Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?


Kwanini unazungumzia vita vya kwanza vya dunia baadala ya vita vya pili vya dunia?? Ukitaka kuielewa Russia na iliyokuwa Soviet Union zungumzia WWII...Soviet union ndiyo iliyoiokoa dunia kutoka kwa Hitler...Eastern Front ambako Hitler alipambana na Soviet ndiko kulikoamua hatima ya WW II.
 

Naomba nikubaliane na wewe kwamba hakupoteza kila kitu, lakini kitaalamu mifumo ya nchi ikiparanganyika na kufa basi nchi inayozaliwa huwa nyingine kabisa. USSR ilikufa na RF siyo USSR:
Urusi ilipoteza mengi makubwa ndiyo maana NATO ikaamini kwamba Urusi hiawezi inuka tena.
1. Ilipoteza asilimia 23.8% ya eneo lake.
2. Iliopoteza asilimia 48.5% ya watu wake (Hili likitokea Tanzania haponi mtu)
3. Iliopoteza asilimia 41% ya GDP hapa nchi lazima ife.
4. Iliopoteza asilimia 39.9% ya nguvu ya viwanda (Angalia vizuri ukubwa wa hii asilimia)
5. Ilipoteza asilimia 44.6% ya mifumo ya ulinzi na mejeshi.


Kiuchumi nchi yoyote ikikutwa na haya majanga lazima ipoteane kabisa, Uingereza aliyemilika Asilimia 23% ya ardhi ya dunia hadi kufika mwaka 1923, aliuponyang'anywa maeneo kama India na Pakistan mwaka 1947-1948 hajaweza kuamka mpaka leo. Japo unaweza kusema hajapoteza kila kitu lakini The British Empire is no more.
 

Thanks comrade...Hivi ndivyo Jamii forums inavyopaswa kuwa...Asante sana ndugu yangu....hojaza aina hii huwafikirisha vijana wengi humu ambao hawajui kabisa masuala mengi ya dunia...wanachukulia 'uhasama' wa Russia na USA kama ushabiki wa Simba na Yanga...
 
Sawa kabisa Eastern Front ndiko kuliamua hatma ya vita ya pili ya dunia kwasababu Ujerumani alitumia asilimia 80% ya nguvu yake yote ya jeshi lakini akashindwa, hivyo The Great Patriotic War 1941 hadi 1945 ndiyo ilibadili mwelekeo wote wa vita ya pili ya dunia.

Japo sasa, kamwe huwezi kuzungumzia USSR bila kuzungumzia vita ya kwanza ya dunia (Haiwezekani)
Hadi Hitler anavamia USSR mwaka 1941 yote hii mzizi wake ulitokana na Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919-1920 ambao ulivunja Mkataba wa Brest-Litovsk ambao ulimfanya Urusi aweke silaha chini na kukubali kumgawia Poland na nchi nyingine za Ulaya Mashariki.


Hivyo ndugu yangu, lazima ukumbuke kwamba matukio yote ya karne ya 20 hasa yale makubwa kama Vita ya Kwanza ya dunia, Vita ya Pili ya dunia, Vita Baridi, Mapinduzi ya Oktoba yamefungamana sana na huwezi kusema unadiriki kuyatenga hata siku moja.
 

Sawa comrade...nimekuelewa....you are well informed and knowlegeable...congratulations....
 
Safi kabisa. VIVA PUTIN VIVAAAA
 
Duniani hapa kama una Technology na Leadership lazima tu utaendelea na hivyo ndivyo vitu ambavyo sisi kwa masikitiko makubwa hatuna.

Sisi kabla ya vita na Uganda tulikuwa na uchumi mzuri ktk ukanda wote huu lkn baada ya tu ya vita tuliambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18 lkn hadi leo hiyo miezi 18 haijaisha...!!!

Kwa nchi za wenzetu wanasiasa wanawaheshimu sana wataalam na hawawaingilii ktk utendaji wao wa kazi na haya yanayoongelewa humu ni matokeo ya kuheshimu fikra za wataalam.

Sisi tunafanya mambo tukilenga kupata sifa za kisiasa ili iwe mtaji ktk uchaguzi na watalaam wetu wamekuwa heavily brainwashed politically na wenyewe kwa kuendekeza njaa wamekuwa hawawezi ku-practise kile wanachokiamini hasa hilo likiwa tofauti na anachoamini mwanasiasa.

Tumeona mengi kwa akina Mwakyembe, Kabudi na wengine wengi tu. Angalia miradi mingi inayoanzishwa ktk nchi hii ni ile inayochochewa kisiasa pasipo kuangalia Economic Benefits / Viability au hata Environmental Impact zake.

Nchi kama Russia ktk elimu yao wameangalia nini wanahitaji kama taifa na waka-design curriculum yao mahsusi kulenga hicho na ndio maana wana bajeti kubwa sana inayotengwa kwa ajili ya Research kwani pasipo Research hakuna Innovation.

Russia wana kila sababu ya kuendelea na watazidi tu kuendelea kwani wanawekeza ktk maendeleo na wana sera thabiti zinazolenga ktk dhana nzima ya maendeleo. Sisi ngoja tuendelee kuwawinda wale wapinzani wanaokataa sera yetu ya kuunga juhudi.
 
Big up Comred, naona umeyachimbua madini kwelikweli....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Malcolm shida ni kwamba urusi ina wasomi wa tecnolojia kubwa ya kijeshi hakuna wanachoshindwa kutengeneza wakitaka
Na kumbuka NATO iko na inaongozwa na marekani kwa hiyo mrusi anapoona mmarekani yuko Karibu na NATO hasira zinazidi
Na NATO haiwezi kufanya jambo bila kuruhusiwa na Marekani


E&K
 
Wameshindwa kutengeneza stealth plane..
 
Ewaah, sawa kabisa na huu ndiyo msingi wa swali langu:
Sasa nchi ambayo imeshindwa kutengeneza Stealth Plane kama zile F-35 inawasumbuaje NATO ??
Uchumi uko chini, imewekewa vikwazo vizito na imetengwa, kwanini wasiimalize tu mara moja ???
Haiwezekani kuimaliza Russia bila kuweka usalama wa dunia nzima hatihati. Ukisha kuwa nuclear power to the level of Russia lazima uheshimiwe duniani bila ya kujali uchumi wako upo level gani.
 
Yes indeed! Hususani kijana kama Mimi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…