Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Siyo kuwa ninataka kukubalika, ila sipendi kuchafuliwa jina kwenye jamii yetu. Ni afadhali wawe wananyamaza tu kuliko kunijengea jeshi la uadui dhidi yangu huko nyumbani ambapo ni kwetu sote!
mkuu ni afadhali umeziona tabia zao mapema ili ujue unadeal na watu wa aina gani
Kiufupi ndugu zako hawana shukrani na kuna kila dalili kuwa wewe ndio tegemeo la ukoo na ndugu zako baadhi hawafurahii hali hiyo ndio maana wanatafuta kila sababu ya kukuonesha wewe ni mbaya ili kukudogosha na wao waonekane bora zaidi yako mbele za watu
Kitendo cha wao kutumia uwezo wako ili watoto wao wawe kama wako hakitoishia hapo. watataka wawe zaidi ya wa kwako someday ili wajione ni bora zaidi
hizo ni nafsi zao na unatakiwa kuwa makini nazo. Wasaidie tu ili watoto wao wasije kuwa mizigo kwa wanao ila usitarajie CHOCHOTE kutoka kwao