Asalamaleko
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 2,699
- 7,726
Naona chawa upo kaziniTafuteni pesa vijana...
Tangia lini vitu vitamu vinapatikana kwa bei rahisi..?
K mnanunua tena kwa pesa ndefu ila sukari mnataka ipatikane rahisi..?
Kidumu chama tawala
Ukiandama kupinga kupanda bei ya sukari itabidi baadaye tena uandamane kupinga vifuatavyo:-Basi tuandamane kupinga kupanda kwa bei ya sukari
Mkuu.Huwezi pata akili kama hupitii nyakati ngumu.
Rebaging inafanyika kwa products nyingi sana za matumizi ya binadamu. Na wanaoumia n watumiaji wa mwisho. Ntakupa mfano, ngano inafanyiwa rebagging. Inavokuja from Dar, wenye uwezo wa kuagiza mende, wanaagiza, wanashusha, wanakua na mifuko yao wanachota kidogo kidogo lets say robo kilo kwa mfuko. Sasa mende ina mifuko lets say 2000 wat do u expect?What is this in Lower Middle Income Economy!? Alafu eti wanataka tujadili dira mpya ya taifa 2050!?
Huo mchezo mchafu wa ku-rebag products wanaufanya kampuni ya maziwa ya Tanga Fresh wakitumia maziwa ya ASAS, nyumbani kwangu nimeweka ban kutumia Tanga Fresh until further notice.
Kilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kufuata kutoka kwenye anguko hili.
Sababu tunayopewa ni dhaifu kwamba mashamba ya miwa yamefurika maji wakati TMA ilitoa tahadhari miezi 2 kabla ya mvua kushuka. Nadhani ni Tz pekee ambako mvua na jua ni laana isiyokoma kwa kilimo, umeme, maji, mifugo, uvuvi nikitaja kwa uchache.
Aidha, viwanda vya sukari vya Magereza vilivyojengwa kwa kasi ya mwanga hatujui vimefikia wapi baada ya kutumia fedha za umma kwenye ujenzi huo kama machinjio ya kisasa ya Vingunguti, Kibaha, Simiyu na Manyara vilivyobaki kuwa makumbusho ndani ya nchi ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika?
Tz sukari haijawahi kushuka kwa miaka 23 mfululizo tangu Julai 2001 licha ya mashamba ya miwa kuongezeka na viwanda vipya kujengwa Morogoro na Bagamoyo pamoja na uingizaji wa sukari ya nje ya nchi.
Tz sukari ni miongoni mwa bidhaa na huduma ambavyo vimekuwa vya kidemokrasia vikiwemo Korosho, Mafuta ya mitambo, Mafuta ya kula, Katani, Umeme na Maji.
Nchi kubwa, hali ya hewa ya kitropiki, mitambo ipo, rasilimaliwatu rahisi wapo, soko la ndani lipo lakini tumeshindwa hata kwenda kujifunza Uganda tu hapo namna ya kuendesha sekta ya sukari.
Ni kama vifuatavyo vyote 4 vimefeli jumla kwenye sekta ya sukari:-
1. Sheria ya Taifa ya Sukari 2001 (National Sugar Act 2001).
2. Taasisi ya Sukari Tz (National Sugar Institute).
3. Shirika la Maendeleo ya Sukari (Sugar Development Corporation SUDECO).
4. Makampuni ya Sukari (Sugar Factories).
NB.
1. Tz ina makampuni 5 ya sukari kwenye mikoa 4.
2. Kenya ina makampuni 16 ya sukari.
3. Uganda ina makampuni 14 ya sukari.
4. Zambia ina kiwanda cha sukari kikubwa kuliko vyote barani Afrika tangu 1964.
Uganda ina sukari kuzidi mahitaji ya ndani na hawajui wapeleke wapi ziada hadi waliwahi kuiomba Tz ichukuwe sukari yao hata kwa mkopo ili maghala yao yawe wazi kupokea uzalishaji mpya maana hawawezi kumwaga ziada ziwani.
Sasa mapapa wa biashara ya sukari wanapiga jaramba ili serikali iruhusu uagizaji toka nje ya jamhuri. Nadhani kwa spirit ya EAC serikali ichukuwe sukari ya Uganda ambayo nayo pia itapunguza bei kwa sababu ni jirani nasi kuliko kutoa sukari ng'ambo ya bahari. Let us think over and handle this matter strategically, progressively and proactively.
Bei ya sukari ikipanda vifuatavyo navyo vinapanda kwa sababu kuna aina nyingi za sukari zinazotengeneza bidhaa mbalimbali:-
1. Bei ya Soda kufuatia kupanda bei ya sukari.
2. Bei ya vitafunwa (mikate, maandazi, vitumbua, keki nk) kufuatia kupanda bei ya sukari.
3. Bei za madawa ya syrups kufuatia kupanda bei ya sukari.
4. Bei za sharubati kufuatia kupanda bei ya sukari.
5. Bei za sweets kufuatia kupanda bei ya sukari.
6. Bei ya wanzuki (inayotumia sukariguru) kufuatia kupanda bei ya sukari. Whatnot?
NB.
Miili yetu inapokea sukari kwa 99% ya vitu tunavyokula na kunywa hivyo sukari ni maisha (Sugar is Life)
Sir Richard Gordon Turnbull GCMG hakukosea kutumia viboko kutawala Tanganyika.
Vifuatavyo vyote 4 vimefeli jumla:-
1. National Sugar Act 2001.
2. National Sugar Institute.
3. Sugar Development Corporation SUDECO.
4. Sugar Factories.
NB.
1. Tz ina makampuni 5 ya sukari kwenye mikoa 4.
2. Kenya ina makampuni 16 ya sukari.
3. Uganda ina makampuni 14 ya sukari.
4. Zambia ina kiwanda cha sukari kikubwa kuliko vyote barani Afrika tangu 1964.
Ninachoshangaa ni kuwa hao hao wazungu waliobuni sukari wakisema ina umuhimu mkubwa kwa afya za wanadamu ndiyo hao hao leo wamegeuza kibao na kutuambia ni sweet poison.Usitumie sukari , sukari ni sweet poison
Zanzibar hamuhitaji sukari? Mwezi mtukufu sukari ni dhambi kwenye futari na daku? Inawezekana eti muungano ndiyo umeleta mvua nyingi zilizofurikisha mashamba ya miwa na sukari kuhadimika?Yote haya ni karma ya kuivamia Zanzibar na kuuwa maelfu ya watu , Muungano ni laana
Mkuu.BAGAMOYO SUGAR mnatuangusha!!
Ongezeni uzalishaji kisha punguzeni bei, mnaweza kuuza Kg.1 Shs. 2000/=. Kwakufanya hivyo naamini makampuni mengine pia watashusha bei bila kupenda.
Hata huvyo tunaiomba wizara ya Viwanda na Biashara kufuatilia upandaji bei kiholela wa bidhaa zote na ushibitiwe.
Zanzibar kiko kiwanda cha sukari , laana za muungano ni nyingi na laana kubwa ni kupata viongozi wasio na vision na weziZanzibar hamuhitaji sukari? Mwezi mtukufu sukari ni dhambi kwenye futari na daku? Inawezekana eti muungano ndiyo umeleta mvua nyingi zilizofurikisha mashamba ya miwa na sukari kuhadimika?
Kwa mtazamo huo! Kweli muungano ni laana nakubaliana nawe Jagina!
Ninachoshangaa ni kuwa hao hao wazungu waliobuni sukari wakisema ina umuhimu mkubwa kwa afya za wanadamu ndiyo hao hao leo wamegeuza kibao na kutuambia ni sweet poison.
Swiss asilimia kubwa ya GDP yake inategemea sweets ambazo zinatengenezwa na products za sukari. Swiss ni supplier mkubwa duniani wa sweets na wazungu ni wateja wakubwa wa sweets za Swiss.
Wazungu walituletea misahafu wakatuandikia kwamba ndoa za jinsia moja ni dhambi na serikali zetu zikatunga sheria dhidi ya ndoa za aina hiyo, leo wanarudi kwa mlango wa uani kutuambia ndoa za jinsia moja siyo dhambi na kwamba sheria na misahafu zibadilishwe ziruhusu ndoa hizo.
Kutegemea akili za wazungu kama Alpha na Omega iko siku watatuambia kuwa tuwatenge wake zetu maana wanachembechembe zinazofupisha maisha yetu wanaume ndiyo maana tunaishi muda mfupi kuliko wao wanawake.
Jamani tuchukuwe la nani tuache la nani?
Mwezi huu mwisho sukari inaingia kutoka Nje ,hakuna haja ya tamkoKilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kufuata kutoka kwenye anguko hili.