Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Watakaopitia mjadala wetu wa uzi huu na mwingine wataelewa tu
Watakachoelewa si muhimu kama ukweli.

Kwa sababu wanaweza kuelewa vibaya.

Ukweli ni kwamba.

1. Hujathibitisha Mungu yupo.

2. Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

3. Huwezi kuthibitisha Mungu yupo, kwa sababu hayupo.

4. Mungu hayupo, kwa sababu, dhana ya kuwapo kwake inajipinga yenyewe, ina internal contradiction.

5. Ndiyo maana hujaweza ku resolve the problem of evil, if you even know what that is.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
And the worst part about them ni kwamba,Wajapani hawana DINI...
Is that the worst party? Huo ni uthibitisho kuwa dini sio kigezo cha kuleta ustaarabu.
Ila jina la baba yake ndo lilikuwa linaleta shida, tulilizoea hivyohivyo.
 
"Sababu hii ni "contradiction".

Habari ikijipinga yenyewe kwa mambo ya msingi kabisa, haiwezi kuwa ya kweli."

Itanawezekana vipi mimi sikubali ya kuwa niko Geneva na wakati upande mwingine ni kweli niko Mara, Serengeti ila kwa vile kumezuka contradiction ya mimi kutoweza kuweko sehemu zote kwa wakati mmoja ndo ipelekee hiyo habari isiwe ya kweli na mimi nisiwepo?

Ni lini Mungu aliruhusu na kuamrisha watu kufanya mabaya?
 

Mkuu, tumekubaliana jambo lenye contradiction isiyotatulika linaonesha uongo. Dexterous ambaye anasemwa yupo Serengeti na Geneva kwa wakati huo huo hayupo, ni wa kufikirika tu.

Ukipewa kesi ya wizi physically benki Geneva, ukaweza kumuhakikishia Jaji kuwa muda huo ulikuwa Serengeti Mara, utakuwa umeihakikishia mahakama kuwa huyo aliyeiba physically Geneva wakati wewe uko Serengeti si wewe.

Kumbuka, Dexterous aliye Serengeti si sawa na Dexterous anayeweza kuwa Serengeti na Geneva kwa wakati huohuo.

Wa Serengeti tu anawezekana kuwepo. Wa Geneva tu anawezekana kuwepo. Anayekuwa Serengeti na Geneva kwa wakati mmoja hayupo. Ni jambo la kufikirika tu kwamba kuna Dexterous anayeweza kuwa Geneva na Serengeti kwa wakati mmoja.

Sasa basi.

Mungu muweza wa yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote aliweza au hakuweza kuumba ulimwengu ambao maovu hayapo, hayawezi kuwepo, hayawezi hata kufikirika na hivyo hayawezi kutendeka?

Kama aliweza, kwa nini hakuumba ulimwengu huo? Kama aliweza, na hakuumba tu, kwa kuwa hakuumba ulimwengu huo, Je, ni kweli kuna Mungu mwenye upendo na rehema zote? Haiyumkiniki Mungu mwenye upendo na rehema zote, mwenye uwezo wote, ujuzi wote, aumbe ulimwengu ambao mabaya na maovu yanaweza kutokea.

Kama alitaka kuumba ulimwengu huo, kwa mapenzi na rehema zake, ila hakuweza tu, je, ni kweli Mungu ana uwezo wote? Mbona alitaka kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani ila akashindwa tu?

Mungu muweza yote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi asiweze kulibeba?

Kama anaweza, Mungu huyo si muweza yote, maana kutakuwa na jiwe hawezi kulibeba.

Kama hawezi, Mungu huyo si muweza yote, maana hawezi kuumba jiwe ambalo hawezi kulibeba.

Unaona jinsi dhana ya Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo/ rehema zote ilivyo na utata ukiiangalia kwa umakini wa kimantiki?
 
Thibitisha Mungu yupo. Hayo ya miaka 50 leo tutajuaje kwamba hunidanganyi?

Na unajuaje ndani ya miaka 50 nitakuwa nimekufa?
Huna haja ya kujua, itakusaidia nini nawe una nafsi ya kumkana Mungu wako kwa pumzi yako.
Ni kama wewe kutaka kujua rangi ya upepo.
Subiri matokeo , usiwe na mchecheto.
 
Acha umuhimu wa ilo swalo uwe juu yangu, jikite kujibu nilichokuuliza.
Ngoja nikukumbushe ikiwa umesahau swali langu ni :, UNAAMINI KUWA MUNGU YUPO AMA HAYUPO?.
NI JIBU TUENDELEE.
Akikujibu Hayupo Achana nae maana haitakua na maana tena! Akikujibu yupo ndo uendelee nae... "Wisdom must take A lead in such matter"
 
Wakati bongo, mkuu wa shule anaandikiwa barua na mwanafunzi ya kuacha shule.
South Korea wana rate kubwa ya kujiua. Yani halafu wanajiua kwa vitu ambavyo sisi tunaona vya kipuuzi 😄
 
Wakati bongo, mkuu wa shule anaandikiwa barua na mwanafunzi ya kuacha shule.
Mkuu kwakweli sisi waafrika ni watu wagumu tunabeba mengi na tunasurvive.
Uwa hao wenzetu mara sijui wana depression wakaone wana saikolojia, mara sijui wana anxiety, mara sijui alimwona baba anamdunda mama inamsukbua ukubwani anakuwa serial killer. Sisi tunashuhudia zaidi ya hayo hakuna cha mwanasaikolojia wala kuwa suicidal tunadunda tu.
 
Hilo kweli, wanasifika kwa kutokuwa na wizi ila kiasi kikubwa unakuta hawaweki record za hayo matukio ili tu wasichafue sifa yao ya kusifika kuna usalama na hakuna wizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…