Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Hujanijibu swali langu.

Ukifuata common sense kuprove uwepo wa mungu kuna mahala common sense inakupinga.
 
Hujanijibu swali langu.

Ukifuata common sense kuprove uwepo wa mungu kuna mahala common sense inakupinga.
Jibu lipo humo humo..
Kuna mahali walimpeleka mzinzi apigwe mawe.. Wakaambiwa ambaye hana dhambi aanze kumpiga.. Wakaondoka hapo mmoja mmoja...Huoni hapo ilitumika common sense..!!!

Wewe unachotaka ni kuprove.. Common sense haina proof.. Ni sense..!
Kama ukiiba hufeel chochote ndani yako hakuna namna ninaweza prove kuiba ni mbaya..!
 
Hakuna namna unaweza kuhakiki uwepo wa mungu nje ya misingi ya kiimani.

Zaidi ya hapo ni porojo tu.
 
Ni kweli Mungu mwenye sifa hizo hawezi kuwepo labda kama utataka kumpunguzia hizo sifa (ambapo hatakuwa tofauti na sisi) ili aweze ku fit kwenye dhana ya
Mwenye sifa zipi?
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo, ukiondoka kwenye maelezo matupu ya siyo na uthibitisho?

Maana kama ni kupiga hadithi tu, hata mimi naweza kukuambia kwamba kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.

Naweza kukuambia mimi ndiye Mungu, wewe huwezi kujua tu.

Je, hilo linanifanya niwe Mungu?

Pembetatu duara itakuwepo?

Mimi kusema hivyo hakufanyi pembetatu hiyo iwepo.

Au naweza kusema kuna mtu anaitwa Shokolokabangoshee ni balozi wa dunia nzima.

Wakati mtu huyo hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya hayupo, hoja ya kuwepo kwake inqjipinga yenyewe.

Na zaidi ya huyo, hujaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu mwingine yeyote.
 
Ukishakuwa Kipofu..hakuna namna ninaweza kukuhakikishia kuna Mwanga..!
Kipofu haoni lakini akisimama juani atahisi joto la jua.

Ndio hapa huwa mnaishia mkikosa facts ambazo hazipo ndani ya imani, wengi wenu ni vijembe, nahau za kiswahili wengine huwa ni matusi n.k lakini nilijibu vizuri tu kwamba imani ni imani, sayansi ni sayansi.

Kutaka kutumia sayansi kwenye imani haiwezekani au vice versa.

Jioni njema.
 
Hakuna namna unaweza kuhakiki uwepo wa mungu nje ya misingi ya kiimani.

Zaidi ya hapo ni porojo tu.
Imani unaweza kuamini chochote, hata uongo.

Sasa utajuaje unachoamini ni kweli kama unakwenda kwa misingi ya imani tu?
 
Aisee vijembe tena.. hatari kweli.. Akisimama juani atahisi joto la jua..
Usiku akisimama pembeni ya moto atahisi!!!? Sio kila joto ni la jua.. Na sio kila jua lina joto..
Mimi naongelea kuona.. Wewe kuhisi.. Hatari tupu..!

Ikija mambo ya MUNGU hakuna sehemu ya Sayansi wala Imani.. Ni Common Sense..!
Sijaelewa kwanini unakimbilia kwenye imani wakati mimi siamini..!
 
Hata huo moto unatoa mwanga ndio maana anahisi joto.
 
Hata huo moto unatoa mwanga ndio maana anahisi joto.
Whaaaat.. Kipofu changamoto yake ni kuhisi au kuona..!!?
Kwahiyo nikichukua pasi ya moto nikaweka karibu yake.. Lile joto atasema ni mwanga wa jua au wa mshumaa..!!?
Sio kila moto una mwanga..!!!
 
Nachojua tunajadili contradiction.
Contradiction ni errors inayojitokeza katika mchakato wa kuthibitisha na ndio maana hata mifano yako haijakltoka nje ya dhana hiyo
 
Kwa sababu ni mwisho wa uwezo wetu wa kufikiri kama mwanadamu.
Unajuaje mwisho wa kufikiri kama mwanadamu uko wapi kwa kufikiri kama mwanadamu?

That's against Godel's Incompleteness Theorems.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…