Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Walifanya nini cha kulinganisha na hili.
 
Kumlaumu jiwe kunahitaji roho ya mtu asiye na ubongo.
 
Mfalme wa Msoga Kingdom na timu yake wanabishana na Redio.Redio haibishiwi,ikitangaza imetangaza.
Mzee Mwinyi muungwana sana yeye alishasema Magufuli amefanya mambo yaliyowashinda yeye na wenzake kwa muda mrefu.
 
Tanzania kuna wachuuzi wengi na Wafanyabiashara wachache kama Bakhresa,Mo Dewji,Azania,Jambo Group et al.Hao wanaotuuzia Kariakoo bidhaa feki kutoka China ni wachuuzi tu.
 
Mkuu ushawahi kujua mapungufu ya magufuli?????? Au mahaba tu ndio yanakuongoza????
 
Wapwani si unawajua tena na korosho zao, wanahisi wakimtaja mwamba huyu hawana chao tena japo wanajisahauliaha na kujivika miwani ya mbao wakidhani kumuua JPM kutawafanya watanzania wamtoe mihoyoni mwao ....never ever!
Mzee unabagua wapwani au???? Na nani kakwambia kua wapwani ndio walimuua magufuli???
 
Mpango mzima wa kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma, pamoja na kujenga Ikulu mpya, ni White Elephant Project.

Yani tumetatua tatizo ambalo halipo, wakati matatizo yaliyopo mengi tu bado hatujayatatua.

Sasa hapo kuna kipi cha kusifia?
Tatizo lipi lililotatuliwa ambalo halikuwepo? White elephant kwa maana ipi? Waliopita kabla yake walitatua na/au hawakutatua matatizo yapi na kwa nini?
 
Inatosha wewe kumtaja kwa vile kwa upeo wako unaona ndiye Rais bora kuwahi kutokea. Ila usilazimishe hata familia za akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Akwiline, na wale marehemu wa MKIRU zimuone kama wewe unavyomuona.

Kwangu mimi Magufuli atabakia ni Rais aliyetawala kwa hisia zake, ambaye hakuwa na hekima, Rais KATILI na MWONGO. Aliweza kuwapumbaza wengi ikiwa ni pamoja na wewe mtoa mada kwa kujifanya ni mzalendo wa nchi wakati alikuwa ni mwizi tu kama waizi wengine tunaowajua.

Kama angekuwa na sifa hizo unazommwagia, basi Mungu asingemuacha afariki kirahisi vile. Lakini kwa sababu ya uovu wake Mungu aliamua kumtoa machoni petu ili nchi yetu nzuri ISIHARIBIKE na kuwa kama Yemen au Somalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…