Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Ati????Unaunga mkono au unalaumu wanaodhulumiwa?? Ulimsikia katibu mkuu wa umoja wa mataifa alivojaribu kusema ukweli jana??? Mpaka Israel wamesema watawanyima visa viongozi wa umoja wa mataifa.
Walianzisha vita mwenyewe Acha wakipate . Wote ni migaidi na inapenda kufa. Tache kulialia.
 
🤣🤣🤣�Sasa huyo Mungu unaemsema anasema hivi sikiliza...
Kama ningeamua kumuadhibu kila anaefanya dhambi asingebaki binadamu yoyote hapo duniani ila kila mja ana muda wake wa kuondoka..

UNAPOONGEA FIKILIA KAKA
 
kwa taarifa tu israel ina maeneo makubwa haishii palestina tu ni mpaka nchi za jordan, syria, lebanon, misri mpaka ghuba ya uajemi. Ikiamua kujititimua kupanua maeneo yake waarabu watajikuta wako ndani ya israel. Walianza na palestina kidogokidogo. Misri anaujua muziki wa israel ikabidi asaini mkataba wa amani tu atulie, na hao wengine wanajua hilo. Kikubwa wasiwachokoze waisrael wakae kwa amani kufuata mipaka ya kimataifa iliyowekwa iheshimiwe. Israel ni nchi kubwa ile na wanajijua mipaka yao hasa inaishia wapi. Usishangae kuna mataifa ya ulaya na afrika yamo ndani ya israel kama wakiamua kuliamsha dude kutaka maeneo yao ya enzi za mababu zao
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
Udini...
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
Purely atheist ideas! kwa wale wanaoamini monotheism or Abrahamic religions ( judeism, christianity & islam) huwa wanajua kwamba, kuomba Mungu ni sehemu ya ibada, sio lazima upate kile unachotaka au kwa wakati ule unaotaka kwa sisi watu wa maombi tunajua! Baadhi ya walokole mfano, TB joshua na wengine wanajaribu kuonesha tofauti lkn hata hivyo wakati mwingine wanaangukia pua!
 
Siku zote Waisraeli wakimkaidi Mungu waliadhibiwa kwa kupelekwa utumwani Babylon, na mwaka 135 AD wakatawanywa Ulaya na maeneo mengine, lakini pia aliahidi kuwarudisha, na atakapowarudisha(1948),hakuna atakayewatawanya. Soma Amos 9:15.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wakitulia si ndo wanaswagwa wote kama mang'ombe na kuondolewa ktk hiyo ardhi. Kwani huji kuwa Israel haitaki hata kusikia kitu kinachoitwa ONE STATE SOLUTION?
 
What if waliorudi ni wapinga Kristo ili kuandaa ujio wa Kristo wa kweli ambaye atarudisha Wayahudi real?
 
What if waliorudi ni wapinga Kristo ili kuandaa ujio wa Kristo wa kweli ambaye atarudisha Wayahudi real?
Kwa hiyo Nabii Amos mwongo? Je Nabii Zakaria 12:2-3 mwongo? Kama hao ni waongo, basi Quran 5:21 Allah Mungu wa Wapalestina alisema nchi iliyoitwa Kanani walipewa Waisraeli, naye mwongo? Hamas wakae kwa kutulia vinginevyo kipondo kitaendelea mpaka wasambaratike, hiyo vita hawawezi kushinda kwa sababu hatima ya eneo Hilo inajulikana ni ya Waisraeli.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alkna Faiza watakuja na mambo yao ya kimu jahidina, huku wenzao wanakula kichapo
 
Haya masuala yamo kwenye historia yameandikwa uzuri ni kutafuta muda mzuri na kusoma kisha kufanya uchambuzi wako na kufikia hitimisho.
Asante mkuu, 'Richard', kwa kuchukua muda wako kutoa somo kama unavyolielewa wewe, nami kwa mengi ninakubaliana nawe.
Haya ni matatizo yaliyosababishwa, na yanaendelea kuchochewa na haya mataifa ya nje kwa manufaa ya mataifa hayo.
Kwa maelezo yako, ambayo ni kweli, kwamba wayahudi walikuwa wametapakaa sehemu mbalimbali huko nchi za Ulaya, nisilojua vizuri ni kama hapakuwepo na myahudi yeyote hapo ilipo Israel leo hadi walipomegewa kipande na waingereza. Kama ni hivyo, kutakuwa na swali pia, kwa nini waingereza waliona sehemu hiyo ndilo eneo walilotakiwa kuwepo wayahudi. Kuna taarifa nyingine husemwa kwamba moja ya eneo lililofikiriwa kupewa wayahudi ni Uganda (sina hakika na hili).
Je, inawezekana kwamba eneo lile wayahudi waliwahi kuishi hapo na kwa sababu mbalimbali za matukio, wakajikuta baadae wamesambaa kwingine duniani. Habari za maandiko ya vitabuni, ya kidini, historia hiyo ni kweli? Tunajua uwepo wa miji kama Jerusalem na maeneo mengine, ambayo ni wazi yanaonyesha uwepo wa watu hao katika maeneo hayo nyakati hizo za zamani.

Binafsi naamini kwamba, si Hamas, Iran, au hata Israel yenyewe watakaodai na kuwezesha kuondoka kwa mmoja kati ya waPalestina na waIsrael. Hakuna tena kwenye dunia ya leo kulisambaratisha moja kwa moja taifa moja dhidi ya jingine. hawa wakubwa wa dunia leo wanahangaika na maslahi yao, lakini kama ilivyokuwa kwa Himaya nyinginezo zilizopita, hawa wa leo na wao siku zao zinahesabika tu.

Kwa hiyo, la msingi, ni kutafuta njia ya usuluhishi, ili kila taifa liishi katika mipaka yake, na kuheshimu mipaka ya wengine.
Iran hata awe na uwezo kiasi gani, hawezi tena kumwondoa Israel hapo alipo. Kujiapiza kulifuta taifa hilo, ni kujidanganya; kama watakavyojidanganya Israel, kwa kudhani wanaweza kuishi kwa amani kwa kuwakandamiza waPalestina. Haiwezekani.
 
Yaan wewe ndio ungetakiwa ulete hii mada maana umeelezea kwa hali halisi
 
Nadharia yako hii ndipo ubovu unapoanzia, kusema kwamba wapalestina wakae kwa upole hata kama wanakandamizwa.
Hakuna binaadam yeyote aliyewahi kukubali jambo kama hilo milele. Kama mPalestina ataigiza kuwa mpole kwa sasa, kama unavyosema, kuna wakati na kizazi kitakachokataa hali hiyo.
Suluhisho unalolenga wewe ni kwa waIsrael kuwamaliza waPalestina wote, ili Israel aishi hapo kwa amani; lakini unashindwa kutambua kwamba waPalestina wapo duniani kote, kama walivyowahi kuwa wayahudi wenyewe.

Unachosema hapa wewe, katika picha pana zaidi ya kidunia, kuwa hata hizi nchi zetu maskini tukubali tu kila wanachotaka wakubwa kifanyike, kwa vile kukataa kwetu kutaishia kuwa na maumivu ya milele kwetu.
Sikubaliani na nadharia hiyo hata kidogo.
 
Duh!

Haya ya warumi na maandiko ya kwenye hivi vitabu vya kidini kwa kweli mimi siyajui, kwa hiyo siwezi kuyasemea hapa leo. Ninachosema, bila ya kujali hivyo vitabu, haya ya leo yanahitaji utatuzi kufuatana na hali ya leo.
Hata hivyo, nakushukuru kwa hilo somo la historia ya "Warumi, mwaka 133 AD", nilikuwa siijui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…