Swali Fyatu: Kwani Tatizo Gani Wameweza Kulitatua Likaisha?

Halafu ajabu ni kuwa watatatumia hizi kero kama ahadi ya kutaka kutushawishi tuwape kura.

Yaani utasikia tutashughulikia kero ya umeme. Ajira elimu n.k so mtupe kura.😂😂

Nadhani wapuuzi zaidi ni sisi wenyewe watanganyika.
 
Unakela sana na tabia za dini humu kwenye siasa.
Mumeanza kwa kisingizio cha demokrasia. Kama CCM ndio hiyo hiyo haijabadilika. Huyu MMM wakati wa Marehemu Magu alikua muungaji mkono mkubwa. Swali anasimamia wapi? Wakati wa Mkapa akitupa pongezi nyingi lkn alipokuja Jk kawa mkosoaji mkubwa.
CCM ndio hiyo
 
Ujinga mwingine tulio nao ni kuamini matamko ya majukwaani, tumbua tumbua ya barabarani ndio suluhisho na si kuweka mifumo inayohakikisha uwajibikaji.
 
Ccm ni ile ile na vioja vyao ni vile vile.
Baba alikuwa mwizi akamrithisha mtoto madaraka.
Mtoto anapambana kuwa zaidi ya baba. Yaani kuwa mwizi zaidi ya baba yake. Ndicho alichojifunza kwa baba yake.
Tatizo lililopo hapa Tanzania CCM wanacheza pande zote.
Wao wenyewe ndio watawala vilevile wao wenyewe ndio wapinzani.
Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko ila hakuna kwa kubadilikia.
Mzee Mwanakijiji, na mzee@Dr slaa rudini kwenye siasa active mtuokoe, Nchi inazidi kupotea hii.
Kuna kizazi hiki cha 2000's kilichonyimwa elimu ni hatari zaidi.
 

Yaani bado unaamini Dr Slaa aje atuokoe. Ndo haya haya anayosema mleta mada.

Muda mwingine ilikuwa ni heri kuunga mkono mabadiliko maana ilikuwa nafasi pekee ya kuanza kujenga uwajibikaji. Kukosea ukiwa umefanya mabadiliko ni nafuu kuliko kuogopa kufanya.
 
Umeongea vizuri sana

Unadhani tatizo la Tanzania Au Africa ni vyama vya siasa au siasa?

Tatizo ni watu kama mimi na wewe ambao tunadhani siasa ndio solution ya umasikini wetu

The day we drop huu ubwege we western democracy through politicians ndio siku tutabadili bara letu

Wao walibadili mabara yao kabla ya kuja na hizi propaganda na Bendera za vyama

They started with sovereignty before parties

Btw, hata neno party tu may mean anything
 
Yale yale tu mkuu cha msingi tujisahihishe tulipokosea.
Ukinishangaa mimi kuendelea kumuamini Dr slaa, nami pia ntakushangaa wewe kuendelea kumuamini Mbowe.
 
Upo sahihi kabisa na hili ndio tatizo la kudeal nalo.
Na njia yakufika huko ni labda jeshi kuthubutu kuwa wazalendo zaidi.
Kufika huko ni ngumu, lazima uwe jiwe zaidi ya Magufuli.
 
Na alikua timu ileile… right?

When judging… balance

Mnajichanganya sana mjue
Timu Ile ile ila wachezaji tofauti. Wachezaji wengi wa sasa walikuwa benchi na tulianza kuona matokea chanya.
Huyu kocha mpya kabadilisha first eleven yote ya Magu.
Beki hakuna kipa hakuna ni mwendo wa kufungwa tu. Fowadi nazo hazishbulii kabisa.
 
Timu Ile ile ila wachezaji tofauti. Wachezaji wengi wa sasa walikuwa benchi na tulianza kuona matokea chanya.
Huyu kocha mpya kabadilisha first eleven yote ya Magu.
Beki hakuna kipa hakuna ni mwendo wa kufungwa tu. Fowadi nazo hazishbulii kabisa.
Wachezaji walewale

Usichanganye - kama focus ni siasa, basi focus kwenye siasa… wabunge, wenyeviti wa chama, makatibu, watendaji, na nafasi zote za siasa ni walewale

Tatizo mnajipiga chenga wenyewe… hamko clear mnataka nini

Change iliyopo haizidi hata 10%

We need to go deeper kama Kweli tuko serious

Or else kelele ni justification ya kushindwa kutoa solutions na kuanza kulaumu wenhkne

Mtikila alikua ahead of his generation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…