"Sababu hii ni "contradiction".
Habari ikijipinga yenyewe kwa mambo ya msingi kabisa, haiwezi kuwa ya kweli."
Itanawezekana vipi mimi sikubali ya kuwa niko Geneva na wakati upande mwingine ni kweli niko Mara, Serengeti ila kwa vile kumezuka contradiction ya mimi kutoweza kuweko sehemu zote kwa wakati mmoja ndo ipelekee hiyo habari isiwe ya kweli na mimi nisiwepo?
Ni lini Mungu aliruhusu na kuamrisha watu kufanya mabaya?
Mkuu, tumekubaliana jambo lenye contradiction isiyotatulika linaonesha uongo. Dexterous ambaye anasemwa yupo Serengeti na Geneva kwa wakati huo huo hayupo, ni wa kufikirika tu.
Ukipewa kesi ya wizi physically benki Geneva, ukaweza kumuhakikishia Jaji kuwa muda huo ulikuwa Serengeti Mara, utakuwa umeihakikishia mahakama kuwa huyo aliyeiba physically Geneva wakati wewe uko Serengeti si wewe.
Kumbuka, Dexterous aliye Serengeti si sawa na Dexterous anayeweza kuwa Serengeti na Geneva kwa wakati huohuo.
Wa Serengeti tu anawezekana kuwepo. Wa Geneva tu anawezekana kuwepo. Anayekuwa Serengeti na Geneva kwa wakati mmoja hayupo. Ni jambo la kufikirika tu kwamba kuna Dexterous anayeweza kuwa Geneva na Serengeti kwa wakati mmoja.
Sasa basi.
Mungu muweza wa yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote aliweza au hakuweza kuumba ulimwengu ambao maovu hayapo, hayawezi kuwepo, hayawezi hata kufikirika na hivyo hayawezi kutendeka?
Kama aliweza, kwa nini hakuumba ulimwengu huo? Kama aliweza, na hakuumba tu, kwa kuwa hakuumba ulimwengu huo, Je, ni kweli kuna Mungu mwenye upendo na rehema zote? Haiyumkiniki Mungu mwenye upendo na rehema zote, mwenye uwezo wote, ujuzi wote, aumbe ulimwengu ambao mabaya na maovu yanaweza kutokea.
Kama alitaka kuumba ulimwengu huo, kwa mapenzi na rehema zake, ila hakuweza tu, je, ni kweli Mungu ana uwezo wote? Mbona alitaka kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani ila akashindwa tu?
Mungu muweza yote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi asiweze kulibeba?
Kama anaweza, Mungu huyo si muweza yote, maana kutakuwa na jiwe hawezi kulibeba.
Kama hawezi, Mungu huyo si muweza yote, maana hawezi kuumba jiwe ambalo hawezi kulibeba.
Unaona jinsi dhana ya Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo/ rehema zote ilivyo na utata ukiiangalia kwa umakini wa kimantiki?