Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwanza tuwekane sawa, hoja yangu inaanzia kwenye kupinga madai ya kwamba hiyo contradiction(Mungu kuumba huu ulimwengu) ndio inahitimisha au ndio uthibitisho kuwa hakuna Mungu.
Habari ya kuwepo Mungu ni imani hivyo mtu akisema kuwa habari ya kuwepo Mungu si kweli si ajabu maana habari yenyewe ni imani.
Hiyo contradiction ni hoja moja tu ya kuthibitisha Mungu hayupo.
Wewe umeshakubali habari ya kuwapo Mungu ni imani tu.
Na imani si lazima iwe kweli.
Awali ya yote, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote hayupo.
Kwa sababu, ulimwengu uliopo unamkanusha.
Kwanza hiyo habari ya "muweza yote" tu, kimantiki ni contradiction tosha kuonesha Mungu huyo katungwa na watu tu.