Mie nilimaanisha kivita nhasa kutokana na swali lako
"Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ??" . Labda maelezo ya ziada yanatakiwa tujue Marekani anasumbuliwa kivipi na situation gani iwepo ili aonekane hasumbuliwi.
Jinsi umoja wa kisoviet ilivyomalizwa ni mada ndefu na nafikiri haiwezi kuwa credited to NATO/US in its entirety. Matatizo ya ndani ya USSR kutokana na
viongozi wa Communist Party kujilimbikizia mali kulileta manung'uniko kutoka kwa younde generation ambayo haikukubaliana na ideology ya wazazi wao. Vile vile reforms alizoleta Gorbachev kupitia sera zake za
glasnost na
perestroika hazikuta mafanikio yaliyotarajiwa zaidi ya kusababisha uhaba wa bidhaa muhimu. Inaonyesha kuwa hata kuanguka kwa USSR
hakukutegemewa na nchi za magharibi. Siutendei haki uzi huu kwa kutoa jibu hili kwani ni topic ndefu inayohitaji research kabla ya kuandika. Lakini kwa haya machache, inanyesha kuwa nchi za magharibi hazikusababisha umoja wa USSR kumalizwa, na kwa hiyo hakuna sababu ya kujiuliza kwa nini wasiimalize Russia ya sasa kama walivyoimaliza USSR. Na hata kama kweli waliimaliza USSR, haina maana ndio wana mkakati wa kuimaliza Russia sasa hivi.