1. Kama ni suluhisho basi Waizraili nao waondoke maeneo hayo na sio Wapalestina pekee.
2. Unazungumzia chokochoko za Hamas na kuwasahau wanaowasaidia Waizrail ambao ni akina Marekani na washirika wake. Hili hujaliona?
3. Pamoja na kuhitaji msaada, Wapalestina wanapigania haki yao ya kuishi bila kujali watasaidiwa na nchi yoyote iwayo.
4. Ukisema eneo la Ghaza ni dogo hivyo Wapalestina wasilipiganie, huo udogo haubadiliki kuwa ni ukubwa kwa Israel kulipigania kwa nguvu zote. Udogo unapaswa kuonekana na pande zote na sio Wapalestina pekee. Hili nalo ulijue.
5. Ukisema Israel ndio wanamiliki Ghaza kwa namna yoyote, wengine wanasema Wapalestina ndio wanamilki Ghaza ndo sababu kubwa wanalipigania.
6. Ikiwa Israel ina dhamira na nguvu ya kuwakandamiza Wapalestina, kama unavodai, waendelee kufanya hivyo na Wapaestina wataendelea kuipigania ardhi hiyo hadi mwisho.
7. Hakuna wafia dini, kama unavyodai, wanaotaka vita iendelee ila kinachotakiwa ni kupatikana haki kwa kila upande.
8. Ni kweli tumechoka na vita na hatutaki vita. Maneno haya yanapaswa kuonekana kwa vitendo na moyo wa dhati kuanzia kusema, kuandika na katika nyanja zote. Uzi huu hauna sifa hizo. Kwa hivyo nadhani yanasemwa mdomoni, yanaadikwa makaratasini huku kukiwa hakuna imani ya kinachosemwa na kinachoandikwa. Au ndo ule msemo wetu Waswahili "mkuki kwa ngurue, kwa binadamu mchungu?"