Hussein,
Tanzania inaagiza kutoka nje ya nchi sukari, mafuta ya kula, mchele, ngano, mbogamboga, matunda, maziwa, nyama na samaki. Unajisifia nini Hussein?
Tanzania mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 710,000 kwa mwaka. Lakini zaidi ya Tani 420,000 ya sukari Tanzania inaagiza kutoka nje ya nchi. Tatizo.
Mahitaji ya mafuta ya kula Tanzania ni tani 570,000 wakati uzalishaji wa mafuta ya kula ni tani 250,000. Hivyo tani 320,000 tunaagiza nje. Tatizo kubwa.
Tanzania inanunua tani 863,000 za ngano kutoka nje ya nchi huku uzalishaji wa ndani wa zao la ngano ukiwa chini ya tani 100,000. Waziri wa kilimo upo tu?
Tanzania inaagiza kutoka nje mbolea zaidi ya tani 700,000. Wakati ambao mahitaji ya mbolea kwa mwaka Tanzania ni wastani wa tani 500,000.
Zaidi ya 99% mbolea Tanzania inaagizwa kutoka nje ya nchi, siyo za kutengeneza ndani. Hii inaathiri msimu wa uzalishaji kwa wakulima. Waziri hujui?
Tanzania ina ukubwa wa 947,303 km². Eneo lenye maji ni 6.4% ya ardhi yote. 46% ya ardhi yote Tanzania inafaa kwa kilimo (arable land).
Eneo ambalo limetumika kwa kilimo ni 24% ya eneo lote la ardhi ya. Tanzania inatumia zaidi ya TZS 1.3 trilioni kuagiza chakula kwa mwaka. Uzembe.
Miaka mitano (2014 hadi 2019) Tanzania iliagiza chakula kutoka nje chenye thamani ya TZS 7.74 trilioni. Ngano ikiwa ni 53.3%. Wahuni madarakani.
Nchi namba 30 kwa ukubwa wa ardhi Duniani (12 kwa ukubwa wa ardhi Afrika) inatumia TZS 1.3 trilioni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi? Hushangai?
75% ya mbegu Tanzania zinatoka nje ya nchi hasa mbegu za chakula kikubwa kwa watanzania wengi, mahindi. Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza.
Wizara ya Kilimo, wekezeni katika utafiti katika masuala ya bioteknolojia (biotech) na vituo 17 vya Utafiti wa Kilimo Tanzania, vipewe umuhimu.
Wizara ya Kilimo ilitenga Sh8 bolioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika vituo 17 vya TARI katika hekta 854. Vilijengwa?
Mbegu za mbogamboga zote 90% zinatoka nje ya nchi. Unajiuliza kazi ya Agricultural Seed Agency (ASA) ni nini? Kweli fedha za bajeti zinafika?
Wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) wanayo mashamba, kwanini hawazalishi mbegu ya msingi (foundation seed)?
Kwanini wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) waagaize mbegu za kilimo kutoka nje? Waziri upo ofisini tu? Unajiona sawa?
Haya ni mambo ya kufanyia kazi hapo Wizara ya Kilimo. Hiyo ni wizara yenye uti wa mgongo wa watanzania. Siyo wizara ya kufanyia mchezo.
Brigedia Mtikila, MMM.