Oooh sorry. Nilianza kutozipa uzito comment zako na kuzisoma hadi mwisho baada ya kuona unajizungusha kujibu swali rahisi na jepesi namna hii then nimerudia kuzisoma baadhi ya comments zako nimegundua ulinijibu swali langu koment mbili nyuma ya hii.
Sasa Sikia Dogo, ukishasema kitu fulan HAKIPO mjadala unakuwa UMEFUNGWA.
UWEZI KUJADILI KITU AMBACHO USHASEMA HAKIPO.
Wewe sema tu ni mvivu wa kusoma.
Kwanza usiniite dogo hiyo ni dharau, hujui umri wangu.
That is very condescending. Halafu inakuonesha wewe ni mtu wa kufanya assumptions tu.
Kuhusu hoja yako kwamba kitu ambacho hakipo sitakiwi kukijadili, hapo unaonesha utapiamlo katika uwezo wako wa kufikiri kimantiki.
Nitakuonesha kwa nini, kwa mfano rahisi tu.
Kama kuna mganga muongo anasema ana dawa inayotibu ugonjwa mpya, na madaktari wanajua hakuna hiyo dawa, huyo mganga ni muongo, madaktari hao wana wajibu wa kukanusha na kusema hiyo dawa ni ya uongo haipo.
Wataijadili hiyo dawa ambayo haipo ili kuonesha watu kwamba haipo.
Wewe ni kama mganga muongo unayesema kuna dawa (Mungu) wakati hakuna kitu hicho.
Daktari anayejua hiyo dawa haipo (mimi) ana wajibu wa kuweka rekodi sawa na kuonesha uongo wako.
Kwa sababu, kuna watu wanaweza kuzembea kujikinga wakifikiri kuna dawa, kumbe habari za dawa kuwepo ni uongo.
Natumaini umeacha uvivu wa kusoma na umesoma mpaka mwisho.
Vinginevyo hatutawezi kujadiliana.
Mungu hayupo.
Kama unabisha, thibitisha yupo.