Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

This is undoubtedly correct, economic power summons all the ghosts out of the periphery. And for now America calls all of the shots. But again what you fail to acknowledge at by and large is that China will also be calling a lot of shots just like the The US, Germany, The EU and Japan and probably at a tremendous rate than any global power behind her.

Not with the kind of their political economy environment that is fraught with all sorts of weaknesses and solely dependent on state control of the vanguard elites in the Communist Party.

Btw take note that China, despite its impressive economic facade, still has a substantial population living in third world conditions. The State has shown neither ability nor interest to transform this massive segment of its citizenry into modern society.

Realistically, I do not believe in such countries calling shots at the global leadership. They can only do so in our bizarre countries.
 
Hata huku kwetu Africa saa hizi vijana wa kiume wangekua wanachumbiwa tu kirahisi.Naamini ni heri Putin na genge lake wawepo duniani ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kwa kuish
Teh teh teh! Umenifurahisha sana mkuu teh teh 😀😀😀😀
 
Not with the kind of their political economy environment that is fraught with all sorts of weaknesses and solely dependent on state control of the vanguard elites in the Communist Party.

Btw take note that China, despite its impressive economic facade, still has a substantial population living in third world conditions. The State has shown neither ability nor interest to transform this massive segment of its citizenry into modern society.

Realistically, I do not believe in such countries calling shots at the global leadership. They can only do so in our bizarre countries.

Thanks a lot for sharing these useful and thought provoking details. Do you see China taking a center stage to replace US as a global leader, citadel of democracy and a beacon of hope?
 
Mkuu hapo kumbuka Marekani ndio iliyokuwa kiongozi wa kambi ya magharibi (NATO) na hasimu mkuu wa USSR aliyeongoza mashariki (WARSAW) hivyo hakuwa mshindani mdogo na kuna mchango mwingi tu wa Marekani ambao wanahistoria wengi wameandika ambayo sijaiweka (Inahitaji ufatiliaji kidogo) mfano Maendeleo makubwa ya uchumi ya Marekani na washirika wake: Maendeleo haya ya kiuchumi yaliyoenda sambamba na maisha bora kwa raia wa nchi za magharibi yaliinadi na kuupa nguvu ubepari kama itikadi pekee yenye kuleta matokeo chanya kwa kila mtu na sio ushoshalisti. Kudhibiti kujipanua USSR ulimwengu wa tatu: hapa Marekani alihakikisha hii itikadi haisambai mfano hapa Africa huko Ángola akishirikiana na makaburu alimsaidia Savimbi kupambana na serikali ya kimarxi ya Angola iliyokuwa ikisaidiwa na majeshi ya Cuba na alifanya hivyo hata huko Amerika kusini. Kuongezeka utegemezi wa mafuta Marekani :kutokana na maendeleo makubwa ya kiuchumi Marekani pia nishati ya mafuta ilihitajika hivyo uzalishaji wa mafuta uliongezeka huko mashariki ya kati (Uarabuni) hivyo nchi hizo nyingi zilitajirika haraka kwa kuuza kwenye soko kubwa la Marekani na ili kulinda soko lao nyingi ziliamua kuikumbatia Marekani na kuitosa USSR na hata kusaidiana na Marekani kuipiga vita USSR. Zipo nyingi tu mkuu zinazoelezea mchango wa Marekani kuiangusha USSR.
Yawezekana ukawa sahihi na usiwe sahihi pia mkuu, kuna kitu kidogo nijaribu kusema mkuu wangu

Siku zote sehemu yoyote ile yenye shida tatizo ua linaanzia ndani na kisha wa nje wanakuja. Kwanza tufahamu kabisa hakuna single cause iliosababisha kuanguka kwa Soviet, nikiwa na maana kua US na HATA PAKISTAN (soma walichokifanya hawa watu kwa wa Soviet kwenye Soviet-Afghan war) wanahusika pia na kuanguka kwa USSR. Mtu akikuambia ni internal issues peke yake au external issues peke yake ndio ziliangusha hii empire kubwa duniani NAFIKIRI atakua anakuongopea

Ukisoma ule uzi wako namba 121 haya ndio matatizo walioanza nayo, Soviet leaders walisahau kabisa swala la uchumi wakakomaa na jeshi, sources nyingi za habari mpaka leo zinadai chanzo cha kifo cha Soviet ni Gorbachev lakini mimi BINAFSI ua naona bora ata yeye alijaribu kuleta sera za kukuza uchumi japokua hakufanikiwa. Kumbuka pia nchi nyingi za Soviet ata kabla hazijajitoa kwenye muungano zilianza kubadili sera za kiutawala na kuukimbia ujamaa polepole baada ya kuona unawaumiza kiuchumi lakini viongozi hawakushtuka tu

Baada ya matatizo ya ndani ndio walioko nje wakaona hii ndio nafasi nao wakaingiza mguu wao na kukamilisha tu kile kilichoanzshwa na wasoviet wenyewe kwa akili zao

Nakupa mfano rahisi sana mkuu, NATO ikianguka leo hii itakua sio sababu ya RUSSIA, NATO itaanguka sababu ya ujinga wa viongozi wa nchi wanachama wa NATO, mfano unakumbuka Trump alivokua anasema ujinga kuhusu NATO, ilifika hatua John McCain mwishoni mwishoni anasema tulete sheria itakayomzuia rais kuitoa US NATO bila ridhaa ya congress, hapa wala Urusi hausiki. Kama unafatilia vizuri ata France aliwahi kujitoa NATO sababu ya ujinga ujinga wao viongozi, sasa ikitokea Urusi akaitumia hio fursa ya kuivunja NATO atakua yeye kakamilisha walichokianzisha wao tu

Mfano wa mwisho mkuu, tunajua adui mkubwa wa Urusi kwa ulaya ni Waingereza, hivi unakumbuka case ya Skripal yule jasusi kua aliwekewa sumu na Urusi, hivi unafahamu kua mpaka leo hakuna ushahid kua Urusi alihusika lakini kilichofata ni kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi, US aliwafukuza, Canada aliwafukuza pia, nadhani ni Ujeruman tu alikataa akasema nita take action ushahidi ukionesha kua Urusi anahusika, lakini mpaka leo haupo

Unafikiri kwanini nimekuandika hio aya hapo juu..? soma hiki hapa sasa, Saud Arabia wamemuua mtu na ushaidi hupo kabisa bila wasiwasi, nan umesikia kafukuza wanadiplomasia wa Saudia.? ni US hapana, UK je.?, Canada.?. Hii ni karata imechezwa kwa herufi kubwa, mgogoro kati ya West na Saudia wangeuanzisha wao wenyewe, Urusi/China wangekuja kuumaliza vizuri sana uku wana tabasamu ndio maana walikaa kimya wakisubir US ateleze, wangechukua madili ya silaha na wangepewa base Saudia,

Mkuu samahani kwa maelezo marefu, nimejaribu kukupa mifsno jio miwili hapo juu kukuonesha vipi migogoro ya ndani inanufaisha wa nje ambao wanatumia migogoro yenu kuwamaliza nyie mgombanao kama vile west walivofanikwa kwa Soviet

Kumbuka ata American civil war ilivotishia kulivunja vunja taifa ilo, hapa Russia hakuusika

MIMI BINAFSI NAAMINI KUANGUKA KWA SOVIET KULIANZISHWA NA SOVIET NA KUMALIZIWA NA US, KAMA KUSINGEKUA NA UGOMVI WA NDANI, BASI WA NJE ASINGEWEZA

KUA NA MIGOGORO NI JAMBO MOJA, KUA NA VIONGOZI WA KUZUIA OUTCOME MBAYA SABABU YA HIO MIGOGORO NI JAMBO JINGINE, SOVIET WALIKOSA VIONGOZI HAO
 
Baazigar, wewe unajua kila kitu kuhusu kuanguka kwa mfumo wa kisoviet ila sema unataka kumchalenji Mkuu Proved,sasa mimi napendekeza wewe ongeza nyama kwenye komenti yake pale alipoungukiwa,ili watu tujifunze.natambua sana michango yako Mkuu Baazigar.
Hahaha, hapana mkuu, mimi hua najaribu kufikiri tofauti kidogo haijalishi kama nitakua sahihi au sio sahihi

Nimejaribu kumuuliza Proved yeye anajua nini kuhusu hilo labda naweza kuongeza maarifa

Hua nina tabia ya kusoma vitu haijalishi sources ni zipi then najiongeza mwenyewe kujua hipi sahihi na hipi sio sahihi mkuu. Mimi hua napenda kusema ninachokiamini na kukijua ili kama yupo ajuae zaidi anikosoe au aniongeze maarifa
 
Not with the kind of their political economy environment that is fraught with all sorts of weaknesses and solely dependent on state control of the vanguard elites in the Communist Party.

Btw take note that China, despite its impressive economic facade, still has a substantial population living in third world conditions. The State has shown neither ability nor interest to transform this massive segment of its citizenry into modern society.

Realistically, I do not believe in such countries calling shots at the global leadership. They can only do so in our bizarre countries.

On Economic sanctions imposed to Russia orchestrated by US and its allies: Do you think the sanctions bite? If so, to what extent?
 
Thanks a lot for sharing these useful and thought provoking details. Do you see China taking a center stage to replace US as a global leader, citadel of democracy and a beacon of hope?

Nashangaa sana watu wanaoamini kuwa nchi inaweza kuwa super power kwa vitisho vya silaha huku ikiwa na mfumo dhaifu wa kiuchumi na kidemokrasia. Kielelezo rahisi sana ni kuwa Marekani inaunda silaha za nyuklia na nyingine kubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha jeshi lake kulingana na bajeti inayoidhinishwa na kusimamiwa na mihimili mikuu ya uwakilishi nchini. Na hapo, inabidi wahakikishe sekta nyingine za uchumi na maslahi ya wananchi hayatetereki. Wakikosea, kashkash itakayotokea ndani ya nchi si ya kitoto.

Sasa njoo kwenye nchi kama Urusi, China, North Korea, n.k. Wao, ni mtu mmoja au vikundi vya wateule ndio wanaamua rasilimali ya taifa iende wapi. Katika kushindana na Marekani kuna wakati wanahamishia pesa yote jeshini na kwenye makombora bila kujali hali ya sekta zingine kama afya, elimu, kilimo, n.k. Ndio maana si ajabu kusikia nchi yenye nyuklia ina watu wanakufa kwa njaa au baridi. Wanaishia kwenye propaganda na vitisho vya kijeshi tu. Hiyo global leadership wataiwezea wapi? Na lengo la kuzima demokrasia katika nchi hizo ni kwa vile wanajua hawawezi kujenga na kuendesha mifumo thabiti ya kiuchumi. Aidha, wanataka kuhalalisha mfumo wa ufisadi wa wateule. Watu wanaisifu China kwa kupiga risasi mafisadi bila kujiuliza ni mafisadi gani hao wanaopigwa risasi? Wote?
 
Nilich
Hahaha, hapana mkuu, mimi hua najaribu kufikiri tofauti kidogo haijalishi kama nitakua sahihi au sio sahihi

Nimejaribu kumuuliza Proved yeye anajua nini kuhusu hilo labda naweza kuongeza maarifa

Hua nina tabia ya kusoma vitu haijalishi sources ni zipi then najiongeza mwenyewe kujua hipi sahihi na hipi sio sahihi mkuu. Mimi hua napenda kusema ninachokiamini na kukijua ili kama yupo ajuae zaidi anikosoe au aniongeze maarifa
Nilichokitaka umekifanya kwenye post na 225,umefunguka vya kutosha,na nimepata mambo mapya niliyokua siyajui.asante sana kiongozi.
 
S
Mkuu hapo kumbuka Marekani ndio iliyokuwa kiongozi wa kambi ya magharibi (NATO) na hasimu mkuu wa USSR aliyeongoza mashariki (WARSAW) hivyo hakuwa mshindani mdogo na kuna mchango mwingi tu wa Marekani ambao wanahistoria wengi wameandika ambayo sijaiweka (Inahitaji ufatiliaji kidogo) mfano Maendeleo makubwa ya uchumi ya Marekani na washirika wake: Maendeleo haya ya kiuchumi yaliyoenda sambamba na maisha bora kwa raia wa nchi za magharibi yaliinadi na kuupa nguvu ubepari kama itikadi pekee yenye kuleta matokeo chanya kwa kila mtu na sio ushoshalisti. Kudhibiti kujipanua USSR ulimwengu wa tatu: hapa Marekani alihakikisha hii itikadi haisambai mfano hapa Africa huko Ángola akishirikiana na makaburu alimsaidia Savimbi kupambana na serikali ya kimarxi ya Angola iliyokuwa ikisaidiwa na majeshi ya Cuba na alifanya hivyo hata huko Amerika kusini. Kuongezeka utegemezi wa mafuta Marekani :kutokana na maendeleo makubwa ya kiuchumi Marekani pia nishati ya mafuta ilihitajika hivyo uzalishaji wa mafuta uliongezeka huko mashariki ya kati (Uarabuni) hivyo nchi hizo nyingi zilitajirika haraka kwa kuuza kwenye soko kubwa la Marekani na ili kulinda soko lao nyingi ziliamua kuikumbatia Marekani na kuitosa USSR na hata kusaidiana na Marekani kuipiga vita USSR. Zipo nyingi tu mkuu zinazoelezea mchango wa Marekani kuiangusha USSR.
Mkuu Proved,Safi sana haya ndio mambo tunayotakiwa Tuyafahamu,ndo utamu wa IF,tililika kiongozi.
 
Marekani ni moja ya nchi bora kabisa kwenye suala za zima la Elimu hapa duniani. Vyuo vyake vina wasomi wakubwa wenye ushahiwishi duniani kwenye medani za taaluma. Wasomi wa dunia nzima wako Marekani. Asilimia 50% ya PhD za Marekani ni Foreign Born. The Green Card ni moja ya silaha za Marekani.

Lakini hoja yako ya pili ni mufilisi sana kwasababu imekaa kishabiki kuliko kitaalamu. Mtu yoyote makini hawezi kusema kwamba Russian Rubble inaweza kushindana na dola hata siku moja. Ila Chinese Renminbi inaweza kuiangusha kabisa fedha ya Marekani vizuri tu kama ambavyo fedha ya Uingereza iliangushwa na fedha ya Marekani. Kabla ya kukimbilia ushabiki ni vizuri ukasoma na kuelewa mlolongo wote wa kihistoria ambao ulifanya fedha ya Marekani kutawala duniani.

NB: Hembu labda uniambie ni kwanini unahisi fedha ya Marekani haiwezi kuangishwa ???
Nakufuatilia mwalim,mwaga materials,niko na pen na note book nakopia hapa,asiekuelewa wewe atakua amepania kutokuelewa tu na si vinginevyo,ni kama vile mlevi anavyopania kuwa "nitakunywa pombe mpaka wanibebe" na anabebwa kweli.
 
Ha ha haa ndo ivyo tena,hizi sera zao za haki kwa mashoga na ndoa za jinsia moja,zilianza kuletwa kwetu,Mugabe akamwambi Obama Mugabe yuko tayari kumchumbia Obama.he he hee.

Mkuu utambue kuwa sio watu wote America wanaunga mkono same sex marriages!
Wanaounga mkono ushoga America hawafiki hata nusu ya population ya nchi ile.
Conservatives (ambao ndio Uti wa mgongo wa Republican Party) piga ua wanapinga ushoga kwa nguvu zote.
Just because Obama alisapoti ushoga haina maana America nzima iko hivyo
George W Bush alipinga ushoga.
Reagan alipinga ushoga.
George H. Bush alipinga ushoga
Jaji Kavanaugh wa US Supreme Court aliyeteuliwa majuzi kwa mbinde aliteuliwa kwaajili ya agenda ya kupinga ushoga na abortion
Bado kuna baadhi ya states hadi leo ushoga/ndoa za jinsia moja ni marufuku!
 
Naona tayari umeshafanya assumptions na kuniwekea maneno kinywani ambayo sijayaongea.
Nimeuliza maswali ili nijifunze na huo ushabiki unaousema sielewi umeutoa wapi!
Anyways, thanks for clarifying kuwa Russian Ruble haiwezi kushindana na US$$ hata siku moja? Naomba ufafanue ni kwa nini?
Hoja yako ya kuwa Chinese Yuan huenda ikaireplace US$$ as a global reserve currency, naomba utujuze ni kwa nini Ruble ishindwe na Yuan iweze?
I’m not monetary/economics expert ndio maana nimeuliza unielimishe kwa faida ya wote especially mtu kama mimi niliekimbia umande
Thanks

Mkuu wala sikuwekei maneno kinywani mwako na wala hatugombani, lakini sasa:
Kama wewe siyo Mchumi kwanini ukimbilie kusema "Something only a drunkard sailor would agree " ?

NB: Nachangia kwa kuvizia sana, ntarudi tuwekane sawa kwa takwimu.
 
A drunkard sailor would be the one to invest all his investments( portfolio) in a currency that has no proven stability globally. There’s an inherent risk associated with Yuan in terms of uncertainty in its value and its future in general.
No wonder even majority of the Chinese investors overwhelmingly stash their wealth in the west particularly US for reasons that are based on the economic and political stability and presence of strong institutions, something that is absent in China.
Nakusubiri
Karibu sana
 
Wizara ya ulinzi ya marekani Pentagon inatumia gharama kuuuubwa Sana zaidi kufadhili vikundi vya kigaidi duniani, tofauti na Russia huweza pesa zao kijeshi kwa manufaa yao tu...

Kumbuka bajeti ya pentagon hujadiliwa na kupitishwa na congress. Tofauti na bajeti za ulinzi za nchi nyingine ambapo rais na genge lake la wachache ambao huamua hivyo na wakati mwingine wamekuwa wakiwatesa na kuwanyima wananchi Huduma muhimu kisa jeshi na silaha vipewe kilaumbele.
Russia na US wote wanafadhili hivyo vikundi duniani kote
 
NATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??

Sina uhakika kama idadi ya watu ina uzito wowote. Pengine yaweza kuwa hivyo.
Mfano: China ina watu 1.4 billion lakini inasumbuliwa na US yenye watu 300 millioni tu!!
Israel ina watu millioni 9 tu lakini ina wasumbua waarabu wote walioizunguka pale wanafika almost milioni 300-400
Congo DRC ina watu zaidi ya milioni 60 lakini kanchi kadogo kama Rwanda kanaipa tabu
 
kweli kabisa na tena ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi kuliko russia na marekani, anapiga hatua kwa kasi kwnye tech, uchumi na kijeshi, anachokikosa uchina ni ushawish mkubwa kisiasa but hicho kitakuja tu chenyew kadri uchumi wake unavyozidi kukua
Naomba ufafanuzi hapa kwenye mchina kupiga hatua especially kwenye teknolojia.
Teknolojia gani ambayo mchina anapiga hatua?
 
Back
Top Bottom