Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Mwisho wa siku hizo hela zilizotumika/zinazotumika kujengea hiyo moundombinu, ni kodi za Watanzania! Ni mikopo ambayo italipwa na watanzania wote!

Na siyo hao wanasiasa unaotaka wapewe acknowlegment.
Kwani hao watangulizi wa Magufuli walikuwa hawakusanyi kodi? Ukweli ubaki pale pale kwamba Magufuli alikuwa na maono! Wamtendee haki! Mnyonge mnyongeni haki yake apewe! Ila na wewe Mzee Mwanakijiji andika vizuri jina la chuma alikuwa anaitwa Rais Mh. Dk. John Pombe Joseph Magufuli
 
Ni kweli na ikibidi fungua uzi maalum tukampe maua yake. Ila hapa bakia kwenye hoja. Hatuwezi kumpa Mkapa sifa za Mwinyi! Pia vilevile mambo aliyofanya JPM jamaa zenu wasipende kujichomeka waonekane wamo. Mama Samia anastahili maana alikuwa makamu Rais na amekamilisha akiwa Rais.
Hakuna Rais ambaye atamaliza kila kitu.

Fly over ni project ya Kikwete imetekelezwa na Magufuli anamalizia Mama Samia.

Mradi wa world bank wa Dmdp ameanza Kikwete, umetekelezwa awamu ya tano na awamu ya sita wamepewa pesa za Dmdp phase two.

Tatizo lenu kubwa mnadhani kila mtu ni mjinga, wakati nchi inaendeshwa kwa propaganda watu walikaa kimya kunusuru uhai wao, lakini sasa hivi hata mawe yataongea propaganda zenu hazina nafasi.

Mlisema Lowasa mgonjwa mkapiga mpaka pushups matokeo yake mnaliwa na funza kaburini Lowasa bado anapumuwa.

Nakumbuka wakati wa kikwete kulikuwa na mjadala bungeni kuhusu kuhamia Dodoma, serikali ikasema haina mpango wowote wa kuhamia Dodoma, na inafikiria kuleta mswada wa kuangalia upya uamuzi wa kuhamia Dodoma Kama bado una mantiki

Leo sifa anabeba yeye na Mwinyi. Ni Kama viongozi wote wa awamu hii wamekula kiapo cha kutokumtaja Jiwe, hadi bwawa la umeme utasikia ni Jakaya na mama!!!
 
Nakumbuka sukari ilikuwa ni kwa mgao mpaka gari la NMC lije uende na daftari ndio reja yako ya kuuziwa sukari mwisho kilo mbili.

Magufuli ameachiwa nchi na Kikwete hazina ikiwa na pesa za kigeni za kutosha halafu waabudu mizimu wanatufanya wote hatuna akili au tumesahau.
Nakumbuka watu walivyokuwa wanalikimbiza gari la ugawaji na hawajui linakwenda kushusha wapi na nini?

Nyerere aliiweka nchi pabaya sana kwa kuwa skikuwa hashauriki, haambiliki. Rejea kilichomkumba Oscar Kambona.
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Napita nitarudi kesho kutwa
 
Andiko lako refu kutaka Magufuli akumbukwe ungeli "summarise" kwa mistari isiyozidi mitano.

Waswahili wanasema "kuchamba kwingi....".

Wanamichezo wote uliowataja sijaona mtu teyote akiandika kwa kulalamika hawatajwi, jiulize kwanini wanatajwa bila mtu kujilazimisha? au mwengine kulazimisha watajwe?

Jibu ni simpo, ukiona mtu au watu walio wengi au hata wachache wenye akili zao wanajitahidi wasimtaje basi elewa kuwa ana aibu zake nyingi hawataki kuzikumbusha kwa makusudi au kwa bahati nbaya.
Jema halilazimishwi.

Wazo la kuhamia dodoma siyo la Magufuli. Na siyo yeye aliyeanza kuhamishia jiji Dodoma na aliyoamuru yeye ijengwe, pia siyo Ikulu ya kwanza kujengwa Dodoma.

Waliokuwa kabla yake wamefanya yao na yeye kafanya yake na waliopo hivi sasa wanafanya yao.

Kwanini iwe mwao kama watu hawataki kumtaja? Au ni sukuma boy mwenzako?
Hivi akisifiwa yeye na wampendao mnaumia kwa lipi? Maana mnaweza pia kuwasifia muwapendao vile vile.
 
Kwani hao watangulizi wa Magufuli walikuwa hawakusanyi kodi? Ukweli ubaki pale pale kwamba Magufuli alikuwa na maono! Wamtendee haki! Mnyonge mnyongeni haki yake apewe! Ila na wewe Mzee Mwanakijiji andika vizuri jina la chuma alikuwa anaitwa Rais Mh. John Pombe Joseph Magufuli
Ingekuwa hao watangulizi wa Magufuli kweli hawakufanya kitu ungeikuta nchi hii iko hivi? Shida yenu nyinyi vijana ni wajuaji sana. Nyerere alifanya yake akawacha nchi hii katika hali fulani ambayo hata sukari ilikubidi uipangie foleni ndiyo upate mgao. Alikuja Mwinyi akafanya yake, akaingia Mkapa naye akaendeleza na baadae Kikwete. Leo wote hao imekuwa hawakufanya kitu aliyefanya ni Magu tu....... wacheni hizo.
 
Hivi akisifiwa yeye na wampendao mnaumia kwa lipi? Maana mnaweza pia kuwasifia muwapendao vile vile.
Nani kapinga asisifiwe? Tunachokisema, ni watu wasilazimishe asifiwe kama alivyofanya mleta mada.

Kwa nnayoyaona mimi, binafsi, inayofaa kumsifia ntamsifia na nnayoyaona hayafai kumsifia simsifii. Simpo. .
 
Jiwe aliupaisha uchumi mpaka ukafikia wa Kati. Hivi sasa tunaambiwa tumeshuka, inakuwaje tena yeye (JPM) ndo awe amesababisha kutufikisha hapa? Hiyo ni simple logic tu.
Uchumi wa kati my foot! Lilipika data shenzi lile halafu likajitangazia mafanikio lenyewe. WB, MF ama WEF ndiyo wenye mamlaka ya kuitangaza nchi kuwa imefika uchumi wa kati.
 
Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani

Nyoko
 
Duh! Hapa sitii neno...ngoja nirudi kwenye thread inayofikirisha ya mwana JamiiForums, Bams

Mtanzania, kiumbe anayefanana na bindamu, ameendelea kubakia hivyo hivyo mpaka leo​

Asante Bams
 
Unataka wale aliowatangaza kuwa wataishi kishetani wamkumbuke?
Maadam Rais mstaafu mzee wetu Mwinyi anamkumbuka hiyo inatosha kabisa

Kwangu mimi Mwinyi " Ruksa" ndio Rais bora

Shujaa Magufuli Mtendaji Bora

Freeman Mbowe Mwanasiasa Bora

Maalim Seif Mwanasiasa Mvumilivu

Kawawa Mwanasiasa Mnyenyekevu

Jumaa kareem!
 
View attachment 2642893
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu ambao tunawakumbuka kwa umahiri na weledi katika kazi, vipaji au matendo yao. Michael Jordan aliichezea timu ya mpira wa vikapu ya Chicago Bulls na kujionesha kuwa ni mchezaji bora Zaidi wa mchezo huo duniani. Wengi wanalijua jina la Michael Jordan lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzake wanne waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza. Hili pia ni kweli kuhusu mchezaji bora Zaidi wa soka duniani Pele. Wengi wanalijua na kukumbuka jinsi Pele alivyoongoza Brazili kwenye makombe ya dunia. Ni wachache sana wanaweza kukutajia wachezaji kumi wengine walioshinda na Pele kombe la dunia mara ya mwisho.

Hata hapa Tanzania kuna watu wanakumbukwa kwa umahiri wao lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya watu wengine kwenye vikosi vyao. Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, au hata Remmy Ongara. Tunajua nyimbo zao, tumewahi kuzisikia lakini tukiuliza wana bendi wenzao ni kina nani ni wachache wanaweza kutaja hata majina mawili.

Ukweli ni kuwa kuna watu wanatokea katika fani mbalimbali na wanakuwa vinara na bora kuliko wengine. Tunapowataja hawa wengine na kuwasifia haina maana tunadharau mchango wa wengine. Ukimtaja Lionel Messi kwa mfano au Cristiano Ronaldo mara moja watu watajua unawazungumzia kina nani lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzao kwenye zile timu zilizokuza majina yao. Unaposema sifa za vinara haina maana unafuta sifa au unadharau sifa za wengine!

Juzi wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Dodoma ambayo sasa inaifanya Ikulu ya Dar-es-Salaam kuwa Ikulu Ndogo kuna watu walisimama na kumwaga sifa mbalimbali. Niliamka mapema (huku niliko) niweze kushuhudia kama watakuwa na ujasiri wa kumtaja mchezaji kinara aliyewafanya wawepo pale siku ile. Bahati mbaya karibu kila aliyesimama ama alinyemelea kulitaja jina la mchezaji huyo bora au alilitaja kama kulipita tu kuwa “alikuwa ni mmoja wa timu”.

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana kwamba na yeye alikuwa na mchango kama wengine tu. Yote hiyo ilifanywa kwa makusudi kabisa wakijaribu kufifisha jina hilo na hawakutaka kusikia makofi na shangwe ambazo wangelitendea haki zingesikaka. Waliogopa kuona kuwa yumkini huyu bwana akiwa amelala kaburini milele kuna watu wanamkumbuka na kummiss!

Wanatuambia kuwa mpango wa kuhamishia Ikulu ulianza toka miaka ya sitini na hatimaye maamuzi yakachukuliwa na taratibu hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa ili kuhamia taratibu Dodoma. Jakaya Kikwete akatupa stori kuwa aliagiza watu waende Malaysia waone mambo yanavyofanyika huko na sisi tuje kuiga. Sikumbuki kwa miaka kumi ya Kikwete kama kuna siku ulifanyika mjadala hata mmoja Bungeni wa jinsi ya kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu Dodoma na kuwa aliwaambia Watanzania kuwa ametuma iende Malaysia! Sijui hiyo timu iliongozwa nan ani! Lakini tunakubali.

Tunaambiwa kuwa viongozi wote waliotangulia wamekuwa wakifanya kama kupokezana vijiti kuliongoza taifa. Wanasahau kuwa Magufuli hakumwachia Samia kijiti; kamwachia gogo! Ni wazi Rais Samia anajitahidi kwa uwezo wake wote kuonekana anaweza kukamilisha miradi hii yote; na kweli tunaona ikimalizwa. Lakini ndugu zetu hawa wanataka tuamine kuwa kama Magufuli asingefanya alivyofanya leo tungekuwa na Ikulu Dodoma au Mji wa Serikali, au miradi hii mingine mikubwa siyo tu ya kimkakati kama inavyoitwa bali ya uthubutu uliopitiliza.

Yaani, kwa miaka Zaidi ya arobaini hawa jamaa walishindwa kuhamia Dodoma walikuwa wanalipia vipindi vya CDA hata sijui tulikuwa tunaambiwa nini. Kwa miaka arobaini walikuwa wanajipanga, na kuandaa ramani, na kuandaa warsha na semina. Kwa miaka arobaini wanaenda Dodoma, usiku usiku wanawahi kurudi Dar, kwa miaka arobaini wanaimba “Dodoma Dodoma” lakini kila wakiama ni “Dar, Dar”.

Akaja Magufuli akasema maneno matupu hayaliwi na upepo haufungwi kanga! Akawakimbiza mchakamchaka watu wazima na majasho hadi kwenye kucha; mambo yakaanza Kwenda. Yaani, yaliyowashindwa kwa miaka arobaini mtu kayaweza kuyasukuma kwa miaka mitano! Halafu wanatuambia “na sisi tulicheza”. Wanasema kweli Pele alifunga goli lakini sisi tulitoa pasi; wanasema Lionel kachukua kombe la dunia lakini sisi tulimbeba! Hatutaki kuwakumbuka!

Sasa wameamua tu kuwa hawamtaja Magufuli kwa sifa zake; hawatamtaja kwa uthubutu wa barabara, meli, mashule, madaraja. Yaani, kuna watu walijenga daraja moja kubwa kwa miaka kumi halafu anakuja mtu anajenga Matano wanajilinganisha naye! “Na sisi tulijenga barabara na sisi tulijenga daraja” msimpe sifa sana yule; alikuwa ati wa kawaida tu. Ni wivu gani huu?

Hivi kweli wakisema sifa za Magufuli kwa haki kabisa, na kusema kuwa alikuwa ni mchezaji nyota wao watapunguziwa sifa zao? Hivi watakapoenda kuwasha umeme wa Bwawa la Nyerere si wataanza kutupigisha stori tena kama za Ikulu! “Oh hili wazo lilikuwa la Nyerere, na sisi wengine tukapokezana vijiti”! Hivi mkimpa sifa Magufuli anazostahili nyinyi mtapungukiwa? Mtaonekana mnamshusha Samia? Au Samia mwenyewe anaweza kuona wivu badala ya kuona Fahari kuwa alikuwa ni sehemu ya miaka mitano ya Magufuli.

Ndio maana ile sauti anayoisikia Rais Samia haikomi. Itaendelea kumlilia na kumkumbusha kutimiza miradi lakini aifanye kwa haki isiwe kana kwamba anaona ana kivuli cha Magufuli. Magufuli akishangiliwa haina maana nay eye hatoshangiliwa; sifa za Magufuli zikiimbwa haina maana za kwake na timu yake hazitaimbwa. Ikulu ya Dodoma wangeachiwa haya ingekuja 2050! Labda wajukuu zao ndio wangeweza kuthubutu! Kama kwa miaka arobaini walichofanikiwa ni kile kilichokuwepo kabla ya Magufuli basi hawa wangeendelea kutenga bajeti ya kula tu kwa kisingizio cha kupanga makao makuu.

Hili ni swali la kwani wakimpa sifa Magufuli wao watapungukiwa naamini bado linahitaji majibu muafaka kwa wakati huu. Ni swali ambalo kama halitajibiwa vyema basi tutajikuta tunaendelea kuliuliza hata kama ni kwa kung’ong’a. Lakini kama siyo wivu, kama siyo kisirani, kama siyo kukereka na kivuli cha Magufuli basi ndugu zetu hawa waanze kuwa wa kweli; mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni; hata kama mnaona zinawapunguzia zenu. Siyo ndivyo haki yenyewe hiyo.

Kwa hiyo basi natangaza hadharani, Ikulu na uamuzi wa kuharakisha kuhamia Dodoma sasa hivi na maendeleo yote ya ujenzi tunayoyaona ni matokeo ya uthubutu, maono, na kujituma kwa Rais wa Awamu ya Tano John Joseph Pombe Magufuli. Mchango wake haulinganishwa na Rais mwingine yeyote kabla yake na baada yake. Anayebisha asimame. Wangekuwa na uwezo na uthubutu huo; wangekuwa wamehamia Dodoma miaka 40 nyuma!

Niandikie:klhnews@gmail.com
RIEP John Pombe Magufuli. Mwenyezi Mungu anayeimiliki na kuipenda Tanzania, kamwe hatatuacha wakiwa. hata kama jina lake linafanyiwa mizaha, kazi yake inajieleza. Hakuna sababu ya kutumia nguvu nyingi.
Wale wazee wa swaga waache waendelee nazo. Uzuri siku hizi mwenye macho haambiwi ona. Tunaona. Tunaanza kujua nani ni nani
 
Ingekuwa hao watangulizi wa Magufuli kweli hawakufanya kitu ungeikuta nchi hii iko hivi? Shida yenu nyinyi vijana ni wajuaji sana. Nyerere alifanya yake akawacha nchi hii katika hali fulani ambayo hata sukari ilikubidi uipangie foleni ndiyo upate mgao. Alikuja Mwinyi akafanya yake, akaingia Mkapa naye akaendeleza na baadae Kikwete. Leo wote hao imekuwa hawakufanya kitu aliyefanya ni Magu tu....... wacheni hizo.
Sasa kama nao walifanya kwa nafasi zao kigugumizi cha kumtaja Magufuli kinatoka wapi? Ukweli usemwe, Magufuli kawazidi wote katika uthubutu!
 
Nani kapinga asisifiwe? Tunachokisema, ni watu wasilazimishe asifiwe kama alivyofanya mleta mada.

Kwa nnayoyaona mimi, binafsi, inayofaa kumsifia ntamsifia na nnayoyaona hayafai kumsifia simsifii. Simpo. .
Ni maoni ya mtoa mara. Hukubaliani naye unanyamaza. Hajalazimisha asifiwe. Kwa maana nyingine unaweza kuanzisha mada ya kumpinga mtoa mada na kumponda msifiwa.
 
View attachment 2642893
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu ambao tunawakumbuka kwa umahiri na weledi katika kazi, vipaji au matendo yao. Michael Jordan aliichezea timu ya mpira wa vikapu ya Chicago Bulls na kujionesha kuwa ni mchezaji bora Zaidi wa mchezo huo duniani. Wengi wanalijua jina la Michael Jordan lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzake wanne waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza. Hili pia ni kweli kuhusu mchezaji bora Zaidi wa soka duniani Pele. Wengi wanalijua na kukumbuka jinsi Pele alivyoongoza Brazili kwenye makombe ya dunia. Ni wachache sana wanaweza kukutajia wachezaji kumi wengine walioshinda na Pele kombe la dunia mara ya mwisho.

Hata hapa Tanzania kuna watu wanakumbukwa kwa umahiri wao lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya watu wengine kwenye vikosi vyao. Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, au hata Remmy Ongara. Tunajua nyimbo zao, tumewahi kuzisikia lakini tukiuliza wana bendi wenzao ni kina nani ni wachache wanaweza kutaja hata majina mawili.

Ukweli ni kuwa kuna watu wanatokea katika fani mbalimbali na wanakuwa vinara na bora kuliko wengine. Tunapowataja hawa wengine na kuwasifia haina maana tunadharau mchango wa wengine. Ukimtaja Lionel Messi kwa mfano au Cristiano Ronaldo mara moja watu watajua unawazungumzia kina nani lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzao kwenye zile timu zilizokuza majina yao. Unaposema sifa za vinara haina maana unafuta sifa au unadharau sifa za wengine!

Juzi wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Dodoma ambayo sasa inaifanya Ikulu ya Dar-es-Salaam kuwa Ikulu Ndogo kuna watu walisimama na kumwaga sifa mbalimbali. Niliamka mapema (huku niliko) niweze kushuhudia kama watakuwa na ujasiri wa kumtaja mchezaji kinara aliyewafanya wawepo pale siku ile. Bahati mbaya karibu kila aliyesimama ama alinyemelea kulitaja jina la mchezaji huyo bora au alilitaja kama kulipita tu kuwa “alikuwa ni mmoja wa timu”.

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana kwamba na yeye alikuwa na mchango kama wengine tu. Yote hiyo ilifanywa kwa makusudi kabisa wakijaribu kufifisha jina hilo na hawakutaka kusikia makofi na shangwe ambazo wangelitendea haki zingesikaka. Waliogopa kuona kuwa yumkini huyu bwana akiwa amelala kaburini milele kuna watu wanamkumbuka na kummiss!

Wanatuambia kuwa mpango wa kuhamishia Ikulu ulianza toka miaka ya sitini na hatimaye maamuzi yakachukuliwa na taratibu hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa ili kuhamia taratibu Dodoma. Jakaya Kikwete akatupa stori kuwa aliagiza watu waende Malaysia waone mambo yanavyofanyika huko na sisi tuje kuiga. Sikumbuki kwa miaka kumi ya Kikwete kama kuna siku ulifanyika mjadala hata mmoja Bungeni wa jinsi ya kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu Dodoma na kuwa aliwaambia Watanzania kuwa ametuma iende Malaysia! Sijui hiyo timu iliongozwa nan ani! Lakini tunakubali.

Tunaambiwa kuwa viongozi wote waliotangulia wamekuwa wakifanya kama kupokezana vijiti kuliongoza taifa. Wanasahau kuwa Magufuli hakumwachia Samia kijiti; kamwachia gogo! Ni wazi Rais Samia anajitahidi kwa uwezo wake wote kuonekana anaweza kukamilisha miradi hii yote; na kweli tunaona ikimalizwa. Lakini ndugu zetu hawa wanataka tuamine kuwa kama Magufuli asingefanya alivyofanya leo tungekuwa na Ikulu Dodoma au Mji wa Serikali, au miradi hii mingine mikubwa siyo tu ya kimkakati kama inavyoitwa bali ya uthubutu uliopitiliza.

Yaani, kwa miaka Zaidi ya arobaini hawa jamaa walishindwa kuhamia Dodoma walikuwa wanalipia vipindi vya CDA hata sijui tulikuwa tunaambiwa nini. Kwa miaka arobaini walikuwa wanajipanga, na kuandaa ramani, na kuandaa warsha na semina. Kwa miaka arobaini wanaenda Dodoma, usiku usiku wanawahi kurudi Dar, kwa miaka arobaini wanaimba “Dodoma Dodoma” lakini kila wakiama ni “Dar, Dar”.

Akaja Magufuli akasema maneno matupu hayaliwi na upepo haufungwi kanga! Akawakimbiza mchakamchaka watu wazima na majasho hadi kwenye kucha; mambo yakaanza Kwenda. Yaani, yaliyowashindwa kwa miaka arobaini mtu kayaweza kuyasukuma kwa miaka mitano! Halafu wanatuambia “na sisi tulicheza”. Wanasema kweli Pele alifunga goli lakini sisi tulitoa pasi; wanasema Lionel kachukua kombe la dunia lakini sisi tulimbeba! Hatutaki kuwakumbuka!

Sasa wameamua tu kuwa hawamtaja Magufuli kwa sifa zake; hawatamtaja kwa uthubutu wa barabara, meli, mashule, madaraja. Yaani, kuna watu walijenga daraja moja kubwa kwa miaka kumi halafu anakuja mtu anajenga Matano wanajilinganisha naye! “Na sisi tulijenga barabara na sisi tulijenga daraja” msimpe sifa sana yule; alikuwa ati wa kawaida tu. Ni wivu gani huu?

Hivi kweli wakisema sifa za Magufuli kwa haki kabisa, na kusema kuwa alikuwa ni mchezaji nyota wao watapunguziwa sifa zao? Hivi watakapoenda kuwasha umeme wa Bwawa la Nyerere si wataanza kutupigisha stori tena kama za Ikulu! “Oh hili wazo lilikuwa la Nyerere, na sisi wengine tukapokezana vijiti”! Hivi mkimpa sifa Magufuli anazostahili nyinyi mtapungukiwa? Mtaonekana mnamshusha Samia? Au Samia mwenyewe anaweza kuona wivu badala ya kuona Fahari kuwa alikuwa ni sehemu ya miaka mitano ya Magufuli.

Ndio maana ile sauti anayoisikia Rais Samia haikomi. Itaendelea kumlilia na kumkumbusha kutimiza miradi lakini aifanye kwa haki isiwe kana kwamba anaona ana kivuli cha Magufuli. Magufuli akishangiliwa haina maana nay eye hatoshangiliwa; sifa za Magufuli zikiimbwa haina maana za kwake na timu yake hazitaimbwa. Ikulu ya Dodoma wangeachiwa haya ingekuja 2050! Labda wajukuu zao ndio wangeweza kuthubutu! Kama kwa miaka arobaini walichofanikiwa ni kile kilichokuwepo kabla ya Magufuli basi hawa wangeendelea kutenga bajeti ya kula tu kwa kisingizio cha kupanga makao makuu.

Hili ni swali la kwani wakimpa sifa Magufuli wao watapungukiwa naamini bado linahitaji majibu muafaka kwa wakati huu. Ni swali ambalo kama halitajibiwa vyema basi tutajikuta tunaendelea kuliuliza hata kama ni kwa kung’ong’a. Lakini kama siyo wivu, kama siyo kisirani, kama siyo kukereka na kivuli cha Magufuli basi ndugu zetu hawa waanze kuwa wa kweli; mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni; hata kama mnaona zinawapunguzia zenu. Siyo ndivyo haki yenyewe hiyo.

Kwa hiyo basi natangaza hadharani, Ikulu na uamuzi wa kuharakisha kuhamia Dodoma sasa hivi na maendeleo yote ya ujenzi tunayoyaona ni matokeo ya uthubutu, maono, na kujituma kwa Rais wa Awamu ya Tano John Joseph Pombe Magufuli. Mchango wake haulinganishwa na Rais mwingine yeyote kabla yake na baada yake. Anayebisha asimame. Wangekuwa na uwezo na uthubutu huo; wangekuwa wamehamia Dodoma miaka 40 nyuma!

Niandikie:klhnews@gmail.com
Kwani lisipotajwa hilo jina la shetani lenu la Chato tunapungukiwa nini?
 
Back
Top Bottom