Suluhisho la Kudumu la Mgogoro wa Maziwa Makuu (Rwanda, Congo et al) ni kutenga na kupata nchi ya hao waliopo hapo sasa (North Kivu)

Hakuna kabila linaitwa Watutsi wala Wahutu. Kabila lazima liwe na lugha yake. Hakuna lugha ya watusi. Watusi na Wahutu ni madaraja ya kijamii ( social classes). Madaraja haya utayakuta eneo lote la interlacustrine – Banyarwanda, Barundi, Baha, Banyankole, Bamushi, Basubi, Banyambo nk.


Je Jamii hizi zipo katika eneo linaloitwa sasa Kongo? Ndio. Himaya za Kirundi na Kinyarwanda zimekuwa Kongo miaka 500 kabla ya King Leopold kutwaa kilichokuja itwa Congo Free State na kabla ya mipaka ya Wakoloni ya mwaka 1884/1885.

Kabla ya Wakoloni kuja huku kwetu Himaya zetu zilikuwa zinavuka mipaka ya sasa. Ikiwemo Himaya ya Rwanda ( Rwanda Kingdom chini ya Mwami Rwabugiri ) ambayo ilikuwa maeneo yote ya Kivu ya Kaskazini na sehemu ya Kivu ya Kusini.


Sultan wa Zanzibar kwa mfano alikuwa anatawala Mashariki ya Kongo kupitia bwana Tipu Tippu makao makuu yake yakiwa Kindu Jimbo la Manyema. Ndio maana eneo kubwa la mashariki ya kongo wanaongea Kiswahili, swahiliphone, kwa sababu lilitawaliwa na Maliwali waswahili.

Ulichoandika hapa ni kitu kinaitwa conspiracies na sio historical facts. Kwa maandiko yako utakuja kusema watu wa Katanga, Kalemie, Moba, Manono, Kindu, Bukavu, Uvira, Baraka nk sio wakongo kwa sababu ni Swahiliphones. Kama unawatambua swahiliphones kama wakongo, vile vile rwandophones ni wakongo pia.


Mzizi wa fitna ni raia wote kupata haki zao sawa na majirani waache kuleta mizozo Kongo.

Kwa hiyo ondoa neno ukweli mchungu na weka neno nadharia za kikonsipirasi!
 
Shida yenu mnahisi kuonewa wakati nyinyi ndio wakorofi,sijui mtaacha lini kudeka.
Hata JK alivyo warudisha mlilalamika sana na kusema tuna Waonea sasabu wazee wenu walikuja Tz miaka mingi iliopita. Tungewachekea basi tungevuna mabua
 
Shida yenu mnahisi kuonewa wakati nyinyi ndio wakorofi,sijui mtaacha lini kudeka.
Hata JK alivyo warudisha mlilalamika sana na kusema tuna Waonea sasabu wazee wenu walikuja Tz miaka mingi iliopita. Tungewachekea basi tungevuna mabua
Myopic thinking kwa kusema watusi wa Kongo ni Wakongo na mimi nimeshakuwa Mtusi au mtu wa Rwanda ? Tatizo watu kama wewe kesho hamkiwii kusema kabila fulani liende kwenye mkoa fulani (ni mentality ambayo waliitumia sana wakoloni n kufanikiwa ) Divide and Rule...

Binafsi fikra zangu zimeshatoka huko siangalii ni nani, rangi gani au kabila gani linafanya nini bali ni nini kinafanyika na kama ni kibaya it does not matter nani anakifanya...; Kwahio wewe unaona ni sawa kwa mtu kusema watu wa aina fulani (no matter ni raia) basi warudi kule ambapo kuna watu kama wao wengi.... !????

And they say it's White Man I Should Fear..., But its My Own Kind Doing all the Killing Here...
 
Nadhani tukianza kusema sio Raia na kuwaonea na kutokuwapa Haki ambazo wanapewa Raia wengine huenda wangesema eneo la Upanga basi wabaki peke yao na mtu mweusi asipite kwa hofu kwamba anaweza kuwauwa (Mfano Mtikila alivyoanza issue za Gambachori that was dangerous) na kila Muhindi angeanza kutafuta bodyguard tusingewalaumu...; Kwahio tunapoangalia ubaya wa Kagame; Museveni na Serikali ya Congo huko Kinshasa tusiache kuangalia na hao waliopo hapo Congo ambapo pia ni kwao kuhakikisha wanaishi kama Binadamu / Wakongo wenzao; Ukitaka kujua shida au raha ya kitu jaribu kuvaa viatu vya muhusika.
 
Huwezi kugawa nchi Ili kufurahisha kundi fulani tu la kikabila.
 
ndicho kagame anachotafuta, na wakifanya hivyo hawatamaliza hata mwaka, wataungana na rwanda na kuwa nchi moja ili rwanda iongezeke kieneo na kiresources.
 
Una hoja ya msingi,
Congo igwanywe tu kwa sababu imeshindwa kutawalika kutokea Kinshasa, DRC Mashariki wapewe nchi yao.
Hakuna wa kuigawa Drc..
 
ndicho kagame anachotafuta, na wakifanya hivyo hawatamaliza hata mwaka, wataungana na rwanda na kuwa nchi moja ili rwanda iongezeke kieneo na kiresources.
Kuna tatizo gani ikiwa hivyo?
Mbona Russia wamechukua 20% ya Ukraine na hawajafanywa chochote?
 
Mkuu mimi sio mzoefu, naweza pia kuwa nakosea, ila ninavyofahamu vita vya M23 si sawa na vya nyuma,

Joseph Kabila alipendekeza Katiba mpya na hao jamaa walipewa haki yao ya kura na mambo mengine, Banyamulenge ambao nao pia asili yao ni Rwanda wakawa Upande wa Kabila na hata ilipoanzishwa M23 Banyamulenge wakakataa kuunga mkono, japo wanateswa na Wao ila atleast hawa unaweza uka elewa struggle zao na namna wanavyolinda Ethnicity yao.

Issue ya watutsi ni kutaka wao kuwa superior, kwamba wao mazungumzo ni wao kuwa na power na Wengine wote waliopo ni kama hawana shida.
 
Yani masharti ya kugawa hilo eneo ni kuwapa Watutsi kama Viongozi, so hata likigawanywa ina maana hutawasaidia wa kazi wa Kivu, pengine wakachezea kichapo kuliko cha sasa, watapata tabu kama wanazopata Wanyarwanda.

Uhuru wa Kweli ni kuwapa watu wa Kivu wenyewe ambao wapo hapo miaka nenda miaka rudi,
 
Trump hajaivamia Greenland na Panama kama Kagame na Putin walivyovamia jirani zao
Greenland wakianza kupigania mpakani mwa Marekani atavamia.
 
Greenland wakianza kupigania mpakani mwa Marekani atavamia.
Huu ni mtazamo wako tu, sio lazima iwe hivyo na kwanini wapigane ?...

Magenge ya wauza unga wa Mexico yanapigana yenyewe kwa yenyewe mpakani mwa Mexico na Marekani ila Marekani hajaivamia Mexico.

Kagame kavamia Drc Ili na kuivuruga hiyo nchi kwa manufaa yake binafsi na wanasiasa wenzake wachache.
 
Mkuu, mwafrika akili zake anazijua mwenyewe. Sudan walipigana mpaka wakatenga Sudan mbili. Ajabu ile Sudan ya Kusini baada ya kuwa nchi, wakashindwana wao kwa wao na sasa wanapigana.
Unajifunza kuwa tatizo siyo nchi, tatizo ni maslahi binafsi ya viongozi wa pande zisizokubaliana.

Ndiyo maana hata hapa kwetu utasikia Tanganyika iwe nchi na zanzibar iwe nchi kamili then kuwe na federal government, so what??? Yaani imagine mimi niliyezaliwa Tanzania nianze kuidai nchi ya Tanganyika ambayo hata siijui ilikuwa inafananaje. So sad

Mtoa hoja anafikiri, wakipewa kipande cha kile wanachoona ni chao, ndiyo machafuko yatatulia. jambo ambalo sio sahihi ukirejea kesi ya sudan kusini nk
 
Mexico kuna wakati huwa inaruhusu Task Forces za DEA kuingia kufanya operations baadhi ya maeneo, pia DRC imekuwa na vita tangu enzi za Mobutu wakati Rwanda ikiwa na viongozi wajinga wajinga.
 
Mexico kuna wakati huwa inaruhusu Task Forces za DEA kuingia kufanya operations baadhi ya maeneo, pia DRC imekuwa na vita tangu enzi za Mobutu wakati Rwanda ikiwa na viongozi wajinga wajinga.
Mexico inafanya hayo kwa ridhaa yake, huo sio uvamizi

Ila Kagame kaivamia Drc na kuteka ardhi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…