Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Huko Afghanistan itabidi akubali yaishe tu.. Majitu unayatandika sawasawa kesho ukiamka haya hapa..
Hao wafaghnistan hata Alexandre great nasikia alichemsha,,wale wanafanya vita katika mafungu ya miaka mia mia,
Wao na wayemen,,yaani wamebobea,,
Kule stan hii vita imeanza mtoto anazaliwa na sasa yuko Udsm bado inaendelea
 
Wataalamu wanaiita nchi ya Afghanistan, The Graveyard of Empires.
Dola la Makedonia walikwama kwenye milima ya Hindu-Kush, (330 K.B)
Dola la Muingereza nalo lilijaribu kupambana likakwama vibaya sana, (1838-1842)
Dola la Urusi ya Kisovieti walipambana kwa miaka 10 lakini wakakwama ,(1979-1989)
Dola la Marekani limeshakata pumzi tayari, sasa ni suala la muda tu, (2001-2020)
 
Sawa kabisa Eastern Front ndiko kuliamua hatma ya vita ya pili ya dunia kwasababu Ujerumani alitumia asilimia 80% ya nguvu yake yote ya jeshi lakini akashindwa, hivyo The Great Patriotic War 1941 hadi 1945 ndiyo ilibadili mwelekeo wote wa vita ya pili ya dunia.

Japo sasa, kamwe huwezi kuzungumzia USSR bila kuzungumzia vita ya kwanza ya dunia (Haiwezekani)
Hadi Hitler anavamia USSR mwaka 1941 yote hii mzizi wake ulitokana na Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919-1920 ambao ulivunja Mkataba wa Brest-Litovsk ambao ulimfanya Urusi aweke silaha chini na kukubali kumgawia Poland na nchi nyingine za Ulaya Mashariki.

Hivyo ndugu yangu, lazima ukumbuke kwamba matukio yote ya karne ya 20 hasa yale makubwa kama Vita ya Kwanza ya dunia, Vita ya Pili ya dunia, Vita Baridi, Mapinduzi ya Oktoba yamefungamana sana na huwezi kusema unadiriki kuyatenga hata siku moja.
Thanks comrade
 
Isis huwezi kuwaweka hapo, hao ni wahuni tu.

Hata hao waliopigwa ni wachovu tu,
Hao ISIL unaosema ni wachovu walizivuruga nchi mbili (Iraq and Syria) na kushika maeneo yake makubwa ndani ya muda mfupi sana. Kama ISIS wangekuwa ni kikundi cha Wahuni sidhani kama wangeweza kushindana na Syria wala Iraq kama ambavyo walifanya. Kibaya zaidi ni kwamba kupambana na kikundi kama ISIS inahitaji utaalamu wa mkubwa wa kijeshi kuliko kupambana na majeshi ya kawaida.

Hivi hushangai kikundi kidogo kama Al Qaeda kilisababisha madhara makubwa kwa nchi ya Marekani ndani ya muda mfupi kuliko madhara ambayo Ufalme wa Japani uliyasababisha kwa Marekani kwenye vita ya pili ya dunia mwaka 1941 kule Hawaii. Wajapani walitumia ndege za kivita zaidi ya 100 na waliua wanajeshi wa Marekani kama 2000, lakini Al Qaeda wao walikuwa na ndege za kiraia 4 tu na wakaua watu 3000. Sasa unaposema ni kikundi cha wahuni nakushangaa.

Vikundi vya wanamgambo kama ISIS, Al Qaeda, Al Shabaab, FARC na Taliban hutumia mbinu za vita zisizo rasmi (Irregular Warfare) ambazo zimekataliwa na sheria za vita kama uuaji wa raia, ubakaji, utekaji, uharibifu wa mali, ugaidi, uzandiki na hujuma nyingine. Mipangilio yao huwa ya kisiri na huchangamana na raia wa kawaida kama watoto na wanawake ambao huwezi hata kuwahisi. Kitendo cha Urusi kuwavunja uti wa mgongo migambo wa ISIS kimethibitisha kwamba jeshi la Urusi siyo la mchezo.

Urusi alijifunza somo zuri sana la jinsi ya kukabiliana na makundi ya kigaidi baada ya kuona madhara ambayo hivi vikundi vinaweza kusababisha. Migambo wa Kiislamu wa kule Chechnya ambao walifandhiliwa na Marekani, walilipa jeshi la Urusi na Mashirika ya kijasusi uzoefu mkubwa mno wa kupambana na magaidi.
 
Huyo Isis unayesema mchovu Marekani na washirika wake kawatoa jasho.pasipo Urusi IS wangekuwa washateka Dunia yote
Assad mwenyewe alikuwa anawamudu hao wahuni ndio iwe Marekani ?

Isitoshe Assad aliwaruhusu wapate nguvu kama mkakati wake wa kuwatumia kuwavunja nguvu maadui zake na kuhamisha magoli,mbinu ambayo ilifanikiwa.

Yaani Dunia ingetekwa na hao wahuni wanaotumia pickup? Acha utani bhana.
 
Hawa Isil walikuzwa mno na propaganda ila hawakuwa na nguvu kiasi hicho.

Kingine cha muhimu ni kuwa, jeshi la Assad hapo awali lilijikita zaidi kupambana na makundi mengine ya waasi (FSA) hivyo Isis wakabaki wanapambana na Wakurdi tu.

Assad aliwaacha Isis wapate nguvu makusudi ili kuwavunja nguvu wapinzani wake (FSA) na washirika wao hasa Uturuki na nchi za ghuba kumbuka hata Isis ilikuwa inapigana na FSA,hii mbinu ilimsaidia kwani Marekani na hata hizo nchi za ghuba isipokuwa Qatar na Uturuki ziliamua hatimaye kuachana na mpango wa kumg'oa Assad yaani kusitisha msaada kwa FSA na kujikita zaidi kupambana na Isis.

Hata huko Iraq, Isis ilinufaika na mgogoro uliokuwepo kati ya serikali ya waziri mkuu Al Maliki na Wasunii hivyo ilijipatia wafuasi wengi kwenye jamii ya wasuni na hata baadhi ya askari wa Iraq wa kisunni waliamua kuondoka kwenye uwanja wa Vita kwa kutoridhika na serikali yao, hivyo jeshi lilikosa morali na Isis kuteka maeneo kilaini.

Pia mbinu zao za kikatili na kujitoa mhanga ziliwapa mafinikio kwa kuingiza raia wengi waliokuwa wanaishi kwenye maeneo waliyodhibiti kuishi kwa hofu na kuogopa kuwapinga.

Hata Putin aliwatumia tu kama kisingizio cha kujiingiza Syria ili amwokoe Assad kama unakumbuka mashambulizi mengi ya Urusi yaliwalenga waasi wa FSA na machache yaliwalenga Isis.
 
Assad mwenyewe alikuwa anawamudu hao wahuni ndio iwe Marekani.

Yaani Dunia ingetekwa na hao wahuni wanaotumia pickup? Acha utani bhana.
US kwanza angemalizana na TALEBAN ila baada kuona ngoma ngumu wakaona wakaechini wayajenge.....
 
Assad mwenyewe alikuwa anawamudu hao wahuni ndio iwe Marekani ?

Isitoshe Assad aliwaruhusu wapate nguvu kama mkakati wake wa kuwatumia kuwavunja nguvu maadui zake na kuhamisha magoli,mbinu ambayo ilifanikiwa.

Yaani Dunia ingetekwa na hao wahuni wanaotumia pickup? Acha utani bhana.
Itakuwa Isis wa chanika unaowasema wewe.ila sio ninaowajua mimi. izo ni IRAQ na Syria bado yemen, afghanistan na Libya
800px-Territoires_de_l'Etat_islamique_juin_2015.jpeg
 
ukishajua lengo kuu la Western nations ni rahisi kujua kwa nini Russia ni tishio kwa nchi za magharibi in short ni mtu ambaye anawaharibia mipango yao na amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu,
 
Itakuwa Isis wa chanika unaowasema wewe.ila sio ninaowajua mimi. izo ni IRAQ na Syria bado yemen, afghanistan na LibyaView attachment 1490535
Hao wanaotembea na smg/ AK47 juu ya pickup walikuwa ni kama upepo mbaya tu kwa muda.

Ndiyo maana kwa sasa wamebaki historia.Ukiondoa propaganda hakuna cha zaidi walichokuwa nacho.
 
Hao wanaotembea na smg/ AK47 juu ya pickup walikuwa ni kama upepo mbaya tu kwa muda.

Ndiyo maana kwa sasa wamebaki historia.Ukiondoa propaganda hakuna cha zaidi walichokuwa nacho.
Ndo maana nikakwambia kuwa unaongelea Isis wa chanika, ila sio ninaowajua mimi.naona toyota wametoa pickup new model
images%20(14).jpeg
images%20(15).jpeg
images%20(16).jpeg

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom