Swali Gumu: Kwanini kila ninayemsaidia huwa hana shukrani?

Swali Gumu: Kwanini kila ninayemsaidia huwa hana shukrani?

Inaonekana unajali sana maneno ya watu/ndugu

Kwa kawaida inabidi ufanye yale unayoweza tu na wala usitarajie chochote kile in return!

Ukiwasaidia watasema, usipowasaidia watasema na hayo ndio maisha yalivyo! Saidia kulingana na nafasi yako yaliyobakia hayakusu tena!!
 
Ukiwa unatenda wema na kutarajia urudishiwe chochote huo hukuwa unatenda wema bali unafanya biashara

Mm kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa inatakiwa afanyiwe operations mbili moja ya kongosho na nyingine ya tezi dume na alikuwa na sh 60000 but gharama za pale kcmc hospital ni 2.3ml

Nkaampa bima yangu akafanyiwa operations zote hizo kwa bima yangu,nilijitoa tu kama rafiki wala sikuwa natarajia chochote kutoka kwake

Alivyopona akanitoa na konyagi ndogo ya 3500,
Ila mpaka Leo akiniona ananikimbia cjui ni kwa nn?
Hahahaha nimecheka kama mazuri Ila yote Kwa yote binadamu wachache sana wenye kushukuru
 
Zamani sana bendi moja hapo Dar: ama Dar es salaama Jazz au Western Jazz iliimba kuwa "Tenda Wema, nenda zako, usingoje shukurani". Maudhui ya wimbo huu yamesharudiwa na waimbaji wengi sana siku za hivi karibuni.

Mimi ni mtu wa makamo sana wakati huu na katika maisha yangu nimeshasaidia watu wengi sana, jambo ninalojivunia mno. Kila msaada ninaotoa huwa ina maana ya mimi na familia yangu kujinyima ili tuwasaide wengine, siyo kwamba huwa nina dimbwi kubwa la pesa za kuchota bure bure bure.

Sasa kinachonishangaza ni kuwa ndugu na marafiki wengi niliowahi kusaidia huwa hawaonyeshi shukrani yoyote ukilinganisha na wale ambao huwa sina uhusiano nao. Ndugu na marafiki huwa wanataka zaidi wala hawawezi kutosheka na msaada, na ikitokea nikasema sasa msaada niliokwishatoa unatosha inabidi ajiendeleze mwenyewe, basi wananilaumu kama vile kile nilichokwishawafanyia siyo kitu kabisa. Yaani wanakuwa wananiongea vibaya tu bila shukrani yoyote.

Ni wapi ninapokosea katika kusaidia ndugu na marafiki ili watambue msaada wangu kwao?

Kuna mmoja nilimlipia mtoto wake kwa miaka minne mfulizo chuo kikuu cha dar es salaama wala hakuchukua mkopo wa serikali, akamaliza na 3rd class. Sasa mtu huyo ananilaumu kwa nini simsaidii mtoto huyo kusoma masters! Kibaya anatumia lugha mbaya kuwa nina wivu sipendi watoto wake waendelee kama mimi wakati bado ninasaidia mtoto wake mwingine ambaye yuko sekondari ninayomlipia mimi!!
Wewe ni mjinga , am sorry.
Una kipato kizuri na una roho nzuri ila umeshindwa kujua kuwa ndugu wa Kiafrika ni nusu mtu nusu shetani.
Huo ndio ujinga wako
 
Ukiwa unatenda wema na kutarajia urudishiwe chochote huo hukuwa unatenda wema bali unafanya biashara

Mm kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa inatakiwa afanyiwe operations mbili moja ya kongosho na nyingine ya tezi dume na alikuwa na sh 60000 but gharama za pale kcmc hospital ni 2.3ml

Nkaampa bima yangu akafanyiwa operations zote hizo kwa bima yangu,nilijitoa tu kama rafiki wala sikuwa natarajia chochote kutoka kwake

Alivyopona akanitoa na konyagi ndogo ya 3500,
Ila mpaka Leo akiniona ananikimbia cjui ni kwa nn?
kwenye bima kumbe inawezekana hapo?
 
Wewe ni mjinga , am sorry.
Una kipato kizuri na una roho nzuri ila umeshindwa kujua kuwa ndugu wa Kiafrika ni nusu mtu nusu shetani.
Huo ndio ujinga wako
Sukutegemea matusi hapa, ila hata Bill Gates hutoa sana misaada duniani kote. Sina uwezo wa Bill Gates, hivyo misaada yangu nikawa ninaweka kwenye ukoo tu. Kama huo ni "ujinga+- ambalo mimi naona kuwa ni tusi, basi samahani sana.
 
Tofauti ni scenario tu ila context ni ile ile.

Lea nuclear family kwa nafasi, acha kuwabana eti unasaidia.
Usitegemee shukran toka kwa uliyemsaidia na ukisaidiwa move on. Kwanza tabia za kusaidiana saidianabzinachangia uvivu na kuchochea utegemezi.
Kuna kipoint nimekinyaka hapa🤗
 
Wanadamu si wa kuwaendekeza hata kidogo.
Yaani kinachokukuta ww ni kama mimi japo mimi sijawahi lipia mtu ada. Mtu akikuomba unampa ila siku akikuomba ukawa huna basi inakuwa lawama. Inavunja sana moyo.
Ninachoshangaa mimi sijawahi sononeka au kumlaumu mtu kwa kushindwa kunisaidia.
 
Weka nia ya kupata malipo kwa Mola wako kwa Wema ufanyao

Si bora wewe hawaoneshi shukran…mwingine anasema kabisa Jamaa Misifa sana anapenda kujifanya anazo

Au Ukiyumba utaskia Kiko wapi…enzi hizo ukimuomba elf 10 anakupa 20
 
Mkuu unawalipiaje ada watoto wawili wa mtu mmoja? Ni kwamba hana namna kabisa, yeye kuzaa kusomesha unasomesha wewe?. Wema usizidi ndio maana hawathamini unachowafanyia maana hawajui ugumu wake.
 
Ndugu nimewachoka sana miye sasa hv naishi nao km hawapo
Bora wewe! Narudia bora ndugu zako!
Dadangu ananifanyiaga figisu za ajabu ....yy figisu zake anachotaka anione nikiwa OMBA OMBA kama yeye !aliwah mwambia beki 3 atafute kwa hali na mali leseni yangu ya madini sijui alitaka aifanyie nn!!..🙌🙌...majuzi changamoto ya upumuaji ikanipata naskia akawa anasema ehee . Naskia corona haitibiwi kwa bima🤣! Akihisi nitasanda chaaa!
 
Weka nia ya kupata malipo kwa Mola wako kwa Wema ufanyao

Si bora wewe hawaoneshi shukran…mwingine anasema kabisa Jamaa Misifa sana anapenda kujifanya anazo

Au Ukiyumba utaskia Kiko wapi…enzi hizo ukimuomba elf 10 anakupa 20
Bwana wee..bwana weee ..ngoja niishie hapa
 
Labda kajiridhisha Wewe ni Muhujumu Uchumi na Tapeli uliotapeli Mfuko wa Bima ya Afya kwa kumpa kadi Mtu asiestahiki
Ukiwa unatenda wema na kutarajia urudishiwe chochote huo hukuwa unatenda wema bali unafanya biashara

Mm kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa inatakiwa afanyiwe operations mbili moja ya kongosho na nyingine ya tezi dume na alikuwa na sh 60000 but gharama za pale kcmc hospital ni 2.3ml

Nkaampa bima yangu akafanyiwa operations zote hizo kwa bima yangu,nilijitoa tu kama rafiki wala sikuwa natarajia chochote kutoka kwake

Alivyopona akanitoa na konyagi ndogo ya 3500,
Ila mpaka Leo akiniona ananikimbia cjui ni kwa nn?
 
Bora wewe! Narudia bora ndugu zako!
Dadangu ananifanyiaga figisu za ajabu ....yy figisu zake anachotaka anione nikiwa OMBA OMBA kama yeye !aliwah mwambia beki 3 atafute kwa hali na mali leseni yangu ya madini sijui alitaka aifanyie nn!!..🙌🙌...majuzi changamoto ya upumuaji ikanipata naskia akawa anasema ehee . Naskia corona haitibiwi kwa bima🤣! Akihisi nitasanda chaaa!
Duuuh pole sana, miye hadi wanajua kuwa sitaki masihara nao. Jibu langu moja tuu ICU, kuna last born wetu amepata kazi huko Bakharain wanamtafuta hata kuniuliza wanashindwa. Na mzee alipofariki wanamtafuta kuniuliza wanashindwa wanabaki kunikodolea macho. Miye kimya km askari kakosa posho washenzi sana hawaridhiki kila ukifanya padogo.
 
Back
Top Bottom