Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Ahsante sana mkuu,
Sasa kama Urusi alikuwa na nguvu nyingi zaidi ya hizi za leo kwanini alishindwa Vita Baridi ??
Katika mantiki hii unataka kuniambia kwamba Urusi ya zamani ilikuwa na nguvu kuliko Marekani ??
Kwa fikra zangu, USSR haikuanguka kwa sababu ilikuwa dhaifu kiasi cha kuangushwa, la hasha. Yafuatayo yaweza kuwa yalisababisha.

Kwanza huenda moja ya majimbo yake halikuwa uchochoro wa maadui. Ukisoma historia ya kuanguka kwake, utagundua kuwa kuna maadui waliijenga ndani ya USSR ili kuidhoofisha.

Pili, wazungu si watu wa kuwaamini sana. Huenda ulikuwa ni muungano uliopangwa kwa malengo fulani. Baada ya malengo kufikiwa, hapakuwa na haja ya kuendelea na muungano ule. Kila mmoja akachukua njia yake. Nina uhakika kama lilikuwa basi ulikuwa ni mpango wa baadhi ya majimbo, na baadhi hawakuwa na hili wala lile.

Tatu, huenda kuna viongozi wa baadhi ya majimbo walirubuniwa na maadui hivyo kutoa msukumo wa kuvunja umoja ule kwa maslahi ya walioshawishi. Dhana hii ninaijenga kwa kuhusianisha na namna ambavyo Afrika inavyoshindwa kuimarisha umoja wao. Si kwamba viongozi wa Afrika hawawezi, bali shinikizo la maadui wa nje ya Afrika ndo hudhoofisha juhudi zao. Kiongozi yeyote wa Afrika anayesimama kidete kuiunganisha Afrika au kuonesha kupinga wazi uonevu wa wazungu kwa Waafrika, haachwi asogee hatua mbili mbele. Lazima lifanyike jambo kuvuruga.
 
Nadhani jibu ni kwamba,marekani yenyewe na muungano wa NATO nazo ni dhaifu na zimesambaratika pia.
Urusi na china,ni nchi ambazo zimeanza kujengeka na kuimarisha uhusiano wao kupitia BRICS.
Kwa hiyo,ni km nguvu mbili zinazopambana kuongeza nguvu na ushawishi wakati mmoja wapo akiwa anaelekea chini ya mzani na mwingine anainuka kupitia mzani huo huo ambao ni uchumi.
 
Wataalamu wanaiita nchi ya Afghanistan, The Graveyard of Empires.
Dola la Makedonia walikwama kwenye milima ya Hindu-Kush, (330 K.B)
Dola la Muingereza nalo lilijaribu kupambana likakwama vibaya sana, (1838-1842)
Dola la Urusi ya Kisovieti walipambana kwa miaka 10 lakini wakakwama ,(1979-1989)
Dola la Marekani limeshakata pumzi tayari, sasa ni suala la muda tu, (2001-2020)
Hapo mwisho utabiri wako uliuharakisha kidogo.

Ila umepotea sana siku hizi hapa intaneshno, mambo yamepamba sana moto kule mashariki ya mbali na hapo Ukraine, unahitajika sana sasa kuliko ilivyokuwa zamani.
 
Hapo mwisho utabiri wako uliuharakisha kidogo
Niliharakisha wakati Marekani ameshaondoka Afghanistan tayari, AU umeamua kujisahaulisha mkuu! Mimi niliandika mwaka 2020 Marekani atasalimu amri, mwaka 2021 Marekani akasalimu amri na kuondoka, nilikosea mwaka moja tu. Teh teh teh teh....!!!

Hivi unafahamu madhara ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama ambayo yataikumba Marekani na dunia nzima kwa kuondoka kwake kwa aibu kule nchini Afghanistani ???? Teh teh teh

PICTURE ME ROLLIN............ 😎 😎
 
Niliharakisha wakati Marekani ameshaondoka Afghanistan tayari, AU umeamua kujisahaulisha mkuu! Hivi unafahamu madhara ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama kwa Marekani na dunia nzima yaliyosababishwa na Marekani kuondoka Afghanistani kwa aibu namna ile ???

PICTURE ME ROLLIN............
Sana sana washirika wa Marekani hasa Saudia na baadhi ya nchi za ulaya zimeingia wasiwasi kuhusu hakikisho la Marekani kuwalinda..

....zaidi ya hapo hakuna madhara mengine kumbuka Marekani bado ina ushawishi mkubwa sana hapa Duniani
 
Niliharakisha wakati Marekani ameshaondoka Afghanistan tayari, AU umeamua kujisahaulisha mkuu! Mimi niliandika mwaka 2020 Marekani atasalimu amri, mwaka 2021 Marekani akasalimu amri na kuondoka, nilikosea mwaka moja tu. Teh teh teh teh....!!!

Hivi unafahamu madhara ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama ambayo yataikumba Marekani na dunia nzima kwa kuondoka kwake kwa aibu kule nchini Afghanistani ???? Teh teh teh

PICTURE ME ROLLIN............ 😎 😎
Ulikuwa ni utani tuu bro, naelewa hiyo miezi sita kabla ilikuwa kwenye margin of error.
 
Russia was a global power even before Putin was born, before the soviet union placed the first man in space. And yes even before America was a country.....
Maneno haya nimemkumbuka marehemu Prof. Stephen F. Cohen. Kwenye kumbukumbu zangu (kama zipo sawa) alizungumza maneno kama haya.

Nimejihisi na majonzi. Umerudisha kumbukumbu zangu za nyuma sana.
 
Putin na Urusi yake wanapenda sana chokochoko...

Hili la Sasa huko Ukraine huenda likamalizika kwa Urusi kumega tena ardhi ya Ukraine
Nilidhani kuanzisha vita ni jambo gumu kumbe ni rahisi sana. Mchezo ambao wanaoucheza Marekani+EU (NATO) ni wa hatari sana. Ni kama alivyosema Servei Lavrov ni kama unazungumza na bubu na kiziwi.

Putin leo amefanya kikao na baraza la usalama nchini mwake. Moja ya mambo yaliyozungumziwa wana baraza waliyopendekeza ni Russia kuyatambua majimbo mawili yanayopambana na jeshi la Ukraine.

Ila huu mchezo unahitaji mahesabu makali sana.
 
Putin leo amefanya kikao na baraza la usalama nchini mwake. Moja ya mambo yaliyozungumziwa wana baraza waliyopendekeza ni Russia kuyatambua majimbo mawili yanayopambana na jeshi la Ukraine.
Dah!...Putin alitambua majimbo yaliyokuwa yakipigana na serikali ya Georgia na huenda yakamezwa na Urusi hapo baadae.

Akaja akaimega Crimea na Sasa hili eneo la mashariki ya Ukraine huenda likamegwa...

Putin ameamua kuyaadhibu haya mataifa kwa kumega ardhi zao kibabe (huu si uungwana).
 
Maneno haya nimemkumbuka marehemu Prof. Stephen F. Cohen. Kwenye kumbukumbu zangu (kama zipo sawa) alizungumza maneno kama haya.

Nimejihisi na majonzi. Umerudisha kumbukumbu zangu za nyuma sana.
We dearly miss him, may his soul rest in peace.
 
URUSI KACHEZA MCHEZO WA AKILI KUBWA MNO HII LEO:
Ametangaza kuyatambua majimbo ya Donbass (Lugansk and Donestky) kama nchi huru, kama ilivyokuwa Crimea mwaka 2014. Hii sasa ndiyo HYBRID-WARFARE, wanacheza na jeshi, diplomasia, siasa kwa pamoja. Marekani kawekwa kwenye mtego mbaya sana, maana nchi kama Uchina ikiyatambua haya majimbo, hata kama Marekani na washirika wake watagoma, kazi itakuwa imekwisha.

Lakini kubwa na la kuogopesha, ni kwamba kitendo hiki kitaipa uhalali nchi ya Urusi kuweza kupeleka vikosi vyake vya kijeshi kwenye yale maeneo ya Donbass, kwasababu tayari zimeshakuwa nchi huru. Hapa Marekani na Ukraine wakicheza vibaya tu, watapata tabu sana. Marekani anamchokonoa Uchina kule Taiwan, Hong-Kong na Xinjian sasa Uchina anaweza kuyatambua majimbo ya Donbass na ikala kwake.

Vladmir Putin, hate him or love him: The Dude is way ahead of his time.
 
RAISI VLADMIR PUTIN AMEAMURU URUSI IPELEKE VIKOSI DONBASS:

Baada ya eneo la Donbass kuwa huru, Raisi wa Urusi amempa maelekezo Waziri wa Ulinzi kupeleka vikosi vya kutunza amani na usalama kwenye nchi mpya ambazo ni za Donesty na Lugansk. Pia katoa maelekezo waanzishe mazungumzo ya haraka na nchi hizo ili kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia.

Yaani hajatumia kabisa kuimega Ukraine maana kwenye sheria za kimataifa hajafanya lolote lile. Mikataba ya Umoja wa Mataifa inatambua haki ya watu kujitawala wenyewe (A Right to self-determination). Yaani, hii kwenye mchezo wa CHESS tunaita CHECK-MATE, Urusi ametumia mchezo wa Marekani kumshinda Marekani. Tena kafanya kisasa, bila kumwaga damu kama Marekani.....

Hebu tuone Marekani na washirika wake watafanya nini kukabiliana na hili......
 
URUSI KACHEZA MCHEZO WA AKILI KUBWA MNO HII LEO:
Ametangaza kuyatambua majimbo ya Donbass (Lugansk and Donestky) kama nchi huru, kama ilivyokuwa Crimea mwaka 2014. Hii sasa ndiyo HYBRID-WARFARE, wanacheza na jeshi, diplomasia, siasa kwa pamoja. Marekani kawekwa kwenye mtego mbaya sana, maana nchi kama Uchina ikiyatambua haya majimbo, hata kama Marekani na washirika wake watagoma, kazi itakuwa imekwisha.

Lakini kubwa na la kuogopesha, ni kwamba kitendo hiki kitaipa uhalali nchi ya Urusi kuweza kupeleka vikosi vyake vya kijeshi kwenye yale maeneo ya Donbass, kwasababu tayari zimeshakuwa nchi huru. Hapa Marekani na Ukraine wakicheza vibaya tu, watapata tabu sana. Marekani anamchokonoa Uchina kule Taiwan, Hong-Kong na Xinjian sasa Uchina anaweza kuyatambua majimbo ya Donbass na ikala kwake.

Vladmir Putin, hate him or love him: The Dude is way ahead of his time.
[emoji23] [emoji23] Subiri waje wakwamtongole humu wamekasirika balaa
 
Back
Top Bottom