NATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??
USA,ndio nchi inayopokea misaada ya kijeshi kiulinzi na kijasusi Duniani kuliko nchi yeyote ili kuikabili Russiah Federation (RF)
.Baada ya vita kuu ya pili ya dunia,kukatokea vita nyingine mbili lakini sio za moto
1.vita baridi
2.mashindano ya kutengeneza silaha kali duniani.
Vita baridi USSR ilishindwa na USA
Vita ya kutengeneza silaha bado inaendelea, kama vile ilivyokua mwanzo kati ya USSR na USA.lakini USA bado anaendelea kusaidiwa na washirika wake ,wakati RF( Urusi) akiwa peke yake.
Hata baada ya kuvunjika umoja wa Kisovieti,bado USA anasaidiwa kutengeneza silaha na masuala ya Intelijensia ili kikabili Russian Federation( RF) yaani Urusi ya Vladimir Putin.
ONA.
Baada ya WWII, kukaibuka vita baridi kati ya USSR akieneza ukomunist na USA ikieneza ukapitalist.
USSR akaunda Warswa Pact kujihami,USA akaunda NATO kujihami.
USSR ikavunjika na Warsawa Pact ikavunjika ikabaki Russian Federation ( RF)peke yake,Wakati USA ikabaki na NATO ikabaki,lakini Bado hawajaweza kumcontain RF,Urusi.
Baadhi ya nchi zilizokua USSR,zikajiunga na NATO,bado Russia iko peke yake,lkn hawajamweka mkononi RF.
Baadhi ya nchi zilizokua Warswa Pact zikajiunga na NATO,bado Russia iko peke yake lakini hawajaweza kumdhibiti,RF.
Kwa kupitia NATO,USA anapata misaada mikubwa sana ya kiteknolojia,kijeshi na kiintelijensia ili kuikabili Urusi. Nchi kama UK,France,German,etc zimeisaidia sana USA kijeshi kudili na Russia.
MISAADA YA KIJESHI KWA MAREKANI NJE YA NATO
Israel,huisaidia sana USA kijasusi na tech dhidi ya Urusi,
Pakistan iliwahi kuisaidia USA kudili na USSR huko Afghanistan,
Ugiriki,hawa walinunua S300 toka Russia,wakawaalika Waisrael,wakaenda kuichunguza na kuifanyia mazoezi jinsi ya kuishinda,
Uingereza kama nchi pekee nje ya NATO ina bifu la asili na Urusi hapa mashirika ya kijasusi kama MI6,MI5 na CIA huishughulikia kwa pamoja Urusi,anaefaidika sana ni USA,
USA wameshiriki mara nyingi kuiba silaha za URUSI na kwenda kuzisoma na kisha kujua siri zilizowanufaisaha .Rubani mmoja wa jeshi la Iraki aliwahi kuiba MIG ya kirusi kwa faida ya Israel na aliyefaidika ni USA.
Hiyo mifano michache,na mara zote Urusi huwa haiteteleki wala kulalamika.
Ukraine,Georgia,Poland,Chek ni mfano wan chi zinazoinufaisha USA.
Hivyo mbinu zote za kijeshi,kijasusi na baadhi ya vifaa vilivyokua vya baadhi ya wanachama wa Warsaw Pact na nchi zilizokua za Kisoviet zilizohamia upande wa NATO na USA, ZIMEIFAIDISHA sana USA lakini bado wameshindwa kuimudu Russia Peke yake na kuitiisha.
VIKWAZO VYA KIUCHUMI.
Kwa kuwatumia EU na yeye mwenyewe USA,dhidi ya Russia ,bado wameshindwa kumtiisha na kumpinda.RUSSIA limebaki kuwa ni taifa imara.
Saud Arabia
Hawa hutumika kushusha mafuta ili bei ya mafuta ishuke ili kudhoofisha uchumi wa Russia,hii nayo ilifeli.
Haya ni machache tunayoyajua ,ni mangapi tusiyoyajua ,Je mpaka hapa USA haisaidiwi kuliangusha Dubu LILILOKATAA KUFA?
Haya ni maoni yangu tu,na hii ni makala ya kujifurahisha tu ili kuchangamsha ubongo,je si kweli kuwa USA inapewaga MISAADA kidili na URUSI?
Mjadala uko wazi.