Suluhisho la Kudumu la Mgogoro wa Maziwa Makuu (Rwanda, Congo et al) ni kutenga na kupata nchi ya hao waliopo hapo sasa (North Kivu)

Nope sijasema itakuwa sawa na matatizo yatakwisha sababu alternative ni watu kutambuliwa kama wananchi wa Congo; na kupata nafasi za nchi yao hio ya Congo kama wengine, Je hio unadhani itakuwa rahisi kwa watu ambao wenzao wanawaona kama mamluki ? Binafsi mimi naona hizi mali ni mambo ya kupita ila Amani, Uhuru na Maisha ya Usalama ya wananchi waliopo pale (wote jamii zote ikiwemo Watusi) ni ya maana sana; na mpaka sasa inaonekana Serikali yao Congo (ambayo ipo Kinshasa) wamewaacha kama watoto yatima; na Serikali mbalimbali zimekuwa zikiwatumia tu kama nyezo (mfano Kabila Kuchukua nchi) na Mobutu kuwapa nafasi kwenye Serikali akijua kwamba muda wowote anaweza akawageuka kutokana na hatred ya Jamii nyingine dhidi yao.
 
Hamna cha kujitenga wala nini, hiyo Ardhi ni Congo na ubaki kuwa Congo.Sio wao pekee waliogawanywa makabila mengi Afrika yaligawanya, butvwatu wa-remove on..wao Watusi wana-uspecial gani?
1.Watusi wa Congo waheshimu na kutii mamlaka ya Congo bila kuonekana kama pandikizi
2.Serikali ya Congo iheshimu raiavwake unconditionally
3.Serikali ya Congo iache kuwasaidia FDRL - Waasi wa Rwanda walioko Congo
4.Rwanda waache kuwasaidia M23 - Waasi watusi - Wacongo.
5.Kila nchi iheshimu mipaka yake ma ihakikishe isitengeneze mazingira ya nchi nyingine kushambuliwa kutoka kwao - wasifadhili vikundi vyote vya waasi.
6.Kagane na Rwanda yake atambue kuwa Watusi waliochini ya dhamana yake ni Watusi Wanyarwanda, sio Watusi Wacongo, Watusi Waganda, Watusi Watanzania n.k.
7.Kagame akijiona yeye ndo Messiah wa Watusi basi watangaze programmes za kuwarudisha nyumbani kama Wayahudi au wabadirishe uraia na ijulikane moja kuwa ni Watusi Wanyarwanda.
Mbona hatuskii Wamasai wa Kenya au Tz wakijitambulisha either way, huku kusini kuna makabila kibao yalikatwa katikati lkn wanaendelea na maisha...
 
Mimi kwangu hizi zote ni perceptions; haiwezi kuondoa ukweli kuwa suluhisho unalojaribu kuliadvocate ni hatri zaidi ya changamoto iliyopo sasa.

Hap kwetu mambo ni tofauti kidogo, tumejenga umoja wa kitaifa mkubwa na kuruhusu mwingiliano mkubwa baina ya watu wa kabila moja na jengine.

Bahati mbaya kuhusu watu pro tusti sio wa kuchangamana na wengine sana. Hii ndiyo haiba yao, kwa maoni yangu ili DRC iwe salama lazima na wao wabadili mtazamo unless nchi hii itatafunwa na vita miaka nenda rudi. Hata sasa sio mwisho, kumbuka Rais Tshesekedi hatakubali nchi yake igawiwe kipande, vita itaanza upya na lengo itakuwa wao kuondolewa Goma, (kumbuka huko nyuma wamewahi kushikilia Goma kwa wiki) kabla ya kushindwa.

Lakini mwisho, maslahi binafsi ya viongozi ndiyo kitu pekee kinachoitafuna DRC. Ndiyo maana Rais wa M23 ndite aliyekuwa Chair wa Tume ya Uchaguzi aliyemtangaza Rais wa sasa, wakashindwana na haya yametokea….
 
Epuka Sana kukaribisha wageni kwenye ukoo, wakija ni wapole watazaliana wanaongezeka wataanza kumaliza kizazi Cha wazawa. Warudi walipotoka
 
Je unaona hayo yanaweza kutokea ? Pia kwa kufanya hivyo nadhani ni kufukia moto kwa majani makavu ukifikiri sababu hauonekani basi umeuzima; Hata wewe kwa upande wako unaweza ukawapa fair consideration watu ambao unaona ni mamluki kwako ? Na baadhi wamekuwa wakitumiwa kama Kete ya kubadilisha Uongozi (refer Kabila); Ofcource hayo yangefanyika ya Wacongo wote kushirikiana na kujenga nchi yao ingekuwa ndio bora zaidi ila kinachoonekana ni kama baadhi ya wananchi wao wamegeuka kuwa Yatima na kusahaulika na watu wa mataifa ya mbali na karibu kugeuza hio nchi kama sehemu ya kujichotea na kufanya uharibifu...

Nachojaribu kusema Congo ni kubwa sana na hayo mamisitu ni ngumu sana kuweza kuendeshwa from the centre wanahitaji decentralization ya hali ya juu; Na mpaka sasa hakuna mzuri hapo sio Serikali Kinshasha wala hao wanaoibia nchi; Lakini Je hawa raia wanaoendelea kutaabika wakati nchi yao ni tajiri inakuwaje ? What is the easiest immediate alternative.
 
Epuka Sana kukaribisha wageni kwenye ukoo, wakija ni wapole watazaliana wanaongezeka wataanza kumaliza kizazi Cha wazawa. Warudi walipotoka
What if walipotoka kwa wengine ndio hapo hapo ?; Na hatari zaidi kuna wengine kama wao huko mbali ambao wataendelea kuwatembelea ndugu zao na hivyo kuongezeka. Kwahio kama wote hawawezi kuishi kama binadamu kwa ustaarabu tunafanyaje kuwafukuza ambapo hatuwezi kuwafukuza wote (wengine wapo tangia enzi na enzi) au tunawakaribisha wawe kama sisi (ambapo huenda hatutaki kufanya hivyo sababu tunaona sio wenzetu)...

Now what gives ?
 
Loh
 
Kweli kabisa.Kama ilivyopatikana South Sudan.

..kilio ni Watutsi kunyimwa haki zao Congo.

..basi Rwanda iunganishwe ili kuwa jimbo la Congo.

..malalamiko kwamba wanafukuzwa Congo yatakwisha

..shutuma kwamba wanaiba madini ya Congo zitakuwa hazina nguvu maana sasa watakuwa raia halali wa Congo.

..hofu kwamba Congo inataka kumegwa au kugawanywa nayo itaondoka.
 
Huna unalojua wewe Bwege


Mbona kagame hataki kupatana na Wahutu wanaoishi Congo. Watu wako uhamishoni zaidi ya miaka 30 na nchi Yao ni Rwanda ila hawataki ila anataka watusi ambao ni asili yake wapewe nafasi congo.
 
Huna unalojua wewe Bwege


Mbona kagame hataki kupatana na Wahutu wanaoishi Congo. Watu wako uhamishoni zaidi ya miaka 30 na nchi Yao ni Rwanda ila hawataki ila anataka watusi ambao ni asili yake wapewe nafasi congo.
Hapo Kivu waliopo ni Watusi pekee ?
Hakuna makabila mengine ?
Hii kitu huwezi kuiangalia kwa jicho la Kagame au yoyote atakayekuja kesho au keshokutwa; hao ni watu wa kupita ila kama kuna tensions na hazijawa resolved lazima anytime zinaweza zikarudi tena;

Kwahio option kubwa na ya maana ni kwa Congo kuwaangalia raia wake wote wa Congo na kuhakikisha wote wanapata hati na kulindwa sasa kama the centre Kinshasha imeshindwa kutetea na kulinda raia wake wa huku maybe its about time hao waweze kujitegemea na kutumia rasilimali zao kuweza kujilinda na kujinufaisha na sio kubakia kichaka cha waasi ambao wanazaliwa kila leo au kutumiwa kama nyenzo za watu kupata madaraka...
 
Agent wa Kagame yupo kwene INFORMATION WARFARE
 
..kilio ni Watutsi kunyimwa haki zao Congo.
Sio watusi pekee dunia hii chini ya jua haipaswi binadamu yoyote aishi sehemu kama second citizen kama ana uraia either uwe wa makaratasi (legally) au kuanzia ancestors wake kama walikuwepo hapo; kwahio Congo needs to take a hard look at themselves na kuhakikisha the country is protecting their own..., Na kama hawawezi (no systems in place) maybe wawaachie hao ambao wanapata dhahama wajaribu kutumia rasilimali zao pamoja na kujilinda (Saudi Arabia iliweza kutumia rasilimali zake na kujizatiti kijeshi) if that was a good move or not that's another argument
..basi Rwanda iunganishwe ili kuwa jimbo la Congo.
Kwa kutumia hoja gani ? angalau Tanzania tungeweza kusema kwamba Rwanda na Burundi zote zilikuwa ni Deutsch-Ostafrik kwahio tunaweza kuwa na Hoja; kuna hao waliopo hapo watusi wao wanasema mipaka iliwakuta kwahio hapo ni Kwao (sio Rwanda)... Mwisho kabisa tusiangalie hili kwa jicho la Rwanda, Uganda na Congo, tuliangalie kwa jicho la raia anayehangaika hapo kila siku kwa vita visivyoisha na nchi yake / makazi kuwa kichaka cha waasi wasiokwisha..., Mtu huyu na sio Mtusi pekee pale makabila yote yaliyopo hapo anahitaji kuangaliwa na kulindwa na nchi yake (Congo) sasa kama inashindwa kufanya hivyo hatuwezi kusema two wrongs makes a right (wote kuanzia M23, waasi wote na wote wanaosababisha sintofahamu waache kufanya hivyo)
..malalamiko kwamba wanafukuzwa Congo yatakwisha
Kwahio unaona hapo kutakuwa hakuna malalamiko kwamba Congo imechukua Taifa lingine ?; Binafsi naona hata asimilation ya watusi kwenye serikali ya Congo ni jambo gumu sana. Tayari kuna watu wanaona kwamba hawa ni enemy within (sasa unaweza vipi kuwaunganisha)? Ndio maana kuna siku nilisema Hata mgogoro wa ndugu zetu Watusi na Wahutu kwa faida ya vizazi vijavyo waanze kuhakikisha / kuhamasisha intermarriages za kufa mtu...

..shutuma kwamba wanaiba madini ya Congo zitakuwa hazina nguvu maana sasa watakuwa raia halali wa Congo.
Huwezi kuzuia baya moja kwa kutafuta baya jingine kama hawa ni wezi wa madini kwanini wasihakikishe wizi huo unakwisha ? Je ni Rwanda na Uganda pekee ndio wanaiba au hilo ni shamba la bibi kila mtu anajizolea hata maitaifa ya mbali
..hofu kwamba Congo inataka kumegwa au kugawanywa nayo itaondoka.
Congo should take care of their own (all of them) kama hawawezi from the centre (Kinshasha) then maybe they need to find an alternative (for the sake of people at the countries vicinities)
 
Agent wa Kagame yupo kwene INFORMATION WARFARE
Hii ndio definition ya Vioja... au naweza kusema Divide and Rule ya Mkoloni bado ipo kwenye fikra zako (kwa kuona wengine ni maadui) by the way nchi ni zaidi ya mtu mmoja (huyu Kagame next 20 years atakuwa hayupo) ila bila ku sort hili jambo litaendelea kututafuna (na hapo nime kututafuna sio kimakosa ni kwamba nchi zote za maziwa makuu zinapata athari na destabilization iliyopo huko)

By the way Kivu kuna watusi pekee ?
 

..kila upande unawanyooshea wengine kidole na kuwashutumu.

..Watutsi wanalalamika kwamba wanatengwa na kunyimwa haki zao kama Wacongo.


..Wacongo nao wanalalamika kwamba Watutsi wanajiona ni Wanyarwanda, na hawako loyal kwa Congo.

..Kwa hiyo kila upande uangalie umemkosea nini mwenzake ili waweze kuishi pamoja kwa amani, na upendo.

..Kila upande katika huu mgogoro una watu wazuri, na watu wabaya wakatili na wauwaji.
 
..kila upande unawanyooshea wengine kidole na kuwashutumu.
Which means watu hawa ni vigumu kuendelea kukaa kama ndugu sababu hawana imani na kila upande hivyo sisi kama third party inabidi tuangalie ni vipi tunaweza kuwasaidia ndugu zetu wasiendelee kupigana bali kujenga nchi yao na hio ni pamoja na kuangalia Hoja na Madai kama ni reasonable na workable...
..Watutsi wanalalamika kwamba wanatengwa na kunyimwa haki zao kama Wacongo.
Je kuna ukweli wa hili ? Kama ndio je ni kuna uwezekano wa kuweza kuacha kutengwa na watu wanaokuona wewe sio loyal ? Je Congo haina wajibu ya kuwalinda hawa raia wao ambao ni watusi, pia tukumbuke kwamba hapo Kivu sio kwamba ni watusi pekee kuna makabila mengine..., Pia huenda ikitokea machafuko Rwanda wengi zaidi hata ambao sio wacongo watakimbilia hapo sababu kuna watu wenye tamaduni sawa kama wao (na hili lazima litaleta tension zaidi) Kuna siku nilisema hawa watu Hususan Rwanda na Burundi wangejifunza kutoka Tanzania ingawa wameshachelewa ila sio mbaya kuanza mapema ndio maana kuna siku nilisema watu wajifunze kutoka Tanzania

..Wacongo nao wanalalamika kwamba Watutsi wanajiona ni Wanyarwanda, na hawako loyal kwa Congo.
Naam ndio maana nasema ni vigumu sana watusi hawa kuwa assimilated kwenye positions za kubwa kubwa za Congo ingawa wacongo wasio watusi huwa wanawatumia pale wakitaka kupindua Serikali kama Kabila na hata Mobutu aliwatumia kwa kuwapa position akijua hawatamsaliti na aliwafanya nyenzo ya kuwabana wengine.

Kwahio utaona hapo kwa Congo kuwakubali 100 percent kuwa assimilate (watusi) ni vigumu sana, and with good reason (huwezi kuwapa position watu ambao unawaona ni wasaliti); pili kwa Congo kuwatumia wale ambao Rwanda wanadhani wanataka kupindua Serikali ni obvious Rwanda ita support watu wanaopigana nao (hata wasingekuwa watusi)... (that is a good reason; Action and Reaction are equal and opposite)

Kwahio sisi majirani (Big Brothers inabidi tutafute suluhisho la kudumu); what is a long term solution which is practical na sio kuendelea ku postpone the inevitability ? Huyu Kagame tunayesema ni mbaya alitengenezwa na matukio ya 1959 (kwao pangekuwa safe wala asingekuwa mkimbizi).
..Kwa hiyo kila upande uangalie umemkosea nini mwenzake ili waweze kuishi pamoja kwa amani, na upendo.

..Kila upande katika huu mgogoro una watu wazuri, na watu wabaya wakatili na wauwaji.
Pia kuna mazingira yanayosababisha hao wabaya, wakatili na wauwaji kuweza ku survive na ku nourish..., that place is a failed state na kama Congo haiwezi kuwalinda raia wake wa hapo na kuendelea kusababisha mazao ya waasi maybe its about time wanyanyue mikono, leo ni M23 kesho watakuja wengine, na kila anayetaka madaraka anawatumia hawa watu kama ngazi ya kupanda kwenda kupata ulaji
 

..hatua ya kwanza ni pande zote kuweka silaha zao chini.

..hatua ya pili ni Watutsi kutambuliwa kuwa wao ni raia wa DRC.

..Watutsi nao wawe loyal kwa Congo na kuacha kujichukulia kama Wanyarwanda.

..Rwanda ihakikishiwe ulinzi kwa vikosi neutral visivyotokana na majirani wa Rwanda na DRC kulinda mpaka wa nchi hizo.

..DRC iache kuwasaidia Fdlr, na Rwanda iache kuwasaidia M23.
 

..Congo tayari iko decentralized.

..wana mfumo wa utawala wa majimbo.

..hivi m23 haiwezi kuwa chama cha siasa?

..Wacongo wahimizwe kutafuta political solution, na sio military solution, au kuigawa DRC vipande.

..Na sio kwamba DRC ni kubwa mno, na haitawaliki.

..Maeneo yote ya DRC yana amani isipokuwa North Kivu ambako Rwanda inafadhili maasi.
 
kwan huu mgogoro si ulianza miaka 1990s je kabla ya hapo walikuwa wanabaguliwa pia maana hawakuwa na agenda zozote , huez baguliwa kama ww ni mwenyej , kuna namna hao ni wageni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…