Supu ya pweza inanimalizia hela nashindwa kuiacha

Supu ya pweza inanimalizia hela nashindwa kuiacha

Jumlisha na seringeti 2 au 3 ili kushushia mambo! Starehe gharama. Hakikisha na nyumbani unaacha maokoto sio kujipendelea mwenyewe. Haya sasa piga hesabu kwa mwezi. Labda uwe mfanyakzi wa TRA au traffic wa barabarani.
 
😂
 
Inategemea ni wapi umepita ukaona au umeenda kula bibie...

Sijawahi kula kwasababu ya hayo mazingira yake...kila nakopita sijawahi kuona ule 'ustaarabu' wa hata kufunika...nzi kwao wanafukuzwa kwa kuwapepea 🤦‍♀️
 
Za jioni wakuu, supu ya pweza ni maarufu sana Dar es salaam mida ya jioni ambapo tunaona watu wanauza supu kwenye vimeza vyao.

Sasa kitu kinachofanya nije leo ni ulevi wa supu ya pweza aisee nimejitahidi kuacha nimeshindwa yaani kila nikitoka kazini njia ya kwenda nyumbani kuna kibanda cha pweza kama wana dawa vile hawa watu unasema ninywe supu ya mia tatu ,mara unapiga kachori, paap kata mkia wa elfu mbili, weka na prawn puuh elfu tano imeenda.

Nikaamua nipige hesabu kila nikila pweza niandike kwenye google notes aiseee nimekuja kupiga hesabu mwezi december 2023 nimetumia elfu 65600 ukichezesha mwaka mzima kama laki 7 hv jamani si Tv mpya hiii.
Nifanyeje niache huu ulevi wa supu ya mdudu pweza.

Tushee experience walevi wenzangu
Punguza uwe unakula mchuzi wa buku, wanakuwekea na kipande cha mkia,, pia badala ya KILA siku.. fanya KWa wiki mara 3... Ambaa nayo hiyo ratiba,, badae unapunguza tena mwisho wa siku itakuwa unakunywa mara moja au mbili KILA baada ya wiki 2 au mwezi. ..
 
Kikubwa siyo pombe wala mihadarati, we endelea tu! Pia fikiria kuongeza kipato chako.
Mi kinachonisumbua ni magemu 😂 yani kwa wiki namaliza zaidi ya 20k kisa fc24
 
mi nimekuelewa unazungumzia gharama na sio shida supu ya pweza kwanza pole sana utaacha mwenyewe maana tayari mpaka hapo gharama zimeanza kukushinda na umetumia 65600 ambayo ni sawa na 2186 kwa siku mi nabet na sina mpango wa kuacha mwaka jana jumla ya pesa niliyolost ni M.13 .66 na bado staki hata kushauriwa.
 
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom