Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Mjadala sio faida na hasara za kuhamia Dodoma, bali watu kujivisha sifa wasizostahili kabisa. Bora wangesema ni white elephant za Magufuli tuelewe kuwa wanamalizia miradi kwavile hawana jinsi.
.....swali lipo Juu kabisa na tumetafuniwa hata majibu.
Lakini, baadhi wameamua kupuuza kwa makusudi au kwa msukumo huo huo waliokuwa na hao hao "Wanao pungukiwa"

.... Kuna maelezo tosha tu kujibu kifyatu tu ikibidi angalau kupata 65% bila ya kuumiza kichwa!

Watapungukiwa na nini?

Hatahivyo, kiufyatu tu, swali hili linawezekana lishajibiwa na aliyekuwa Spika aliyejiuzulu Bwana Job Ndugai.
 
Mwisho wa siku hizo hela zilizotumika/zinazotumika kujengea hiyo moundombinu, ni kodi za Watanzania! Ni mikopo ambayo italipwa na watanzania wote!

Na siyo hao wanasiasa unaotaka wapewe acknowlegment.
Amen
 
Walifanya lakini ukilinganisha na awamu ya tano walifanya kidoogo sana.

Tatizo CCM ni laanifu ndo maana inaua hata wanachama wake wanaopinga ufisadi
 
Andiko lako refu kutaka Magufuli akumbukwe ungeli "summarise" kwa mistari isiyozidi mitano.

Waswahili wanasema "kuchamba kwingi....".

Wanamichezo wote uliowataja sijaona mtu teyote akiandika kwa kulalamika hawatajwi, jiulize kwanini wanatajwa bila mtu kujilazimisha? au mwengine kulazimisha watajwe?


Jibu ni simpo, ukiona mtu au watu walio wengi au hata wachache wenye akili zao wanajitahidi wasimtaje basi elewa kuwa ana aibu zake nyingi hawataki kuzikumbusha kwa makusudi au kwa bahati nbaya.
Jema halilazimishwi.

Wazo la kuhamia dodoma siyo la Magufuli. Na siyo yeye aliyeanza kuhamishia jiji Dodoma na aliyoamuru yeye ijengwe, pia siyo Ikulu ya kwanza kujengwa Dodoma.

Waliokuwa kabla yake wamefanya yao na yeye kafanya yake na waliopo hivi sasa wanafanya yao.

Kwanini iwe mwao kama watu hawataki kumtaja? Au ni sukuma boy mwenzako?
 
Haikua rahisi watu kama hawa kumtaja Magufuli kwa namna hii.

Hakuna jinsi kila mtu atamtaja Magufuli kila mmoja kwa wakati wake, lakini atatajikana kwa wema tu.
View attachment 2642952
Hawa wapinzani kuna wakati huwa hawajielewi kabisa. Wao kila wakati ni kutafuta namna ya kushinda sasa, hawana mipango endelevu bali ni mipango kulungana na upepo. Wapo tayari kumsifu aliyetangulia kwa namna yoyote ili mradi sifa hizo kwa mtangulizi zinambomoa aliyepo.

Magu yupi ambaye angechomoa watu maofisini kwa report ya CAG?
Magu huyu ambaye alimchomoa CAG mwenyewe baada ya kutoa report?
 
Huwezi kujenga miundombinu kwa damu za watu wasio na hatia halafu utegemee na kustahili sifa. Licha ya hayo yote ulioyataja bado Magufuli ni kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea Tanzania.

Aliua watu wenye mawazo tofauti na yake, kateka na kutesa wapinzani, kaanzisha magenge ya "wasiojulikana" wanaojulikana, kaiba pesa za umma na kuzificha kunakojulikana....
Kwa waliokuwa awamu ya tano na kujua aliyoyafanya Magufuli kwa undani, anatakiwa awe mvuta bangi au sukumagang kuweza kujitokeza hadharani kumsifia mwehu yule.
 
🤣🤣🤣🤣ila kweli tunatofautiana yaan mi nshasahau kama kuna rais aliyeitwa magufuli, ila watu bado mnakumbu kumbu
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana

Niandikie:klhnews@gmail.com
Nimeupenda huo mstari, nitakuandikia.
Miongoni mwa makala ninazo zimisi kwenye local media yetu ni gazeti la Cheche, na makala za MM Mwanakijiji na Lula wa Ndali Mwananzela.
P
 
Anayekunyanyua ndio anayeweza kukudondosha,Magufuli he was nobody kama sio Kikwete kuamua kumpa huo Urais.
So,Kikwete ndio aliyemnyanyua na yeye na gang lake ndio waliomdondosha.Magufuli alishindwa game so acha washindi waandike History.

Acha malalamiko,politics is the game na Magufuli aliishindwa.
 
Kwanza nchi hii kama tunapenda sifa za kijinga basi hakuna anayestahili sifa zaidi ya Mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi alikabidhiwa nchi ikiwa imefilisiwa na Nyerere kwa kuingia vita binafsi na Idd Amin.

Tulikuwa tunakula unga wa njano na kuvaa midabwada, mafundi cherehani walikuwa bize sana kushona midabwada.

Wengine tumezaliwa Dar na kukulia Dar lakini wakati wa Nyerere nakumbuka tulikwenda shuleni pekupeku, imagine hiyo ni Dar sijui hali ilikuwaje vijijini.

Leo hii watu wanaingiza tu eacher Marco polo kufanya biashara ya usafiri lakini hawajui Mwinyi ndio aliruhusu mpaka gari za mizigo zibebe abiria.

Tukianza kumrundikia sifa Mzee Mwinyi hapa basi ukurasa huu hautatosha.

Mwinyi alivyokuwa anampamba Magufuli hizo ndio tabia za watu waliostaarabika kutambuwa mchango wa wenzao na ndio maana Mungu amembariki umri mrefu wa kuishi.

Magufuli alidiriki kujipa Umungu kwamba akiondoka yeye hakuna wa kufanya hayo, haya sasa amekufa, Ikulu imesimamiwa na mama na imezinduliwa na leo tunapokea ndege ya mizigo ambayo ni usimamizi wa mama.
 
Kweli kabisa, Mzee Mwinyi ndiye aliyeipa uhai hii nchi, ilikuwa chali.

Mzee Mwinyi anastahiki jina lake liandikwe kwa wino wa dhahabu.
 
Kwani Magufuli amedai kutajwa? angekuwa hai tungeacha ajitetee! Rudi kwenye hoja, Ma Rais waliopita walistahili sifa zipi kwenye ujenzi wa ikulu ya Dodoma? Hata mzee Mwinyi toka awali alikiri Ma Rais wote walifeli jambo ambalo mwenzao alifanya kwa muda mfupi.
 
Kweli kabisa, Mzee Mwinyi ndiye aliyeipa uhai hii nchi, ilikuwa chali.

Mzee Mwinyi anastahiki jina lake liandikwe kwa wino wa dhahabu.
Ni kweli na ikibidi fungua uzi maalum tukampe maua yake. Ila hapa bakia kwenye hoja. Hatuwezi kumpa Mkapa sifa za Mwinyi! Pia vilevile mambo aliyofanya JPM jamaa zenu wasipende kujichomeka waonekane wamo. Mama Samia anastahili maana alikuwa makamu Rais na amekamilisha akiwa Rais.
 
Kweli kabisa, Mzee Mwinyi ndiye aliyeipa uhai hii nchi, ilikuwa chali.

Mzee Mwinyi anastahiki jina lake liandikwe kwa wino wa dhahabu.
Nakumbuka sukari ilikuwa ni kwa mgao mpaka gari la NMC lije uende na daftari ndio reja yako ya kuuziwa sukari mwisho kilo mbili.

Magufuli ameachiwa nchi na Kikwete hazina ikiwa na pesa za kigeni za kutosha halafu waabudu mizimu wanatufanya wote hatuna akili au tumesahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…