Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza

Ati????Unaunga mkono au unalaumu wanaodhulumiwa?? Ulimsikia katibu mkuu wa umoja wa mataifa alivojaribu kusema ukweli jana??? Mpaka Israel wamesema watawanyima visa viongozi wa umoja wa mataifa.
Walianzisha vita mwenyewe Acha wakipate . Wote ni migaidi na inapenda kufa. Tache kulialia.
 
kwa taarifa tu israel ina maeneo makubwa haishii palestina tu ni mpaka nchi za jordan, syria, lebanon, misri mpaka ghuba ya uajemi. Ikiamua kujititimua kupanua maeneo yake waarabu watajikuta wako ndani ya israel. Walianza na palestina kidogokidogo. Misri anaujua muziki wa israel ikabidi asaini mkataba wa amani tu atulie, na hao wengine wanajua hilo. Kikubwa wasiwachokoze waisrael wakae kwa amani kufuata mipaka ya kimataifa iliyowekwa iheshimiwe. Israel ni nchi kubwa ile na wanajijua mipaka yao hasa inaishia wapi. Usishangae kuna mataifa ya ulaya na afrika yamo ndani ya israel kama wakiamua kuliamsha dude kutaka maeneo yao ya enzi za mababu zao
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
Udini...
 
Ila Allah kweli kama yupo angeshawakomboa wapalestina zamani. Anavyoabudiwa kwa nidhamu, mashindano na kutajwatajwa kila wakati kwa ajili ya wapalestina yani angeshaifutilia mbali taifa teule Israel.
Purely atheist ideas! kwa wale wanaoamini monotheism or Abrahamic religions ( judeism, christianity & islam) huwa wanajua kwamba, kuomba Mungu ni sehemu ya ibada, sio lazima upate kile unachotaka au kwa wakati ule unaotaka kwa sisi watu wa maombi tunajua! Baadhi ya walokole mfano, TB joshua na wengine wanajaribu kuonesha tofauti lkn hata hivyo wakati mwingine wanaangukia pua!
 
Mungu akiwarejesha sio USA wala UK na Mungu akiwarudisha wala haitohitajika vita bali mazingira yataandaliwa!!

Biblia gani hiyo unasoma? Unajitafsiria unabii juu juu tu. Waliambiwa wasipomtii watatandikwa tu kama unabisha kasome kabila la Dani lilivyopotezewa na Mungu
Siku zote Waisraeli wakimkaidi Mungu waliadhibiwa kwa kupelekwa utumwani Babylon, na mwaka 135 AD wakatawanywa Ulaya na maeneo mengine, lakini pia aliahidi kuwarudisha, na atakapowarudisha(1948),hakuna atakayewatawanya. Soma Amos 9:15.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wakitulia si ndo wanaswagwa wote kama mang'ombe na kuondolewa ktk hiyo ardhi. Kwani huji kuwa Israel haitaki hata kusikia kitu kinachoitwa ONE STATE SOLUTION?
 
Siku zote Waisraeli wakimkaidi Mungu waliadhibiwa kwa kupelekwa utumwani Babylon, na mwaka 135 AD wakatawanywa Ulaya na maeneo mengine, lakini pia aliahidi kuwarudisha, na atakapowarudisha(1948),hakuna atakayewatawanya. Soma Amos 9:15.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
What if waliorudi ni wapinga Kristo ili kuandaa ujio wa Kristo wa kweli ambaye atarudisha Wayahudi real?
 
What if waliorudi ni wapinga Kristo ili kuandaa ujio wa Kristo wa kweli ambaye atarudisha Wayahudi real?
Kwa hiyo Nabii Amos mwongo? Je Nabii Zakaria 12:2-3 mwongo? Kama hao ni waongo, basi Quran 5:21 Allah Mungu wa Wapalestina alisema nchi iliyoitwa Kanani walipewa Waisraeli, naye mwongo? Hamas wakae kwa kutulia vinginevyo kipondo kitaendelea mpaka wasambaratike, hiyo vita hawawezi kushinda kwa sababu hatima ya eneo Hilo inajulikana ni ya Waisraeli.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ubishi, ukaidi na ujeuri wa wapalestina kutaka kupambana na Israel itapelekea maafa na mateso zaidi kwa watu wasiokuwa na hatia. Ama kwa kupenda au kutokupenda, suluhisho rahisi na lenye kuleta amani mashariki ya kati ni wapalestina kuwa watulivu ili waendelee kukaa pale kwa amani au kuhama kabisa maeneo yale ili kuepusha shari zaidi.

Hizi choko choko za vikundi vya Hamas nk. ni kujilisha upepo na kuongeza mateso, hazina msaada wowote endelevu kwa wapalestina. Wapalestina wakae wakijua, hakuna nchi ya kiarabu itajiingiza kichwa kichwa kuwapigania pale, sio Iran, Lebanon, Syria, Egypt, Jordan au Saudi Arabia ambayo ina muda, nguvu, rasimali au dhamira ya dhati ya kwenda moja kwa moja kuwapigania wapalestina, kila taifa linapambana na hali yake tu.

Hilo eneo la Gaza hapo mashariki ya kati ni dogo sana, kavu mnoo, halina rasilimali zozote muhimu za kiuchumi ukiachilia hizi blah blah za kiimani ambazo zinatumika na pande zote kinafiki tu na kimchongo ili kujitengenezea uhalali wa kumiliki hayo maeneo kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria.

Sasa kwanini watu wakae kwa wagombana?
Kwani dunia haina sehemu zingine za kuishi?
Kuna raha gani kuishi katika hali hiyo?

Unaweza kusema au kuwaza kuwa kwanini waisraeli wao wasihamishwe pale? Jibu ni moja tu, Israel kwa sehemu kubwa ndio inapamiliki pale kwa sasa (iwe kwa haki au mabavu), Israel haina muda wa kuchokoza wapalestina ili iendelee kukaa pale bali ina dhamira, muda na nguvu za kutaka kuwakandamiza zaidi na kuwatuliza vilivyo ikiwa wapalestina watataka kuendelea kubakia pale.

Kama kuna wafia dini huku duniani wanaoona ni lazima kuendelea kupigana vita pale mashariki ya kati basi waende wao pale kwa vivuli vya dini yao kupigana na sio kutumia wapalestina kama chambo.

Note:
Taifa la Palestina lina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti tofauti wakiwemo waislamu (97%) na wakristo (3%), wakati taifa la Israel nalo lina waumini wa kiyahudi (81%), waislamu (14%), dini za asili (3%) na wakristo (2%). Lakini kote huko kwa hayo mataifa na hao waumini ukichunguza utagundua miongoni mwao kuna wapagani na wahuni kibao, hivyo tusilazimishe hii vita kuwa ni vita ya kidini wakati ni siasa na tamaa tu.

TUMECHOKA NA VITA
HATUTAKI VITA
Alkna Faiza watakuja na mambo yao ya kimu jahidina, huku wenzao wanakula kichapo
 
Haya masuala yamo kwenye historia yameandikwa uzuri ni kutafuta muda mzuri na kusoma kisha kufanya uchambuzi wako na kufikia hitimisho.
Asante mkuu, 'Richard', kwa kuchukua muda wako kutoa somo kama unavyolielewa wewe, nami kwa mengi ninakubaliana nawe.
Haya ni matatizo yaliyosababishwa, na yanaendelea kuchochewa na haya mataifa ya nje kwa manufaa ya mataifa hayo.
Kwa maelezo yako, ambayo ni kweli, kwamba wayahudi walikuwa wametapakaa sehemu mbalimbali huko nchi za Ulaya, nisilojua vizuri ni kama hapakuwepo na myahudi yeyote hapo ilipo Israel leo hadi walipomegewa kipande na waingereza. Kama ni hivyo, kutakuwa na swali pia, kwa nini waingereza waliona sehemu hiyo ndilo eneo walilotakiwa kuwepo wayahudi. Kuna taarifa nyingine husemwa kwamba moja ya eneo lililofikiriwa kupewa wayahudi ni Uganda (sina hakika na hili).
Je, inawezekana kwamba eneo lile wayahudi waliwahi kuishi hapo na kwa sababu mbalimbali za matukio, wakajikuta baadae wamesambaa kwingine duniani. Habari za maandiko ya vitabuni, ya kidini, historia hiyo ni kweli? Tunajua uwepo wa miji kama Jerusalem na maeneo mengine, ambayo ni wazi yanaonyesha uwepo wa watu hao katika maeneo hayo nyakati hizo za zamani.

Binafsi naamini kwamba, si Hamas, Iran, au hata Israel yenyewe watakaodai na kuwezesha kuondoka kwa mmoja kati ya waPalestina na waIsrael. Hakuna tena kwenye dunia ya leo kulisambaratisha moja kwa moja taifa moja dhidi ya jingine. hawa wakubwa wa dunia leo wanahangaika na maslahi yao, lakini kama ilivyokuwa kwa Himaya nyinginezo zilizopita, hawa wa leo na wao siku zao zinahesabika tu.

Kwa hiyo, la msingi, ni kutafuta njia ya usuluhishi, ili kila taifa liishi katika mipaka yake, na kuheshimu mipaka ya wengine.
Iran hata awe na uwezo kiasi gani, hawezi tena kumwondoa Israel hapo alipo. Kujiapiza kulifuta taifa hilo, ni kujidanganya; kama watakavyojidanganya Israel, kwa kudhani wanaweza kuishi kwa amani kwa kuwakandamiza waPalestina. Haiwezekani.
 
Tufikirie pia nje ya boksi.

Kuna matatizo makubwa matatu.

1. Mataifa mawili Israeli na Palestina kurasimishwa na kutambuliwa kimataifa. Hapa tatizo ni kwamba Hamas wana msimamo (na imeandikwa kwenye vitabu vyao) kwamba hakuna taifa liitwalo Israeli ndani ya ardhi ya mpalestina ambayo ni Uingereza kwa hila zao waliwapa wale walowezi na wahamiaji wa kutoka Ulaya.

Tukumbuke kwamba wakati wa machafuko huko Ulaya nyakati za akina Adolf Hitler kuwasaka hawa wayahudi wa Ulaya (Wayahudi wa ulaya ni kutoka Poland, Lithuania, Romania na nchi zingine ndogondogo) wengi walikimbilia hapo palestina ilokuwa chini ya mwingereza ambae alianza kuwaruhusu kuwa na ardhi.

Palestina ilikua chini ya uangalizi wa Uingereza (Palestine Mandate under UK) baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia ambapo Uingereza iliwashinda waturuki wa Himaya ya Ottoman na kuchukua sehemu hiyo.

Hivyo hapo mleta mada wakosea sana unaposema mpalestina aondoke kwenye ardhi yake.

2. Paletina kuwa ni sehemu ya kistratejia kwa mataifa ya magharibi. Hii haisemwi sana lakini ndo inotakiwa kuwa sababu namba moja kwani haka kasehemu ka Gaza kana hifadhi kubwa ya gesi asilia ambayo ndo yamezewa mate na mataifa haya khasa Marekani na Uingereza. Palestina ikiachwa yenyewe ijitawale na ifanye maamuzi yake kama taifa kamili basi itakuwa rahisi kuwavuta nchi kama Iran, Syria na hatimae kuwakaribisha nchi kubwa za Russia na China katika ukanda wake wa bahari ya Mediterranean.

3. Mpango wa Marekani kuishambulia Iran ili kuhodhi ukanda mzima wa Ghuba. Marekani imekuwa kwa muda mrefu ikijianda kuishambulia Iran ambayo sasa hivi imejizatiti kwa kuwa na mitambo imara ya ulinzi (ADS) dhidi ya mashambulizi yoyote ya Marekani.

Msingi mkubwa wa vita ya kuu ya pili ya Dunia ulikuwa ni kwa Marekani kuhakikisha inatawala hifadhi ya nishati katika eneo lote la Mashariki ya kati na Magharibi mwa Asia. Iran ina hifadhi kubwa ya mafuta na gesi asilia na pia kijiografia ipo sehemu nzuri ya kimkakati ikiwa katikati ya Afghanistan, Pakistan, sehemu ya India, Asia ya kati na mfereji wa Hormuz.

Huu mfereji wa Hormuz ndo asilimia 25 ya nishati yapita hapa kwenda Ulaya na Marekani lakini ni Iran ndo kikwazo kwa mataifa ya magharibi na taifa mteja la Israeli ( Client State) kwani Iran khasa baada ya mapinduzi ya 1979 bado ni taifa huru na Iran yatishia usalama wa taifa la Israeli na mstakabali mzima wa kuhodhi sehemu hiyo ya ghuba. Pia Iran yatishia matumizi ya Dola ya Marekani pamoja na nguvu yake ya kijeshi.

Iran mpaka sasa imejiendeleza na kutengeneza mifumo imara ya kiusalama kiasi cha kuweza kuzizuia Marekani na Israeli kuifanyia mashambulizi ya moja kwa moja kama walofanya kwa Irak na Afghanistan. Iran ina makombora ya maafa marefu na yale ya masafa mafupi (ballistic and cruise missiles) ambayo mengine yaweza kutua Israeli na kusini mwa bara la Ulaya.

Jambo hili pia latiliwa mkazo na Iran kujiunga na nchi za Urusi, China na Korea Kaskazini katika kupambana na Marekani na mataifa ya magharibi. Hivyo hapo harakati zote ni kutafuta sababu ili Iran ijiingize kwenye huu mgogoro lakini yashindikana kwani Iran ipo chini ya mwongozo wa Urusi na China.

Hizi ni sababu chache tu ambazo zaweza kukupa mwanga kwamba Israeli yupo katika kufanya kazi alotumwa na Marekani ambayo kwa mbali ameweka meli zake mbili za kivita katika bahari ya Mediterranean.

Ndo nikasema katika mada kadhaa humu kwamba huu ni mpango maalum kwa kuhakikisha wale walowezi wa Israeli ambao ni kizazi cha wale walowezi waloteka na kuchukua ardhi baada ya vita kuu ya 1967 ( Six Days War) na ambao wengi wamo kwenye baraza la mawaziri wa Benjamini Netanyahu, sasa hivi wataka kuchukua ardhi zaidi upande wa kaskazini wa Ukanda wa Magharibi jambo ambalo limestukiwa na wapalestina.

Haya masuala yamo kwenye historia yameandikwa uzuri ni kutafuta muda mzuri na kusoma kisha kufanya uchambuzi wako na kufikia hitimisho.
Yaan wewe ndio ungetakiwa ulete hii mada maana umeelezea kwa hali halisi
 
Asante sana kwa kunijibu kwa hekima na kujenga hoja muhimu.

Mimi nimesema ili amani iwepo pasipo kutaka kuchimba nani mwenye haki na nani mbaya. Choko choko yoyote ya kivita inayoanzishwa na wapelestina inapelekea kufa kwa waisrael wachache zaidi lakini inaishia kufa kwa wapalestina wengi wengi, Israel kuchukua eneo kubwa zaidi, miji mingi ya wapalestina kukaliwa kimabavu na mateso ya kimaisha kuzidishwa maradufu.

Sote tunajua kwa sasa Israel
1. Ametawala eneo kubwa.
2. Ana nguvu kubwa ya kijeshi.
3. Amedhamiria kuangamiza kila kimelea wa Hamas
4. Hana tena huruma wala simile dhidi ya mpalestina yoyote anasimama mbele yake kupambana naye.
5. Amepata sababu ya kutaka kulifuta kabisa taifa la Palestina kwa mtutu wa bunduki pale Gaza.

Sasa katika mazingira hayo, nini suluhisho la amani pale Gaza?
Kuendelea kulaani tu?
Wapalestina kuendelea kukaza shingo?

Dawa ni wapalestina wakae kwa utulivu pale Gaza (wakose uhuru lakini amani waipate) ama wahame kabisa Gaza (wakose makazi yao ya asili lakini maisha yao yaendelee popote).
Nadharia yako hii ndipo ubovu unapoanzia, kusema kwamba wapalestina wakae kwa upole hata kama wanakandamizwa.
Hakuna binaadam yeyote aliyewahi kukubali jambo kama hilo milele. Kama mPalestina ataigiza kuwa mpole kwa sasa, kama unavyosema, kuna wakati na kizazi kitakachokataa hali hiyo.
Suluhisho unalolenga wewe ni kwa waIsrael kuwamaliza waPalestina wote, ili Israel aishi hapo kwa amani; lakini unashindwa kutambua kwamba waPalestina wapo duniani kote, kama walivyowahi kuwa wayahudi wenyewe.

Unachosema hapa wewe, katika picha pana zaidi ya kidunia, kuwa hata hizi nchi zetu maskini tukubali tu kila wanachotaka wakubwa kifanyike, kwa vile kukataa kwetu kutaishia kuwa na maumivu ya milele kwetu.
Sikubaliani na nadharia hiyo hata kidogo.
 
Umepoteza muda tu kuleta mada ndegu kama hiyo. Allah ambaye ni Mungu wa Hamas ameshawaambia kwenye Quran 5:21 kuwa nchi iliyoitwa Kanani walipewa Waisraeli. Waisraeli walipigwa na Warumi mwaka 133 AD na kutawanywa, mwaka 1948 walirudi kwenye nchi yao, Hamas wapishe, labda Quran 5:21 nayo ibadilishwe iseme nchi hiyo ni ya Hamas.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Duh!

Haya ya warumi na maandiko ya kwenye hivi vitabu vya kidini kwa kweli mimi siyajui, kwa hiyo siwezi kuyasemea hapa leo. Ninachosema, bila ya kujali hivyo vitabu, haya ya leo yanahitaji utatuzi kufuatana na hali ya leo.
Hata hivyo, nakushukuru kwa hilo somo la historia ya "Warumi, mwaka 133 AD", nilikuwa siijui.
 
Back
Top Bottom