Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Hawa watu sijui wanaliabudia lile jitu!
Kutwa kulialia humu oooh mbona hatajwitajwi.!!!
 
Hata ujenzi wa bwawa la umeme siku wanafungua maji, walikuwa wanakwepakwepa hivyo hivyo. Kihalisia CCM kuna shida ambayo ipo siku itafumka na mengi sana.

Asante MM tumemiss makala nzito kama hizi.
Mkimtaja nyie inatosha
 
Swali linakuja kwanini hao wengine hawakutumia hizo kodi za wananchi kufanya hayo mambo kwa miaka yote 40? Au kodi ilianza kukusanywa kipindi cha JPM?
Walifanya mengine.
Ndo mana Ngosha akapata fursa ya kufanya mengine pia.
Kama angekuta nchi haina shule, vyuo vikuu kambi za jeshi nk bila shaka asingeanza na Ikulu.
Wenzie walijenga barabara za kufika Dom na yeye akajenga Ikulu. Bila wenzie kujenga hizo barabara ht yeye asingejenga hiyo Ikulu
 
Tatizo ni Samia yeye ndiye mwanzilishi na anayeruhusu hilo.

Anaogopa kufunikwa wakati kiuhalisia kiutendaji hamkaribii hata kidogo Magufuli.
Samia yuko juu sana ya Ngosha
 
Nani kapinga asisifiwe? Tunachokisema, ni watu wasilazimishe asifiwe kama alivyofanya mleta mada.

Kwa nnayoyaona mimi, binafsi, inayofaa kumsifia ntamsifia na nnayoyaona hayafai kumsifia simsifii. Simpo. .
hapo ndipo penye shida. Ni kama vile hakuna raisi yoyote mwengine aliyefanya kitu zaidi ya JPM, kitu ambacho siyo sahihi. Kuna baadhi ya miradi kama ya barabara aliikuta na akaiendeleza, sawa na wenzake kama Mkapa alivyokuta daraja lile la kusini naye akaliendeleza.
 
Sasa kama nao walifanya kwa nafasi zao kigugumizi cha kumtaja Magufuli kinatoka wapi? Ukweli usemwe, Magufuli kawazidi wote katika uthubutu!
hakuna kigugumizi cha kutajwa pale anapostahili, ila asipewe sifa mpaka zisizokuwa zake.
 
Kwako mtoa mada,

Kuna kitu watanzania hatujakifikiria kwa undani... Au utashi wa kifikra..

Tanzania inahitaji maendeleo hasa ya mtu mmoja mmoja tena wa ngazi ya chini..
Ili kuweza kufika hapo tunahitaji mtizamo sahihi ambapo wananchi wananufaika kibiashara, kilimo, uvuvi, Elimu,afya, ajira sekta binafsi na umma...nk Mahusiano mazuri kimataifa...

Tuje suala la kuhamia Dodoma...

Je lilikuwa kwenye ilani 2015 ? Au msukumo binafsi?

Je kuhamia Dodoma ni maendeleo kwa nchi yetu ? Au kwakuwa Nyerere alisema tuhamie Dodoma.. Basi ni maendeleo?

Kuna watu wanafikiri kila fikra aliyokuwa nayo Nyerere ni sahihi na tatizo linaanzia hapo..

Nyerere alisema twende Dodoma kwakuwa kipindi hiko hakukuwa na mtandao wa barabara

Magufuli alipoingia madarakani na kuchota hela hazina zikajenge Dodoma ulikuwa uamuzi wa kudidimiza uchumi wa nchi ..

Kujenga Dodoma kwa hela ambayo sio kipaumbele kwa nchi kumesababisha mzunguko wa fedha kuharibika ndani ya nchi..

Kulikuwa na wakandarasi, makampuni wanadai hela halali Serikalini wengi hawakulipwa na hela ikapelekwa kujenga Dodoma..
Kampuni nyingi zilikufa kwa kisingizio eti ukaguzi wa madeni ya Serikali..

Wengine wamekuja kulipwa mwaka jana tuu..

Pengine kama Magufuli angepata ushauri mzuri.. Ingekuwa kujenga Dodoma kwa awamu.. Ili na mambo mengine yafanyike...

Mwinyi, Mkapa, Kikwete walipata ushauri hasa kwa wachumi wa nchi..

Hakuna kitu kibaya kama kuchezea uchumi wa nchi kwa projects kubwa na za gharama ambazo output haionekani...

Narudia kujenga Dodoma kama alivyosema Nyerere sio maendeleo kwa nchi yetu yenye uchumi mdogo, zaidi tumeongeza gharama kwa maofisa wa Serikali kila siku safari za Dodoma na Dar..

Uchumi wetu mdogo kuwa na Ikulu mbili kubwa na wafanyakazi kukaa mara Dar au Dodoma...

Ni afadhali kidogo project ya Nyerere Dam.. Na tuombe tuu mito isikauke miaka ijayo..
 
Labda kama hauelewi kiswahili ,Mh SSH ameelezea historia nzima ,Kikwete ameeleza mchakato wote ,Huyo Shujaa wenu ametajwa labda mmeshangaa kugundua wazo la kuhamia dodoma lilitolewa na Mbunge Nyerere.
 
Walifanya mengine.
Ndo mana Ngosha akapata fursa ya kufanya mengine pia.
Kama angekuta nchi haina shule, vyuo vikuu kambi za jeshi nk bila shaka asingeanza na Ikulu.
Wenzie walijenga barabara za kufika Dom na yeye akajenga Ikulu. Bila wenzie kujenga hizo barabara ht yeye asingejenga hiyo Ikulu
Kama wengine wanavyopewa sifa zao kwa kufanya hayo uliyoyataja,na yeye mpeni sifa zake kwa kufanya aliyoyafanya...sasa siku ile kuzunguka zunguka kote kule kulitokana na nini?
 
Tatizo lipi lililotatuliwa ambalo halikuwepo? White elephant kwa maana ipi? Waliopita kabla yake walitatua na/au hawakutatua matatizo yapi na kwa nini?
Tatizo lililotatuliwa ambalo halikuwepo ni tatizo la kuwa na makao makuu mapya ya serikali.

Hili halikuwa tatizo, lakini tumeamua tu kulitatua kwa gharama kubwa sana. Bila msingi wowote wa kueleweka.

A white elephant project is one which has no economic benefit.

See here

white elephant​

noun


Synonyms of white elephant
1
: an Asian elephant of a pale color that is sometimes venerated in India, Sri Lanka, Thailand, and Myanmar

2
a
: a property requiring much care and expense and yielding little profit
b
: an object no longer of value to its owner but of value to others
c
: something of little or no value

Nyerere angalau alipandisha literacy ikafika karibu 100% hususan kwa elimu ya watu wazima na kusaidia kupunguza ujinga. Lakini na yeye ndiye alianzisha huu ujinga wa kuhamia Dodoma ambao hauna tija yoyote kiuchumi wala kisiasa.
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Ha ha haaa. Haya bwashee umeeleweka. Hauna namna ya kukaa kimya make ulilipwa kumdhalilisha Magufuli
 
Maadam Rais mstaafu mzee wetu Mwinyi anamkumbuka hiyo inatosha kabisa

Kwangu mimi Mwinyi " Ruksa" ndio Rais bora

Shujaa Magufuli Mtendaji Bora

Freeman Mbowe Mwanasiasa Bora

Maalim Seif Mwanasiasa Mvumilivu

Kawawa Mwanasiasa Mnyenyekevu

Jumaa kareem!
Kuna watu wanashukuru kuondoshwa kwake mapema na Mungu.

Aliwafanyia mambo ya ajabu sana.
 
Huwa mnapenda kulishwa uongo na wanasiasa. Wanawapikia dhana batili wanawaletea nanyi mnazifakamia kama zilivyo na kuanza kuzibwabwaja mtaani.
Amkeni.
Ninalishwaje uongo wakati
Tanzania kuna wachuuzi wengi na Wafanyabiashara wachache kama Bakhresa,Mo Dewji,Azania,Jambo Group et al.Hao wanaotuuzia Kariakoo bidhaa feki kutoka China ni wachuuzi tu.
Uchuuzi (trading) sio aina mojawapo ya biashara? Bila mchuuzi unadhani ni rahisi manufacturer kumfikia mteja? Punguza ujuaji.
 
Aliyefanikiwa kupenyeza chuki miongoni mwa Watawala na timu zao Mungu anamwona.

Mbona wakati wa kuachiana madaraka Mwl. na Mzee Ruksa hakukuwa na hayo mambo.

Ruksa na Ben

Ben na JK

JK na JPM 🤔
Sasa ni JPM na Mama 🤷‍♂️

Kuna haja hayo mambo ya Reconciliation yafanyike miongoni kuvunja timu miongoni mwa WanaCCM

Vinginevyo itakuwa ni kuchafuana na kuumizana kisa timu

Kila mmoja amefanikiwa kujenga Nchi
 
Hakuna Rais ambaye atamaliza kila kitu.

Fly over ni project ya Kikwete imetekelezwa na Magufuli anamalizia Mama Samia.

Mradi wa world bank wa Dmdp ameanza Kikwete, umetekelezwa awamu ya tano na awamu ya sita wamepewa pesa za Dmdp phase two.

Tatizo lenu kubwa mnadhani kila mtu ni mjinga, wakati nchi inaendeshwa kwa propaganda watu walikaa kimya kunusuru uhai wao, lakini sasa hivi hata mawe yataongea propaganda zenu hazina nafasi.

Mlisema Lowasa mgonjwa mkapiga mpaka pushups matokeo yake mnaliwa na funza kaburini Lowasa bado anapumuwa.

Mkuu unapiga spana hatari
 
Kama wengine wanavyopewa sifa zao kwa kufanya hayo uliyoyataja,na yeye mpeni sifa zake kwa kufanya aliyoyafanya...sasa siku ile kuzunguka zunguka kote kule kulitokana na nini?
Kama ambavyo ht wewe hutaki kuwapa sifa wengine.
Tuwe huru sote.
Nyie msifuni Ngosha tu nasi twawasifu wengine kwa mchango wao ktk Taifa hili
 
Back
Top Bottom