Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Muwe mnakunywa supu sukari sio lazima matumizi mengine mbadala uwe chumvi kwa nilipo sukari IPO tele bei ni 3400/kg halafu ni kawaida kila mwaka viwanda vinasitisha uzalishaji kwa mda kufanya maintainance ya mitambo muwe mnasoma alama za nyakati sio kulialia
 
Bei elekezi ni sawa na corona.

Inaitwa elekezi. Bado natafuta maana yake. Ni bei inayopendekezwa au ni laizma iwe hivyo maadam mheshimiwa mmoja katamka?

Si tulishasema ni soko huria? Yaani mtu akauze chini ya bei aliyonunulia?

Sasa hivi itaingia nyingi ya magendo. Toka Jiwe aingie anaongelea viwanda vya sukari. Viko wapi? Kachemsha bila shaka.
 
3400 sio bei elekezi.. wakikamatwa laki 5 washike na meno!
 
Sukari imekua balaa sasaiv sukari hapa Dar bei ni 3500 ukienda Dukani wanasema wao hawawezi kuuza chini kwasababu ananunua bei ya juu...
 
Kiuchumi inafafanulikaje ulichoandika
Kiuchumi n kwamba bei ya bizaa sokoni asilimia kubwa inaamuliwa na wingi wa hiyo bidhaa na mahitaji. Tatzo sukari inayozalishwa nchini haitoshelezi mahitaji ya watanzania na pia huenda sukari inayoagizwa kutoka nje pia huenda n kidogo, hali hii ni lazima hii bizaa itakuwa juu kibei coz wanao ihitaji ni wengi. Pia hapa napo ndio wafanyabiashara wengi wanapopigia faida coz anajua sukari ipo kidogo nchini piga ua lazma atauza akiamua kuuza kwa bei ya juu. Solution serekali lazma iagize sukari kwa kiasi kinachotosha kujazia kiasi kilichopelea km mkakati wa haraka lkn la pili kuwepo na mkakati wa muda mrefu kuongeza production ku meet demand ikiwa possible tuuze nje pia. Unajua huwa najiuliza tatzo n nn katika uzakishaji wa sukari.. je n uzakishaji mdogo wa miwa?. Je ni gharama kubwa za uzalishaji hususani katika stage ya production baada ya uvunaji wa miwa au n nn.
 
Ahsante nimekuelewa.

Mashamba ya miwa yapo ila wanadai kipind hiki cha mvua inakua haina content ya sugar vyakutosha hivyo kupunguza uzalishaji.
Garama bado ni zilezile lakin ili sukari iwe kwny bei himilivu lazima iagizwe kutoka nje, sasa aibu ya hivi serikali hawaitaki bali wanataka kushinda kwa kukandamiza wafanyabiashara. Ma wafanyabiashara hawakubali.

Serikali ije na wazo jipya au sera mpya kwenye hili.
 
Umemuinua johnthebaptist ,yeye anakunywa chai na sukari ya kutosha
 
Ni takribani wiki sasa tangu bei elekezi ya sukari kuwekwa hadharani na serikali kupitia waziri mwenye dhamana.

Mimi nimemuuliza leo wife kwa Dada Rose (Mchaga) sukari kanunua kwa bei elekezi ya 2600 TSH, kasema hapana.
Je, huko mliko bei elekezi inazingatiwa?

Kama haizingatiwi je, serikali imeshindwa kusimamia hili?

Au serikali ilitoa bei elekezi bila kuzingatia mambo muhimu kama upatikanaji na uzalishaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…