Wadau Nawasabahi
Nimekuwa nasikia kuna Kundi linaitwa SUKUMA GANG je Kundi hili ni la kina NANI?Je lina Lengo gani Uwepo wake?Je Ofisi zao zipo Wapi?Je Kiongozi wao ni NANI?
Na kwanini liitwe SUKUMA GANG je ni kwa Ajili ya Wasukuma tu? Mwenye UFAHAMU wa Kundi hii ATUJUZE.
Hilo kundi halipo na halijawahi kuwepo na halitakuwepo ni mkakati umesukwa na watu wachache ili kuua hoja mahususi za wananchi ikiwemo udhaifu wa baadhi ya mawaziri, kuua hoja za ziko wapi Bilioni 260 za CSR za Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, ziko wapi Trilioni 1 na ushee anazotakiwa kulipa Mkandarasi kwa kuchelewesha mradi.
Hoja za wakulima wengi kushindwa kulima kutokana na mfumko mkubwa wa bei ya mbolea hadi kufikia 140,000 na ushee kutoka 50,000 na mauchafu mengine mengine ndio wameunda huo msemo kama njia ya kunufaika na kutobainika udhaifu wao kiutendaji ili kupengeneza presha ionekane hawa watu wa Magufuli..
Ukitaka kuwakamata hao wanaotengeza huo uzushi waulize ni Nani aliyemuweka Mh Samia Suluhu Hassan kwenye nafasi ya Makamu wa Rais, na sasa ni RAIS wa JMT nani aliyemuweka Majaliwa kwenye uwaziri Mkuu, nani aliyemuweka Tulia Ackon kwenye Unaibu Spika na sasa Spika, nani aliyemuweka Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, nani aliyemuweka DGISS, nani aliyemuweka IGP, nani aliyemuweka CGI nani aliyemuweka Januari Makamba kwenye uwaziri kamili, nani aliyemuweka Nape kwenye uwaziri kamili.... kama kwanini hao wote hawaitwi Suguma Gang.
Kwanini kila siku watajwe Ndugai, Lukuvi, Kabudi, Polepole, Gwajima
Wambieni wajibu hizi hoja za kwanza za wananchi ndio turudi kuanza kujadili huo ujinga wao