Hichi ulichokizungumzia hapa kinaitwa The Heartland Theory au Nadharia ya moyo wa dunia.
Iliandikwa mara ya kwanza kabisa na mwanasayansi wa siasa kutoka Uingereza aitwaye Sir Halford MckKinder ambaye mwaka 1904 alisema kwamba kama taifa litafanikiwa kutawala eneo la Ulaya Mashariki na Asia (Eurasia) basi litatawala Ulaya yote na Asia. Aliyaandika haya kwenye chapisho lake liitwalo The Geographical Pivot of History na akasema kutokana na utajiri wa rasilimali wa eneo hilo taifa lolote litakalotawala Ufalme wa Urusi basi linaweza tawala dunia.
Ikumbukwe Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa wingi wa rasilimali zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 75. Marekani na ujanja wake wote ana rasilimali zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 4, hivyo Urusi kama ikisambaratika nchi nyingi za Ulaya zinaweza kunufaika sana na utajiri wake.
Wanahistoria wanaamini kwamba moja ya sababu kubwa za Adolf Hitler kuvamia Urusi mwaka 1941 kabla ya nchi nyingine zote ni kwasababu Wanazi waliamini kwenye The Heartland Theory kwamba kama watampiga Urusi mapema basi watatumia rasilimali zake zote kuipiga dunia yote na ndiyo maana mataifa ya Ulaya na Marekani ikabidi watume msaada wa kipesa kwa Urusi. Hata baada ya vita ya dunia kuisha, Vita Baridi ilichangiwa sana na hii nadharia ambayo Waingereza na Wamarekani iliwakaa sana kichwani.
Tatizo la Urusi la anguko la Urusi ya Kisovieti lilikuwa siyo kusaidia mataifa mengine lakini mfumo wake mbovu na kukataa kubadilika kwa viongozi wa Kisovieti hasahasa wale kama Leonid Brezhnev. Tukisema kwamba tatizo ni kusaidia mataifa mengine tutakuwa tunasahau kitu cha muhimu sana kwamba hata Marekani naye alisaidia sana mataifa mengi sana duniani tena kwa nguvu nyingi sana kuliko hata Urusi.
Wakati Urusi alikuwa ana washirika wa Kijeshi wa Ulaya tu kupitia The Warsaw Pact, Marekani alikuwa na washirika wa kijeshi dunia nzima Kuanzia NATO, ANZUS, SEATO hadi CENTO. Mpaka leo Marekani ana mikataba ya ulinzi kama 60 hivi.
Misaada ya kiuchumi wote walitoa huku Marekani akianza na The Marshal Plan huku wasovieti wakija na The COMECON. Wote walisomesha watu huko Harvard, Yale, Moscow State University na University of St.Petersburg lakini Urusi aliachwa mbali sana. Kwanini ?? Mfumo mbovu wa kiuchumi au kuruhusu serikali kutawala uchumi kwa kila kitu (Command or Centralization of Economy). Uchumi wa Urusi haukuruhusu ushindani wa ndani ya nchi, wakati Marekani makampuni binafsi yalikuwa yanazalisha bidhaa na kupunguzia serikali mzigo. Uchina chini ya Deng Xiapoing waligundua hili mapema ndiyo wakaryuhusu mfumo wa masoko utawala nchi. Hivyo hapa sikubaliani na wewe kidogo mkuu wangu kwasababu kama kusaidia wote walisaidia mataifa ya nje kwa sana tu.
Hapa nakubaliana na wewe kwamba Urusi alikuwa na nguvu sana hadi kutanua lile eneo lake lote. Alifanya hivyo kwenye Vita Baridi ya kwanza aliyopigana na Muingereza tokea mwaka 1813 hadi 1907 ambayo iliitwa kama The Great Game au The Tournament of Shadows. Lakini naomba nikukosea kidogo hapo uliposema Marekani alikuwa hana nguvu: Nifahamuvyo mimi mpaka kufika mwaka 1916 Ujerumani alikuwa ameshashinda vita ya kwanza ya dunia na Muingereza alikuwa anajiandaa kusalimu amri, lakini aliyebadilisha mwelekeo ule wote ni Marekani chini ya Prof. Woodrow Wilson.
Mbali na hapo ikumbukwe kwamba Ujerumani alipanga kumvamia Marekani mwaka 1897 na Mfalme Kaiser Wilhelm alimtuma Ebenhard Von Mantey kupanga uvamizi kwa kutuma vikosi 100,000 lakini mpango huu ulikufa baada ya Marekani kuonesha nguvu zake kwa kumtwanga vibaya Mhispania kwenye vita ya mwaka 1898 (The Spanish American War)na kumnyang'anya CUBA na makoloni yake muhimu. Hapa utasemaje Marekani alikuwa hana nguvu ???
Unahisi Uingereza angeshinda Vita ya kwanza ya dunia dhidi ya Ujerumani bila Marekani kuingilia kati ?
Pia tusisahau kwamba Urusi ilisalimu amri mapema sana kutoka kwa Ujerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia hadi wakina Lenini wakasaini Mkataba wa hovyo kabisa wa Brest-Litovsk ambao ulikubali kumruhusu Ujerumani achukue sehemu za Urusi kama Poland, Estonia, Finland, Latvia, Ukraine na Lithuania. Bila Marekani kuingia kwenye vita uandhani haya maeneo yangerudi kirahisi ?
CC: Wick , muyovozi , MASAMILA , neo1
Kwanini unazungumzia vita vya kwanza vya dunia baadala ya vita vya pili vya dunia?? Ukitaka kuielewa Russia na iliyokuwa Soviet Union zungumzia WWII...Soviet union ndiyo iliyoiokoa dunia kutoka kwa Hitler...Eastern Front ambako Hitler alipambana na Soviet ndiko kulikoamua hatima ya WW II.