Mkuu hapo kumbuka Marekani ndio iliyokuwa kiongozi wa kambi ya magharibi (NATO) na hasimu mkuu wa USSR aliyeongoza mashariki (WARSAW) hivyo hakuwa mshindani mdogo na kuna mchango mwingi tu wa Marekani ambao wanahistoria wengi wameandika ambayo sijaiweka (Inahitaji ufatiliaji kidogo) mfano Maendeleo makubwa ya uchumi ya Marekani na washirika wake: Maendeleo haya ya kiuchumi yaliyoenda sambamba na maisha bora kwa raia wa nchi za magharibi yaliinadi na kuupa nguvu ubepari kama itikadi pekee yenye kuleta matokeo chanya kwa kila mtu na sio ushoshalisti. Kudhibiti kujipanua USSR ulimwengu wa tatu: hapa Marekani alihakikisha hii itikadi haisambai mfano hapa Africa huko Ángola akishirikiana na makaburu alimsaidia Savimbi kupambana na serikali ya kimarxi ya Angola iliyokuwa ikisaidiwa na majeshi ya Cuba na alifanya hivyo hata huko Amerika kusini. Kuongezeka utegemezi wa mafuta Marekani :kutokana na maendeleo makubwa ya kiuchumi Marekani pia nishati ya mafuta ilihitajika hivyo uzalishaji wa mafuta uliongezeka huko mashariki ya kati (Uarabuni) hivyo nchi hizo nyingi zilitajirika haraka kwa kuuza kwenye soko kubwa la Marekani na ili kulinda soko lao nyingi ziliamua kuikumbatia Marekani na kuitosa USSR na hata kusaidiana na Marekani kuipiga vita USSR. Zipo nyingi tu mkuu zinazoelezea mchango wa Marekani kuiangusha USSR.
Yawezekana ukawa sahihi na usiwe sahihi pia mkuu, kuna kitu kidogo nijaribu kusema mkuu wangu
Siku zote sehemu yoyote ile yenye shida tatizo ua linaanzia ndani na kisha wa nje wanakuja. Kwanza tufahamu kabisa hakuna single cause iliosababisha kuanguka kwa Soviet, nikiwa na maana kua US na HATA PAKISTAN (soma walichokifanya hawa watu kwa wa Soviet kwenye Soviet-Afghan war) wanahusika pia na kuanguka kwa USSR. Mtu akikuambia ni internal issues peke yake au external issues peke yake ndio ziliangusha hii empire kubwa duniani NAFIKIRI atakua anakuongopea
Ukisoma ule uzi wako namba 121 haya ndio matatizo walioanza nayo, Soviet leaders walisahau kabisa swala la uchumi wakakomaa na jeshi, sources nyingi za habari mpaka leo zinadai chanzo cha kifo cha Soviet ni Gorbachev lakini mimi BINAFSI ua naona bora ata yeye alijaribu kuleta sera za kukuza uchumi japokua hakufanikiwa. Kumbuka pia nchi nyingi za Soviet ata kabla hazijajitoa kwenye muungano zilianza kubadili sera za kiutawala na kuukimbia ujamaa polepole baada ya kuona unawaumiza kiuchumi lakini viongozi hawakushtuka tu
Baada ya matatizo ya ndani ndio walioko nje wakaona hii ndio nafasi nao wakaingiza mguu wao na kukamilisha tu kile kilichoanzshwa na wasoviet wenyewe kwa akili zao
Nakupa mfano rahisi sana mkuu, NATO ikianguka leo hii itakua sio sababu ya RUSSIA, NATO itaanguka sababu ya ujinga wa viongozi wa nchi wanachama wa NATO, mfano unakumbuka Trump alivokua anasema ujinga kuhusu NATO, ilifika hatua John McCain mwishoni mwishoni anasema tulete sheria itakayomzuia rais kuitoa US NATO bila ridhaa ya congress, hapa wala Urusi hausiki. Kama unafatilia vizuri ata France aliwahi kujitoa NATO sababu ya ujinga ujinga wao viongozi, sasa ikitokea Urusi akaitumia hio fursa ya kuivunja NATO atakua yeye kakamilisha walichokianzisha wao tu
Mfano wa mwisho mkuu, tunajua adui mkubwa wa Urusi kwa ulaya ni Waingereza, hivi unakumbuka case ya Skripal yule jasusi kua aliwekewa sumu na Urusi, hivi unafahamu kua mpaka leo hakuna ushahid kua Urusi alihusika lakini kilichofata ni kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi, US aliwafukuza, Canada aliwafukuza pia, nadhani ni Ujeruman tu alikataa akasema nita take action ushahidi ukionesha kua Urusi anahusika, lakini mpaka leo haupo
Unafikiri kwanini nimekuandika hio aya hapo juu..? soma hiki hapa sasa, Saud Arabia wamemuua mtu na ushaidi hupo kabisa bila wasiwasi, nan umesikia kafukuza wanadiplomasia wa Saudia.? ni US hapana, UK je.?, Canada.?. Hii ni karata imechezwa kwa herufi kubwa, mgogoro kati ya West na Saudia wangeuanzisha wao wenyewe, Urusi/China wangekuja kuumaliza vizuri sana uku wana tabasamu ndio maana walikaa kimya wakisubir US ateleze, wangechukua madili ya silaha na wangepewa base Saudia,
Mkuu samahani kwa maelezo marefu, nimejaribu kukupa mifsno jio miwili hapo juu kukuonesha vipi migogoro ya ndani inanufaisha wa nje ambao wanatumia migogoro yenu kuwamaliza nyie mgombanao kama vile west walivofanikwa kwa Soviet
Kumbuka ata American civil war ilivotishia kulivunja vunja taifa ilo, hapa Russia hakuusika
MIMI BINAFSI NAAMINI KUANGUKA KWA SOVIET KULIANZISHWA NA SOVIET NA KUMALIZIWA NA US, KAMA KUSINGEKUA NA UGOMVI WA NDANI, BASI WA NJE ASINGEWEZA
KUA NA MIGOGORO NI JAMBO MOJA, KUA NA VIONGOZI WA KUZUIA OUTCOME MBAYA SABABU YA HIO MIGOGORO NI JAMBO JINGINE, SOVIET WALIKOSA VIONGOZI HAO