Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Ina maana aliyefanikiwa kuwaangusha ni USA tu mwaka 1991? Au unaamini kilichoiangusha USSR ni matatizo ya ndani na sio USA?

Hao nliotaja hapo juu ni wale waliojaribu kutumia mabavu,kuhusu kuvunjika kwa USSR kwa nadharia ya kibiashara ni kama conglamorate inapoamua kustreamline,ina kampuni mia lakini wingi wa hizo kampuni unafanya efficiency kuwa ndogo hivyo inaamua kuuza baadhi ya kampuni na kumerge baadhi,zinabaki kampuni chache ambazo unaweza kuzimanage vizuri.
 
Uoni lakini USSR ilivomeguka nchi mpya zilizoundwa (mfano Ukraine, Georgia) mbona zimeshindwa kuwa na uhusiano mzuri na nchi Mama (Urusi) na mpaka kesho hazitaki kumezwa tena mpaka zingine zimeamua kukimbilia NATO?
 
Ukiwa mshirika wa Russia huwezi ukakua kiuchumi sana sana unaweza ukaishia kutengeneza silaha kama AK 47 nk pamoja na kuwa more belligerent.

Ila ukiwa mshirika wa Marekani fursa ya uchumi wako kukua ni mkubwa sana kando na hayo mengine.
 
Guys, however articulate you may be, however the plausibility of the facts you may throw in to bolster your contentions; and however colourful the language of your theses may be. Just get this point: when the chips are down, it is the country with the most powerful economic system that calls the damn shots globally.

Now, judge for yourselves between RF, PRC and USA who controls the global economic system. Ask yourselves why RF with all its power is so concerned about the kinda guy who gets to enter the White House.

As for the WMD many posses them. Even North Korea with its poverty and desperation. Hence, it’s natural for the powerful not to want to ignite the MAD option which is not a strategy at all. They need to live and let live - at the top.
 
Putin =Russia kwa sasa maana haonekani wa kumrithi (Inside Russia no one can challenge the strong man "monster" in Kremlin).
Ilikuwa hivyohivyo hata kipindi cha Stalin na Brezhnev. Nchi kama ile ambayo ina miaka zaidi ya 500 haiwezi kupotea tu kirahisi kisa mtu moja "Vladmir Putin" ndugu yangu.

Halafu kibaya zaidi ambacho nashangaa ni pale ambapo mnaamini kwamba Urusi hakuna wa kumrithi Putin wakati hamfuatilii siasa za Urusi. Kabla ya Putin Sergey Shoigu alishawahi kupendekezwa kama Raisi. Dmitry Medvedev anaweza kuwa Raisi. Sergey Lavrov anaweza kuwa Raisi sema ni mzee. Valery Gerasimov anaweza kuwa Raisi.
 
This is undoubtedly correct, economic power summons all the ghosts out of the periphery. And for now America calls all of the shots. But again what you fail to acknowledge at by and large is that China will also be calling a lot of shots just like the The US, Germany, The EU and Japan and probably at a tremendous rate than any global power behind her.
 
Uoni lakini USSR ilivomeguka nchi mpya zilizoundwa (mfano Ukraine, Georgia) mbona zimeshindwa kuwa na uhusiano mzuri na nchi Mama (Urusi) na mpaka kesho hazitaki kumezwa tena mpaka zingine zimeamua kukimbilia NATO?

Mkuu ukishaachana na mkeo alafu akapata bwana mpya,huwa kunakuwa na animousities na kutokuelewana,especialy ikiwa ulimuoa na kuishi naye kimabavu(forced marriage),ama ikiwa ndoa yenu haikuwa na maeleweno na tafauti zilikuwa nyingi baina yenu,na bwanake mpya naye akawa anazidi kuwafitinisha.
 
Mbona unajichanganya mkuu, umeorodhesha sifa na nguvu kibao za kiuchumi, Kijeshi na Kiteknolojia ilizonazo Urusi alafu wakati huohuo unaliita TAIFA MASIKINI!!!
KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schroeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.

KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.

KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.

KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union

NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
 
Ilikuwa hivyohivyo hata kipindi cha Stalin na Brezhnev. Nchi kama ile ambayo ina miaka zaidi ya 500 haiwezi kupotea tu kirahisi kisa mtu moja "Vladmir Putin" ndugu yangu.

Halafu kibaya zaidi ambacho nashangaa ni pale ambapo mnaamini kwamba Urusi hakuna wa kumrithi Putin wakati hamfuatilii siasa za Urusi. Kabla ya Putin Sergey Shoigu alishawahi kupendekezwa kama Raisi. Dmitry Medvedev anaweza kuwa Raisi. Sergey Lavrov anaweza kuwa Raisi sema ni mzee. Valery Gerasimov anaweza kuwa Raisi.
Hivi mkuu hao uliowataja wataweza kukumbatia sera za kibabe za Putin au watageuka na kukumbatia usasa wa kimagharibi?
 
Putin =Russia kwa sasa maana haonekani wa kumrithi (Inside Russia no one can challenge the strong man "monster" in Kremlin).
Kama hufatilii siasa za Urusi unaweza kukubali kabisa hakuna wa kumrithi Putin, kuna wengine walisema hivo hivo kipindi raisi ni Medvedev kua hakuna atakaeweza kumrithi kiti cha urais lakini akatokea Putin, hivi unamuonaje waziri wa ulinzi wa Urusi.? Sergey Shoigu, hawezi kua raisi huyu bwana..?
 
Na Shoigu amekua akitajwa tajwa sana kuwa anaweza kumrithi VVP,jamaa naye ni mtata na mwenye siasa kali kama VVP.
 
wewe binafsi unaamini kipi, je ni matatizo ya ndani ndio yaliyo iangusha Soviet au ni US, na sababu zako za kuamini unachokiamini ni zipi mkuu.?
Mkuu kwa upande wangu kilichoiangusha USSR ilikuwa ni matatizo ya ndani sana sana mfano Kushindwa kwa sera za Gorbachev : Mwaka 1987 utawala wa raisi Gorbachev ulianzisha sera mbili ili kuinua uchumi wa kisovieti uliokua unasuasua sera hizo ni Perestroika (Hii sera ililenga kuinua uchumi wa kisovieti kwa kukumbatia baadhi ya nadharia za soko huria kama kuruhusu baadhi ya raia wenye uwezo kuendesha biashara bila udhibiti wa dola yaani kuruhusu biashara huria hii haikukidhi mahitaji na haikua endelevu hivyo ilishindwa baadae).Sera nyingine ni glasnost hii sera ilihusisha uwazi hii ni baada ya kuona raia wengi wa muungano hawapendezwi na usiri pamoja na udhibiti mkubwa wa uendeshaji wa muungano hivyo baadhi ya mambo yaliwekwa wazi ambapo raia walifahamu ukweli wa matatizo yalioukabili muungano kama mdororo wa kiuchumi, huduma mbovu za afya, rushwa na mengineyo hivyo kuzusha upinzani dhidi ya muungano, pia kuna sababu kama Mkwamo wa kiuchumi Kumbuka USSR ilikuwa kubwa kuliko hata baadhi ya mabara kama Ulaya, Amerika kaskazini na Amerika kusini hivyo ilikuwa ngumu kupanga maendeleo kulingana na vipaumbele hivyo yako maeneo yaliyo faidika sana huku mengine yakiachwa nyuma. Kukosekana kwa ugatuzi Madaraka yote yalikuwa huko Moscow na mataifa madogo ya muungano yaliminywa japo nayo pia yalichangia kodi ila hayakuwa na sauti). Ubaguzi wa kieneo (Baadhi ya nchi ndani ya muungano zilijiona bora na zenye hadhi ya kupendelewa kuliko nyingine hivyo mbegu ya chuki ilimea na kusababisha baadhi ya maeneo kutaka kujitawala ) na kwa upande wa Marekani huwezi kusema waliiangusha USSR ila tunasema walichangia anguko la USSR kupitia sera za rais Reagan kama Kuunga mkono Mujahidina waliokuwa wakipigana na majeshi ya soviet huko Afghanistan kisilaha, fedha huku Pakistan akitoa mafunzo kwa wapiganaji wa Mujahidina, Kidiplomasia (Utawala wa Reagan uliendesha kampeni kali kuitenga USSR kimataifa na hata kusababisha nchi nyingi kususia olympic iliyofanyika Moscow mwaka 1982 Kumbuka hata marehemu bondia Mohamed Ali alifika Tanzania na kenya kama sehemu ya kampeni hiyo na pia kuna sababu kama Mashindano ya uzalishaji silaha za nyuklia yaliyogharimu uchumi na pato la serikali ya Kisovieti hivyo kifupi tunasema "USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR".
 
Back
Top Bottom