Jamaa huyu anaitwa
Kiranga amewabana mbavu, linapokuja suala la kuthibitisha mnatumia mihemko, hasira na akili za hisia kujibu hoja zake.
Wengi wenu hamjui hata ni kwa nini ni waumini wa hizo dini zenu, ili muelewe jikite zaidi kuelewaa nini maana ya 'imani'?
Muumini wa imani ya dini ya kikristo.
Muumini wa imani ya dini ya kiislamu.
Muumini wa imani ya dini ya budha n.k, hizi zote ni imani, dini ni imani na kila dini ina misingi yake.
Kwa hio kuwa mfuasi wa dini fulani, tayari ume base zaidi kwenye spiritual conviction rather than proof ambapo hio ndio imani.
Kiranga na wewe hio ni imani yako, kwa kuamini mungu hayupo ina maana unaamini hakuna maisha baada ya kifo, tukifa tunaishia hapo hapo, hiyo ni imani yako kwani huwezi thibitisha hilo.
Hivyo wewe pia una imani kama wenye dini tu, tofauti zenu mnaamini vitu tofauti.
Imani ni kuamini pasipo evidince sasa unapotaka kuamini kwa evidence lazima uweke evidence ambazo bado zipo ndani ya imani unapotoka nje ya misingi ya imani ndipo hapo unakosa jibu kwa sababu umetoka nje, sawa na tafiti za kisayansi lazima ziwe katika misingi na taratibu za kisayansi.
Huwezi weka facts kwenye suala la imani hapo umetoka kabisa kwenye misingi ya imani.
Dini ni kuamini katika kitu ambacho hukifahamu, mfano ukifanya uzinzi unaona umetenda dhambi lakini dhambi huioni, wala huwezi ishika bali una amini una dhambi, unakwenda kanisani kutubu ukiamini mungu anakusamehe, unatoka kanisani ukiamini mungu amekusamehe, we umejua vipi amekusamehe? unajua vipi ile dhambi haipo?
Kwa maana hakuna sehemu ya kuangalia kama ile dhambi ipo ama haipo, hio ndio imani.
Hivyo kujibu swali la uthibitisho wa uwepo wa mungu kwa kufuata facts mtakesha kwa sababu mnataka kutumia taratibu za kisayansi kwenye imani, beliefs doesnt care about facts.
Hivyo inatosha kabisa kusema kwamba hakuna facts katika imani, which means huwezi tumia proof na facts kuthibitisha uwepo wa mungu.
Thats it.
Kikubwa kila imani ya mtu iheshimiwe, anayeamini, asiyeamini.