wewe binafsi unaamini kipi, je ni matatizo ya ndani ndio yaliyo iangusha Soviet au ni US, na sababu zako za kuamini unachokiamini ni zipi mkuu.?
Mkuu kwa upande wangu kilichoiangusha USSR ilikuwa ni matatizo ya ndani sana sana mfano
Kushindwa kwa sera za Gorbachev : Mwaka 1987 utawala wa raisi Gorbachev ulianzisha sera mbili ili kuinua uchumi wa kisovieti uliokua unasuasua sera hizo ni
Perestroika (Hii sera ililenga kuinua uchumi wa kisovieti kwa kukumbatia baadhi ya nadharia za soko huria kama kuruhusu baadhi ya raia wenye uwezo kuendesha biashara bila udhibiti wa dola yaani kuruhusu biashara huria hii haikukidhi mahitaji na haikua endelevu hivyo ilishindwa baadae
).Sera nyingine ni
glasnost hii sera ilihusisha uwazi hii ni baada ya kuona raia wengi wa muungano hawapendezwi na usiri pamoja na udhibiti mkubwa wa uendeshaji wa muungano hivyo baadhi ya mambo yaliwekwa wazi ambapo raia walifahamu ukweli wa matatizo yalioukabili muungano kama mdororo wa kiuchumi, huduma mbovu za afya, rushwa na mengineyo hivyo kuzusha upinzani dhidi ya muungano, pia kuna sababu kama
Mkwamo wa kiuchumi Kumbuka USSR ilikuwa kubwa kuliko hata baadhi ya mabara kama Ulaya, Amerika kaskazini na Amerika kusini hivyo ilikuwa ngumu kupanga maendeleo kulingana na vipaumbele hivyo yako maeneo yaliyo faidika sana huku mengine yakiachwa nyuma.
Kukosekana kwa ugatuzi Madaraka yote yalikuwa huko Moscow na mataifa madogo ya muungano yaliminywa japo nayo pia yalichangia kodi ila hayakuwa na sauti
). Ubaguzi wa kieneo (Baadhi ya nchi ndani ya muungano zilijiona bora na zenye hadhi ya kupendelewa kuliko nyingine hivyo mbegu ya chuki ilimea na kusababisha baadhi ya maeneo kutaka kujitawala
) na kwa upande wa
Marekani huwezi kusema waliiangusha USSR ila tunasema walichangia anguko la USSR kupitia sera za rais Reagan kama
Kuunga mkono Mujahidina waliokuwa wakipigana na majeshi ya soviet huko Afghanistan kisilaha, fedha huku Pakistan akitoa mafunzo kwa wapiganaji wa Mujahidina,
Kidiplomasia (Utawala wa Reagan uliendesha kampeni kali kuitenga USSR kimataifa na hata kusababisha nchi nyingi kususia olympic iliyofanyika Moscow mwaka 1982
Kumbuka hata marehemu bondia Mohamed Ali alifika Tanzania na kenya kama sehemu ya kampeni hiyo na pia kuna sababu kama Mashindano ya uzalishaji silaha za nyuklia yaliyogharimu uchumi na pato la serikali ya Kisovieti hivyo kifupi tunasema
"USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR".