Sukari yafika shilingi 5,000 kwa kilo moja

Mbona kama naanza kumchukia huyu mama...sijawahi kumsema vibaya..ila anatafakarisha aisee..suala hili la sukari anashindwa kuagiza nje ya nchi kureplace damage iliyopo...ametulia kama hayuko Tanzania...
Anatafakarisha sio kidogo sukari ni bidhaa muhimu sana kwenye uchumi. Tusipo angalia hii hela yetu itapolomoka sana thamani ndani ya kipindi kifupi. Hata issue ya nauli alitakiwa aliangalie pia ila ndio ivyo lishapita hilo na hili la sukari litapita tu.
 
Anatafakarisha sio kidogo sukari ni bidhaa muhimu sana kwenye uchumi.
Tusipo angalia hii hela yetu itapolomoka sana thamani ndani ya kipindi kifupi.
Hata issue ya nauli alitakiwa aliangalie pia ila ndio ivyo lishapita hilo na hili la sukari litapita tu.
Inasikitisha kwakweli...
 
Ruvuma bei ya sukari jana ilikuwa 92000/-kwa mfuko wa 25kg!ina maana kwa mfuko wa 50kg ni 184000/-twafa!hakuna anaehangaika na wananchi wote wanawaza jinsi ya kurudi madarakani 2025,Shame on them
 
Mwezi huu mwisho sukari inaingia kutoka Nje ,hakuna haja ya tamko
Hawatashusha bei maana serikali haijaruzuku mapapa wa biashara ya sukari kama ilivyoruzuku mapapa wa mafuta ela zikaliwa na bado hawakushusha bei ya mafuta. Subiri utaniambia, nimekaa paleee...

Bei ya sukari haijashuka Tz Bara tangu Julai 2001 miaka 23, sasa leo itashushwa na nini na nani? Acha walete sukari toka nje bei itabaki hiyo hiyo 5000/
 
Hawatashusha bei maana serikali haijaruzuku mapapa wa biashara ya sukari kama ilivyoruzuku mapapa wa mafuta ela zikaliwa na bado hawakushusha bei ya mafuta. Subiri utaniambia, nimekaa paleee...

Bei ya sukari haijashuka TZ tangu Julai 2001 miaka 23, sasa leo itashushwa na nini na nani?.
Soko ndio litashusha na Serikali ndio Imetoa vibali vya kuingiza sukari tani 50,000
 
Mbona kama naanza kumchukia huyu mama...sijawahi kumsema vibaya..ila anatafakarisha aisee..suala hili la sukari anashindwa kuagiza nje ya nchi kureplace damage iliyopo...ametulia kama hayuko Tanzania...
Na mbona chumvi haijawahi kupungua? Wala viberiti? Lol!

Serikali iondoe ruzuku kwenye chumvi ihawilishe (ihamishie) kwenye sukari.
 
Kilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kufuata kutoka kwenye anguko hili.

Sababu tunayopewa ni dhaifu kwamba mashamba ya miwa yamefurika maji wakati TMA ilitoa tahadhari miezi 2 kabla ya mvua kushuka. Nadhani ni Tz pekee ambako mvua na jua ni laana isiyokoma kwa kilimo, umeme, maji, mifugo, uvuvi nikitaja kwa uchache.

Aidha, viwanda vya sukari vya Magereza vilivyojengwa kwa kasi ya mwanga hatujui vimefikia wapi baada ya kutumia fedha za umma kwenye ujenzi huo kama machinjio ya kisasa ya Vingunguti, Kibaha, Simiyu na Manyara vilivyobaki kuwa makumbusho ndani ya nchi ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika?

Tz sukari haijawahi kushuka kwa miaka 23 mfululizo tangu Julai 2001 licha ya mashamba ya miwa kuongezeka na viwanda vipya kujengwa Morogoro na Bagamoyo pamoja na uingizaji wa sukari ya nje ya nchi.

Tz sukari ni miongoni mwa bidhaa na huduma ambavyo vimekuwa vya kidemokrasia vikiwemo Korosho, Mafuta ya mitambo, Mafuta ya kula, Katani, Umeme na Maji.

Nchi kubwa, hali ya hewa ya kitropiki, mitambo ipo, rasilimaliwatu rahisi wapo, soko la ndani lipo lakini tumeshindwa hata kwenda kujifunza Uganda tu hapo namna ya kuendesha sekta ya sukari.

Ni kama vifuatavyo vyote 4 vimefeli jumla kwenye sekta ya sukari:-

1. Sheria ya Taifa ya Sukari 2001 (National Sugar Act 2001).

2. Taasisi ya Sukari Tz (National Sugar Institute).

3. Shirika la Maendeleo ya Sukari (Sugar Development Corporation SUDECO).

4. Makampuni ya Sukari (Sugar Factories).

NB.
1. Tz ina makampuni 5 ya sukari kwenye mikoa 4.

2. Kenya ina makampuni 16 ya sukari.

3. Uganda ina makampuni 14 ya sukari.

4. Zambia ina kiwanda cha sukari kikubwa kuliko vyote barani Afrika tangu 1964.

Uganda ina sukari kuzidi mahitaji ya ndani na hawajui wapeleke wapi ziada hadi waliwahi kuiomba Tz ichukuwe sukari yao hata kwa mkopo ili maghala yao yawe wazi kupokea uzalishaji mpya maana hawawezi kumwaga ziada ziwani.

Sasa mapapa wa biashara ya sukari wanapiga jaramba ili serikali iruhusu uagizaji toka nje ya jamhuri. Nadhani kwa spirit ya EAC serikali ichukuwe sukari ya Uganda ambayo nayo pia itapunguza bei kwa sababu ni jirani nasi kuliko kutoa sukari ng'ambo ya bahari. Let us think over and handle this matter strategically, progressively and proactively.

Bei ya sukari ikipanda vifuatavyo navyo vinapanda kwa sababu kuna aina nyingi za sukari zinazotengeneza bidhaa mbalimbali:-

1. Bei ya Soda kufuatia kupanda bei ya sukari.

2. Bei ya vitafunwa (mikate, maandazi, vitumbua, keki nk) kufuatia kupanda bei ya sukari.

3. Bei za madawa ya syrups kufuatia kupanda bei ya sukari.

4. Bei za sharubati kufuatia kupanda bei ya sukari.

5. Bei za sweets kufuatia kupanda bei ya sukari.

6. Bei ya wanzuki (inayotumia sukariguru) kufuatia kupanda bei ya sukari. Whatnot?

NB.
Miili yetu inapokea sukari kwa 99% ya vitu tunavyokula na kunywa hivyo sukari ni maisha (Sugar is Life)

Sir Richard Gordon Turnbull GCMG hakukosea kutumia viboko kutawala Tanganyika.
Seen.
 
Tarehe 24 tukutane samjoma Hadi ofisi za umoja wa mataifa
 
Waziri wa kilimoo nilikuwa naamini wew ni Genius imekuwaje tena????
 
Gonga like ambao hatutumii sukari.
Mtakamatika kwenye nyama, kilo 1 imetinga 12,000/

Mgahawa mmoja leo nimeomba mishikaki ya ng'ombe wakasema hapa tumeacha kuuza nyama ya ng'ombe na mbuzi, tuna-serve kuku wa kisasa tu maana hatuwezi bei ya nyama ya ng'ombe buchani.
 
Mpaka ifike 10K, ndio tutaelewa kwanini chadema wanaitisha maandamano!
 
Kwa.mwendo huu na ukondoo wetu, kuna siku si nyingi kilo ya sukari itafika laki mbili.

Majitu mazima eti ni vyama vya upinzani yanatumwa na CCM kuharibu mapambano haya. Leo hakuna umeme sijui yenyewe yana Tanesco ya kwao, yako Kwenye giza lkn kwa vile yamepewa suti za mitumba hayaoni nyuma wala mbele
 
Back
Top Bottom