Kwa nini unafikiri swali lako ni muhimu na si off point?
Nikiamini, nisipoamini, kama Mungu yupo, yupo tu, kama hayupo, hayupo tu.
Pia, naweza kuamini Mungu yupo, akawa hayupo, na naweza kuamini Mungu hayupo, akawa yupo.
Sasa kwa nini kuamini kuwe jambo la muhimu, wakati hakutusogezi popote?
Kwa nini tunaangalia imani badala ya facts?
Kwa nini unaniuliza naamini Mungu, badala ya kuniuliza nina facts gani tuzijadili?
Sasa kwa nini unquliza kama mimi naamini Mungu yupo?
Umekubali hata asiyeamini ana haki ya, na anapaswa kuhoji?
Kwa nini kuamini kuwe kitu muhimu wakati mtu anaweza kuamini uongo?
Kama kweli Mungu hayupo, na mimi siamini yupo, na wewe unaamini kimakosa kwamba yupo, hapo nakosa vipi uhalali wa kusema habari za Mungu kuwapo ni uongo na wanaoamini Mungu yupo, kama wanabisha hili, watoe uthibitisho kwamba Mungu yupo?
Hujathibitisha Mungu yupo.
Unarukaruka tu kama bisi kikaangoni.