Hao ISIL unaosema ni wachovu walizivuruga nchi mbili (Iraq and Syria) na kushika maeneo yake makubwa ndani ya muda mfupi sana. Kama ISIS wangekuwa ni kikundi cha Wahuni sidhani kama wangeweza kushindana na Syria wala Iraq kama ambavyo walifanya. Kibaya zaidi ni kwamba kupambana na kikundi kama ISIS inahitaji utaalamu wa mkubwa wa kijeshi kuliko kupambana na majeshi ya kawaida.
Hivi hushangai kikundi kidogo kama Al Qaeda kilisababisha madhara makubwa kwa nchi ya Marekani ndani ya muda mfupi kuliko madhara ambayo Ufalme wa Japani uliyasababisha kwa Marekani kwenye vita ya pili ya dunia mwaka 1941 kule Hawaii. Wajapani walitumia ndege za kivita zaidi ya 100 na waliua wanajeshi wa Marekani kama 2000, lakini Al Qaeda wao walikuwa na ndege za kiraia 4 tu na wakaua watu 3000. Sasa unaposema ni kikundi cha wahuni nakushangaa.
Vikundi vya wanamgambo kama ISIS, Al Qaeda, Al Shabaab, FARC na Taliban hutumia mbinu za vita zisizo rasmi (Irregular Warfare) ambazo zimekataliwa na sheria za vita kama uuaji wa raia, ubakaji, utekaji, uharibifu wa mali, ugaidi, uzandiki na hujuma nyingine. Mipangilio yao huwa ya kisiri na huchangamana na raia wa kawaida kama watoto na wanawake ambao huwezi hata kuwahisi. Kitendo cha Urusi kuwavunja uti wa mgongo migambo wa ISIS kimethibitisha kwamba jeshi la Urusi siyo la mchezo.
Urusi alijifunza somo zuri sana la jinsi ya kukabiliana na makundi ya kigaidi baada ya kuona madhara ambayo hivi vikundi vinaweza kusababisha. Migambo wa Kiislamu wa kule Chechnya ambao walifandhiliwa na Marekani, walilipa jeshi la Urusi na Mashirika ya kijasusi uzoefu mkubwa mno wa kupambana na magaidi.