Haya masuala yamo kwenye historia yameandikwa uzuri ni kutafuta muda mzuri na kusoma kisha kufanya uchambuzi wako na kufikia hitimisho.
Asante mkuu, 'Richard', kwa kuchukua muda wako kutoa somo kama unavyolielewa wewe, nami kwa mengi ninakubaliana nawe.
Haya ni matatizo yaliyosababishwa, na yanaendelea kuchochewa na haya mataifa ya nje kwa manufaa ya mataifa hayo.
Kwa maelezo yako, ambayo ni kweli, kwamba wayahudi walikuwa wametapakaa sehemu mbalimbali huko nchi za Ulaya, nisilojua vizuri ni kama hapakuwepo na myahudi yeyote hapo ilipo Israel leo hadi walipomegewa kipande na waingereza. Kama ni hivyo, kutakuwa na swali pia, kwa nini waingereza waliona sehemu hiyo ndilo eneo walilotakiwa kuwepo wayahudi. Kuna taarifa nyingine husemwa kwamba moja ya eneo lililofikiriwa kupewa wayahudi ni Uganda (sina hakika na hili).
Je, inawezekana kwamba eneo lile wayahudi waliwahi kuishi hapo na kwa sababu mbalimbali za matukio, wakajikuta baadae wamesambaa kwingine duniani. Habari za maandiko ya vitabuni, ya kidini, historia hiyo ni kweli? Tunajua uwepo wa miji kama Jerusalem na maeneo mengine, ambayo ni wazi yanaonyesha uwepo wa watu hao katika maeneo hayo nyakati hizo za zamani.
Binafsi naamini kwamba, si Hamas, Iran, au hata Israel yenyewe watakaodai na kuwezesha kuondoka kwa mmoja kati ya waPalestina na waIsrael. Hakuna tena kwenye dunia ya leo kulisambaratisha moja kwa moja taifa moja dhidi ya jingine. hawa wakubwa wa dunia leo wanahangaika na maslahi yao, lakini kama ilivyokuwa kwa Himaya nyinginezo zilizopita, hawa wa leo na wao siku zao zinahesabika tu.
Kwa hiyo, la msingi, ni kutafuta njia ya usuluhishi, ili kila taifa liishi katika mipaka yake, na kuheshimu mipaka ya wengine.
Iran hata awe na uwezo kiasi gani, hawezi tena kumwondoa Israel hapo alipo. Kujiapiza kulifuta taifa hilo, ni kujidanganya; kama watakavyojidanganya Israel, kwa kudhani wanaweza kuishi kwa amani kwa kuwakandamiza waPalestina. Haiwezekani.