Swali Gumu: Kwanini kila ninayemsaidia huwa hana shukrani?

Anajionea aibu.
Halafu huyo rafikiyo fala kweli mana sio lazima akurudishie angejiweka tu karibu na wewe kama zamani mana humdai ni umejitolea tu sasa kukukimbia kunamsaidia nini
 
unayoyapitia ndio nnayopitia mm kwa marafiki zangu ila kikubwa no kuamini kwamba kulipwa na Mungu ni heri kuliko shukrani za mwanadamu
 
Nadhani pia tatizo lingine linakujaga pale mtu anasaidia kweli ila kila mtu atajua umesaidiwa na fulani.
Yaani anakusaidia ila atatangaza kila mahali kuwa nimemsaidia fulani alikiwa hana hili na hili.
Msaidie mtu kimya kimya yeye ndio akupe sifa pale anapokuta watu wanakuongelea vibaya akusifie.
Na wengine mnasaidia ila na masimango juu.
Ila kuna watu hawanaga shukrani jamani na wala aibu haoni yaani umemsaidia una matatizo wala hataki kujua wala kuhangaika na wewe mbaya zaidi atakuletea shida zake sasa na anataka umsaidie bila kujali kuwa wewe mwenyew upo katika kipindi gani
 
Pole mkuu hao ndio binadamu,tafuta story moja ya "NGANO YA PUNDA" ukiisoma vizuri hakika hutoumiza kichwa kwa binadamu.
 
Pole mkuu.WENZIO YALISHATUPATA NA TUKAELEKEZWA FORMULAR YA KUISHI NA NDUGU JAMAA NA WATU WA KARIBU.ILI UISHI KWA AMANI NA BILA FITNA UZUSHI HUSDA NA ROHOMBAYA KUNA KANUNI NA KANUNI HIZO NI:
1.Ishi mbali na ndugu wa tumbo moja.
2
Wajengee watu wako wa KARIBU uwezo wa kujishughulisha kivyao na achana nao
3..Ndugu,jamaa na WATU wa ukoo wako wasijue mipango yako ya pesa na ukwasi ulio nao
 
Na wni mzembe kata mawasiliano. Una acha kusaidia watoto wako unategemea hao wa ndugu. Hawana msaada wowote kwako in the future. Na usipoteze hata mia tena
 
UWE UNASOMA NENO LA MUNGU ILI UJUE MWANADAMU NI KITU GANI/KIUMBE GANI.


Kama sio muumini basi soma quraan na biblia kama tunzi tu za wajanja nayo yaweza kuwatambua bin adam.
Ni Qur-an tuu ndio kitabu pekee kilicho mueleza kwa undani mwanadamu na jinsi ya uumbwaji wake hadi matilio yake....
Binadamu ni kiumbe cha ajabu.. Ukimsaidi tabu, Usipo msaidia tabu..
Nilimuingiza kazini mtoto wa dada yangu baba mmoja na mimi..
Alivyoanza kupata pesa akawa jeuri kupindukia.. Nikamtimua kazini basi akanishushia fulushi la matusi na nikamtia adabu weka nyuma ya nondo miezi sita..
Alipotoka heshima na adabu japo Mama yake aongei na mimi.. Na mimi naona poa tuu..
 
Ni kukosa maarifa tu na ujinga kumlaumu mtu ambaye sio mzazi wako eti hajakusomesha, hata kama ni ndugu wa karibu ,sio Kazi yake kukusomesha, madam uliwasaidia wamefika mahala,endelea na maisha Yako,ukipata mwingine wa kusaidia kama mfuko unakuruhusu saidia tu
 
Pole na HONGERA.mkuu Kuna matukio makubwa matatu nili yafanya kwa ndugu na marafiki ambayo yananifanya niwe mgumu kuendelea na kuwasaidia kwa KIWANGO Cha 100%
Nili somesha watoto was ndgu.nikaona Bado nina deni
Nikanunua VIWANJA 20 na mashamba nikawagawiya vyote kila mtu ki 1 na shamba waliopenda mashamba.Hapo Ni ndugu,jamaa na marafiki wa KARIBU.baada ya hapo nikagundua baadhi hwaawezi Jenga kwa kuwa uchumi mdogo nikajitahidi kutafuta mshiko na kuwapa mitaji na shughuli za kufanya.
ANGALIZO MKUU:
KAMA NI KAZI MTAFUTIE SEHEMU NYINGINE.NA KAMA NI BIASHARA USIMUWEKE KTK BIASHARA YAKO AU OFISI YAKO ASILANI SIJUI HUINGIWA NA SHETANI GANI ATAANZA KUTAMANI UHARIBIKIWE ANASAHAU KUWA HATA YEYE ANATEGEMEA KULA YAKE HAPO
 
Mimi walinilani mpaka wakasahau kama Dua utakayo muombea mwebzio ndio itakayo kupata.. Nilimvuta Mzee pembeni nikampa ile wazungu wanasema fact.. Mungu amrehemu yule Mzee.. Akananiambia sikia Wafazilika wapundaka kaza buti nakutakia kilabla kheri.. TRA wali piga tukio nikawa hoi. Basi wale nilio wasaidia wakafurahi nikasikia na baadhi wakafanya sherehe ya kiko wapi...
Nikapigwa tafu na mtu nilie kwisha msahau kama kuna wema nilimfanyia..
Aysee maisha safari ndefu sana Ashukuriwe alietuleta hapa duniani..
Mimi niliwahi kula chakula kunacho semekana kina sumu,,bado kidogo niuwache huu ulimwengu dhaifu..
Ikawa haitoshi nilupo kuja Tanzania gari yangu ikalegezwa natt tairi za mbele..
Mkuu saidia lkn usisaidie nyoka..
 
Hata Wana wa Israel walikuwa wanashushiwa chakula na Mungu lakini bado hawakuridhika wakawa wanamwmbia Musa mwambie Mungu wako tumechoka chakula cha kushushiwa tunataka tupike wenyewe...
😀😀😀😀😀😀😀
 
Duh! Mkuu mm nkipata ndugu kam wew hata kunishauri Tu ni zaid ya kuwa na mamilion y ndugu wanafki. Anyway kam umeamua kutoa toa mungu atakulipa
 
Hao unao wasomesha wape darasa kuwa nsaada una kikomo.

Wengine wasiosoma kabla ya kuwapa pesa watafutie walimu wa ujasiliamali wawafundishe kwanza Elimu ya ujasiliamali.

Baada ya kuwapa mafunzo wape hicho kiasi unachotaka kuwapa Kwa masharti ya kurejesha.Wasiporejesha unakuwa huna lawama
 
Kweli kabisa
 
Hao unao wasomesha wape darasa kuwa nsaada una kikomo.

Wengine wasiosoma kabla ya kuwapa pesa watafutie walimu wa ujasiliamali wawafundishe kwanza Elimu ya ujasiliamali.

Baada ya kuwapa mafunzo wape hicho kiasi unachotaka kuwapa Kwa masharti ya kurejesha.Wasiporejesha unakuwa huna lawama
 
Hakika.NILISAIDIA ILI NIWE MBALI NAO .
KUNA ANGALIZO KAMA HUTA WASAIDIA KABISA WATAKACHO FANYA
1.Waku majanilize.
wakishindwa Hilo
2.wakurestishe mwisho wa yote watakutesea familia nzima mkuu, kwa maana kizazi chako
 
Iko hivi, ukimsaidia ndugu huo ni wajibu siyo msaada ndiyo maana hawezi kukushukuru au kurudusha fadhila kwa lolote.
Pili, hakuna mtu muhutaji aliyewahi kutosheka na msaada, unajua msaada ni kama vile mtu anaumwa njaa ukimpa chakula wakati huo atashiba ila baada ya muda atahisi njaa tena ko itabidi atafute chakula tena, , , , sasa ni mara mia zaidi kumsaidia kitu kinachoonekana kuliko pesa ya moja kwa moja kwani ikiisha hatakumbuka kama ulimpa anachohutaji ni apate tena lkn ukimpa kitu cha kumpa fedha atakukumbuka maisha yote hadi anakwenda kaburini.

Mwisho msaada kwa ndugu hauna baraka, baraka utazipata kutoka kwa mtu usiye na uhusiano wa damu naye chukua hiyo, hata usipoona kwako huzo baraka zitakuja kwa uzao wako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…