno kuhusu sukari pls.

Huyu mwenyekiti wa bodi alisema wameagiza sukari nje by Januari mwishoni tatizo linaisha ndio tunaelekea Januari mwishon sijui mwisho ipi alimaanisha.
 
Back
Top Bottom