Swali Gumu: Kwanini kila ninayemsaidia huwa hana shukrani?

Mkuu unawalipiaje ada watoto wawili wa mtu mmoja? Ni kwamba hana namna kabisa, yeye kuzaa kusomesha unasomesha wewe?. Wema usizidi ndio maana hawathamini unachowafanyia maana hawajui ugumu wake.
Huyo mtu ni ndugu yangu wa karibu, ila wakati mimi nanasoma shule yeye alikuwa akila maraha sana wala hakupata elimu ya kutosha; alitumia ujana wake vibaya. Sasa matokeo yake anaishi na familia yake maisha duni sana kiasi kuwa familia yake inapokuwa na matatizo yanayohitaji hela, wanaenda kuomba msaad kwa mama yangu mzazi ninayemlea mimi; hivyo mama analazimika kuwagawia sehemu ya allowance ambayo huwa ninampa. Nikaona kuwa kuondoa tatizo hili ngoja nisaidie watoto wake wapate elimu kusudi waje wachukue responsibility hiyo - yaani kuvunja vicious circle of poverty kwake. Sasa mpaka mtoto amemaliza digrii bado anaomba msaada! Naona ni kama vile tatizo liko kwenye damu.
 
Ndo walimwengu walivyo.

Hakuna ubaya mtu kukushukuru kwa chema ulichomfanyia.

Ndo ustaarabu huo.

Hata mimi watu wa hivyo ninao sana.

Mtu unamsaidia zaidi ya mara 10.

Hakuna ahsante hata moja.

Siku ambayo huwezi kumsaidia, anaanza kukutangaza kwa watu u mchoyo!

Kushukuru ni uungwana na kusambaza uzushi ni ushenzi.
 
Kwahiyo huyo Ni ombaomba mtaalamu(a Professional Bagger)
 
Du!!!!
 
Wewe ni mjinga , am sorry.
Una kipato kizuri na una roho nzuri ila umeshindwa kujua kuwa ndugu wa Kiafrika ni nusu mtu nusu shetani.
Huo ndio ujinga wako
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16]
 
Mkuu unawalipiaje ada watoto wawili wa mtu mmoja? Ni kwamba hana namna kabisa, yeye kuzaa kusomesha unasomesha wewe?. Wema usizidi ndio maana hawathamini unachowafanyia maana hawajui ugumu wake.
Vry true
 
Wanawake wana wivu sana...huwa nawakwepa hata ndugu zangu wa kike

Kuna mtoto wa mamaangu mdogo ile nimeenda kuoga tu akawa anachoma dawa huku ananena jina langu asee...
 
Mkuu funguka vizuri nani aliweka sumu? Kulegeza nati tairi
 
Tenda mema usingoje shukrani cheka na watu wote Muzamir Katunzi.

Your browser is not able to play this audio.
 
Wanawake wana wivu sana...huwa nawakwepa hata ndugu zangu wa kike

Kuna mtoto wa mamaangu mdogo ile nimeenda kuoga tu akawa anachoma dawa huku ananena jina langu asee...
Unaona sasa🤣🤣!yaani sijui kwanini inakua hvyo..mie hata sinaga mpango naye maanaaisha anayoishi ya kuomba omba ni adhabu tosha..kila anachofanya hakifanikiwi ..anapewaga mitaji mirefu balaa...mie kimyaa
 
Uwezo wa kuwasomesha ninao; ninachochukia ni hiyo tabia yao ya kutokutambua kuwa maisha siyo mtelemko tu. Halafu watoto wan huwa hawana makosa; hawakuchagua kuzaliwa na mzazi asiyekuwa na akili !!
 
Unaona sasa[emoji1787][emoji1787]!yaani sijui kwanini inakua hvyo..mie hata sinaga mpango naye maanaaisha anayoishi ya kuomba omba ni adhabu tosha..kila anachofanya hakifanikiwi ..anapewaga mitaji mirefu balaa...mie kimyaa
Atakuloga tu huyo kuwa nae mbali, ana wivu mpaka umekuwa sumu [emoji848][emoji848]

Be careful
 
Hongera kwa kujaliwa na roho ya kusaidia.Kumbuka neno wema hauozi.

N baraka utalipwa hata kwa wajukuu wako .Ikiwa unasaidia usiwe unategemea kupata chochote kutoka kwa hao uwasaidiao.Ipo siku hizi shukurani zitakuja kwako au hata kwa vizazi vyoko.
Mfano kuja kutokea katika familia yako Kama vile mtu kuwa tajili mkubwa Sana / kuwa kiongozi mkubwa Sana .

Kanuni ukitoa kwa kusaidia toa kwa Nia njema na sio kwa kujikweza au kutangaza kwa watu kwamba unasaidia haitafanyika baraka .

Kila la heri
 
Loooh! Pole sana kaka, hali hii imetupelekea sisi wengine kuwa katili kwa watu, yaani sio kwamba hatusaidii, tunasaidia ila hatutaki mazoea tena, mara baada ya kutoa msaada. Hii inafanya wengi kutuita katili watu wa aina yangu. Ila ndiyo maisha niliyochagua, nimeshaumizwa sana kama wewe, nikakaa chini na kusema SASA BAAAASIII!
 
Upo timamu kweli wewe? Yaani unafurahi na kucheka kabisa? Mtu anakuombea kifo halafu unacheka?
 
Jamaa una roho mbaya hatari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…