Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,059
Mada nzuri, hongera!Sukuma gang ni itikadi liyoasisiwa na Magufuli inayoamini katika ukatili unaohusisha matusi, utekaji, uporaji, mauaji na uonevu.
Kwahiyo itikadi hii isihusishwe na kabila la Wasukuma. Mfano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ndugu Sabaya yeye ni Sukuma gang lakini siyo Msukuma. Wengine ni Polepole, Ndugai, Bashiru, Mnyeti, Happi, Kabudi, n.k.
Lakini wapo Wasukuma ambao pia ni wafuasi watiifu wa itikadi hii ya sukuma gang. Sina haja ya kuwataja.
Nimeandika haya ili kuondoa dhana inayotaka kujengwa na baadhi ya watu ama kwa upotoshaji wa makusudi au kwa bahati mbaya kuwa kuwachukia wafuasi wa Sukuma gang ni kuchukia Wasukuma. Hili siyo jambo zuri na kufanya hivyo ni kupanda mbegu ya ukabila.
Mm Sexless mwandishi wa uzi huu nawachukia Sukuma gang na muasisi wao ingawa nami ni Msukuma.
Lakini wanakuaje "itikadi" ndani ya 'CCM moja' halafu wawe tofauti na Msoga Gang, kwa mfano? Haiingii akilini.
Ina maana basi, kuna kitu zaidi ya "itikadi" kinachowaunganisha au kuwagombanisha - Sukuma vs Msoga.
Ni nini hicho? Ni MASLAHI binafsi tu.
Hayo makundi yako ndani ya CCM kwa miaka mingi, toka 1990s. Ni DNA ya CCM. Kundi "linaloshinda" likiingia serikalini huitwa "mtandao" - inakuwa ni zamu yao kula na kufisadi nchi. Ndio utamaduni wa CCM.
Lakini Magufuli alijaribu/aliubadili huo utamaduni - kuyaua na/au kuyasambaratisha makundi kinzani na lake; ila kabla hajakamilisha, akafariki. Sasa baadhi ya makundi yaliyokuwa bench na 'kuchapika' yamerudi kwa 'hasira'!
Ni ukweli kuwa kila linaangalia na kujali maslahi yake tu. Hakuna cha uzalendo wala cha maendeleo. Ni kula na kutesa kwa zamu.
Ndio maana tunataka Katiba Mpya. Haya magenge ni hatari sana kwa usalama na maendeleo ya nchi yetu