Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Nilikuwa nasubiri hii speech ya Biden. Yaani nilikuwa nasubiri sentesi moja tuu kuwa we will protect Kiev militarily ila sijaisikia zaidi ya sanctions...more sanctions hahaaa...US kikaangoni.
 
Mkuu TUJITEGEMEE , Anthony Blinken kapiga simu Beijing kuomba wasadie kulinda uhuru wa Ukraine. Yaani Marekani atakuwa kwenye hali mbaya sana kama Uchina atakuwa upande wa Urusi: Uchina bado hajasema chochote, wala kuchagua upande mpaka sana. Tusubiri
 
Wakat urusi kalianzisha peke us wanaanza kupiga hodi ili kuungwa mkono
 
Mkuu michango yako ni shule tosha kwangu bila shaka na kwa wengine wengi...ni kati ya WanaJF wachache ndani hili jukwaa la Kimataifa unaeongea kitu chanye uhalisia.

Alikuwepo na Mwana JF mmoja Dotworld sijui alipotelea wapi, nae alikuwa mjuvi sana wa siasa za Urusi na Marekani.
 
Warusi wameongeza thamani ya bei ya gesi wanayoiuza Ulaya. Ujerumani amecheza karata yake ya kuusinzisha mkataba baina yake na Urusi. Na kama ulivyosema Ujerumani kwa kipindi kirefu anaitegemea Urusi kwenye hiyo sekta. Grafu ya gesi gharama yake ipo juu kwa nchi za Ulaya ikiwemo Ujerumani. Kwa Urusi kupandisha thamani ya mauzo yake ya gesi nao ni mtego kwa Kansela wa sasa wa Ujerumani. Sidhani kama raia wanaweza kuhimili upandaji wa gharama hiyo naiona kama harufu ya maandamano Ujerumani.

Namuona Ujerumani yupo kwenye wakati mgumu.
 
Niwe mkweli; haya masuala unayajua kuliko mimi/sisi. Sifahamu dunia inaelekea wapi ila kwa lugha nyepesi napata tabu Sana.

Russia ama Putin leo ametoa kauli nzito sana baada ya kutoa ufafanuzi sababu ipi inayopelekea Russia kutuma majeshi yake kulinda amani majimbo yaliyojitenga kutoka Ukraine na katoa onyo ya kuwa: "Yeyote atakayejaribu kutuzuia na kuleta tishia kwa nchi ya Urusi na kwa raia wake afahamu ya kuwa Urusi itajibu mapigo kwa haraka na kukuletea athari/sintofahamu ambayo hamkuwahi kukumbana nayo kamwe, na tupo tayari kwa matokeo ya aina yoyote."

Lakini kabla ya hapo aliwatahadharisha majeshi ya Ukraine kuwa lililobora kwao warudi majumbani mwao wakae na familia zao.

Tukirudi nyuma huu mgogoro ni mkubwa kwa maana umejumuisha mataifa makubwa tofauti tofauti. Kuna NATO, kuna Umoja wa Ulaya..kuna (na Marekani ijapokuwa ipo ndani ya NATO), Urusi jumlisha na Ukraine ambaye ndiye uwanja wa hii kadhia. Ukimsikiliza Putin mwisho wa hotuba yake kaishia na wanajeshi wa Urusi kwa utiifu wao ana imani watatimiliza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

Tunaona nguvu za kijeshi na kiuchumi kutumika. Nahitaji kujua, hii dunia kwa sasa inaelekea wapi?
 
I'm humbled you know.....
 
Urusi leo tena imeshambulia kinu kikubwa Cha nuclear nakukiweka under control baada ya wiki iliyopita kutwaa chenobry hii sass hatari na nadhani naanza kuelewa maana ya military operation anayoizungumzia bwana Putin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…