1. Habari za uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na rehema zote aliyeuumba huu ulimwengu unaoruhusu mabaya zinajipinga zenyewe (zina internal contradiction).
2. Internal contradictions hizo, hazijatatuliwa kimantiki kwa maelfu ya miaka.
3. Habari yenye internal contradiction isiyoweza kutatuliwa kimantiki inaonekana kuwa ni habari isiyo na ukweli (mifano, mtu kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja, pembetatu ambayo hapohapo ni duara).
4. Habari ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na rehema zote aliyeuumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya ni hadithi za kutungwa na watu tu. Hazina ukweli.
5. Watu wengi wanaobishana kuhusu habari hizi hapa JF kwa kutetea uwepo wa Mungu huyu, wanabishana kwa kutetea mapokeo/ dini zao. Wengi wanatetea dini walizozaliwa ndani yake. Hawana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kimantiki (logical thinking), hawana uwezo mkubwa wa kufikiri kidhahania (abstract thinking), hawajasoma maandishi muhimu yanayojadili hoja kuu za kutetea au kupinga uwepo wa Mungu. Hawajui hata "problem of evil" ni nini.
Unamuuliza mtu imekuwaje Mungu mwenye upendo wote na ujuzi wote na uwezo wote akaumba ulimwengu ambao unaweza kuruhusu mabaya yawepo, mtu anakujibu Mungu hakuumba mabaya, watu ndio wamefanya mabaya. Clearly huyu hata swali hajalielewa, hivyo hawezi kulijibu.
6. Watu hawa wengi ni wabishi sana, wana maswali ya logical non sequitur, wanafanya sana fallacy ya "argument from authority" kwa kutumia vitabu vya dini vinavyosemwa vimetoka kwa Mungu, lakini vyenye makosa ya kimant8ki mengi sana.
7. Watu hawa, wengi sana wanabishana kwa kutetea "identity" yao, ambayo wameifunganisha na dini/ imqni ya suoernatural. Kwenye vitu vya kufikirika tu ambavyo haviwezi kuthibitishika.
8. Hata pale wanapoona mwanga kidogo, wana kile kinachoitwa "Sunken Cost Fallacy" kubwa sana. Hii inaendana na "cognitive dissonance" kubwa sana inayoleta attitude ya "my God/ religion/ traditiin, wrong or right"
9. Wengi wanatoa counter arguments zinazopinga point zao wenyewe bila kujua. Mtu anakwambia Mungu lazima yupo kwa sababu uumbaji huu wenye maajabu mengi na complexity kubwa hauwezi kutokea wenyewe bila Mungu kuuumba. Wakiwa hawajajua kwamba, ikiwa kila complexity itahitaji muumbaji, basi Mungu muumba vyote hawezi kuwepo, maana naye atakuwa complex atakayehitaji muumbaji.
10. Watu wengi hawajui hata Kiingereza cha kusoma nqnkuelewa hizi mada, lugha ambayo hoja hizi zimeandikwa sana. Na hivyo kujadiliana nao ni kujadiliana na mtu ambaye kanyimwa kabisa vitabu vyote vilivyoandikwa Kiingereza. Falsafa hizi hazijaandikwa Kiswahili. Wachqche wanaojua Kiingereza inaonekana hawajasoma falsafa ya dini kiqsi cha kuweza kuendeleza majadiliano ya kisomi yenye tija.
Matokeo yake, majadiliano yana devolve.
Kazi ya kumfundisha guluguja string theory inaendelea.