GE2025 Swali hili la Kiranga kwa Polepole lilipuuzwa: What is Polepole's strategy? Lilifanya Kiranga atukanwe sana

GE2025 Swali hili la Kiranga kwa Polepole lilipuuzwa: What is Polepole's strategy? Lilifanya Kiranga atukanwe sana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sasa huyo polepole anamjua huyo kiranga?

Umeandika mashudu 🗑️
Tunaongelea hoja, si lazima Polepole amjue Kiranga.

Ila, watu wanaomfuatilia Polepole ni muhimu waelewe Polepole ni nani?Anataka nini? Anachotaka anatumia mbinu gani kukipata? Je, kwa mbinu hizo atafanikiwa? Au anaj8pa matumaini tu bila mkakati wa kueleweka?

This way, hata kama mtu anataka kumsaidia Polepole anaweza kumsaidia vizuri kwa kuelewa mpango mzima.

Au mtu anayetaka kumkosoa Polepole, anaweza kumkosoa kimantiki si kwa muhemko tu.

Si kumfuata mtu kwa kushabikia mambo kindezi tu halafu mnaishia kutekwa na kuuawa.

Ushaelewa?
 
Wakina Mange wanaofanyia harakati marekani si kila siku mnawaambia warudi tuandamane wote. Watanzania mnatakaje

Polepole hajaandamana.
Ameunga mkono maandamano.

Ilitakiwa wale wa mbele wakina Mange. Polepole . Fatma karume na etal waandamane na wakamatwe au wasionekane .

Hili ndio litaamsha Hasira za watz.
Hasira za Watz ziko mbali ila zikiamka hazitatulizwa. Maana watu ni wengi. Hasa vijana.

Ila hasira hazijapanda bado.
 
Wenye akili kumzidi strategy zao ushawahi kuziona zikifanya kazi popote? Uhalisia ni kuwa akili kubwa za humu ndani ni za maandishi/maneno, kwenye maandishi na maneno zipo akili kubwa kweli humu ila zinaishia kwenye maandishi tu hakuna matokeo.
Akili kubwa za humu ndani ni za maandishi
Duh
Kwahiyo unataka wafanyeje mkuu

Ushauli wako tunauomba
 
Ni swali la kidhahania, si lazima aseme. Aseme, asisema, swali lipo tu.

Kwa sababu kinachojadikiwa ni hoja, si mtu.

Mfano Fidel Castro alipovamia Cuba na Che Guevara mkakati wao ulikuwa wa kijeshi mpaka wakaichukua nchi.

Mandela na ANC walikuwa na mkakati wa kuwabana makaburu kwa vijwazo vya kinataifa, migono ya ndani, maandamano, mpaka kikaeleweka.

Ndiyo tukauliza, huyu Polepole ana mkakati gani?

Maana kusema serikali tu kila mtu anaweza, lakini then what?

It turns out Polepole si tu hakuwa na mkakati wa kukomboa nchi, hakuwa hata na mkakati wa kujilinda yeye mwenyewe.

Watanzania wengi wanapenda kufanya mambo kwa emotions, bila logic, bila mkakati, bila intentionality.

Polepole wengine walifikiri kavuka maisha hayo, lakini matukio yameonesha yuko palepale tu.
Wamemuwahi, Sawa?

Mengine yote umepata kuweka conclusion based on kilichotokea tar 6.
 
Tunaongelea hoja, si lazima Polepole amjue Kiranga.

Ila, watu wanaomfuatilia Polepole ni muhimu waelewe Polepole ni nani?Anataka nini? Anachotaka anatumia mbinu gani kukipata? Je, kwa mbinu hizo atafanikiwa? Au anaj8pa matumaini tu bila mkakati wa kueleweka?

This way, hata kama mtu anataka kumsaidia Polepole anaweza kumsaidia vizuri kwa kuelewa mpango mzima.

Au mtu anayetaka kumkosoa Polepole, anaweza kumkosoa kimantiki si kwa muhemko tu.

Si kumfuata mtu kwa kushabikia mambo kindezi tu halafu mnaishia kutekwa na kuuawa.

Ushaelewa?
Mi nadhani lengo lake lilikuwa ni kusema ukweli ,ukweli watu wengi zaidi waujue na amefanikiwa hilo kwa nafasi yake.
Safari hatua.
 
Mi nadhani lengo lake lilikuwa ni kusema ukweli ,ukweli watu wengi zaidi waujue na amefanikiwa hilo kwa nafasi yake.
Safari hatua.
Ukweli angeweza kusema hata hapa JF bila kutumia jina lake.

Tena hapa angeweka kufunguka mengi ya ndani kabisa.

Strategy maana yake mtu kuwa na end game.

Unapojitokeza na kusema alivyosema, end game yake ilikuwa ni ipi?

Alitegemea nini?

Alitegemea angeishi kwa kujificha Dar mpaka lini?

Polepole alimuwekea sharti Samia asigombee urais, ama sivyo atamwaga mboga, Samia atakiona.

Samia kagombea urais.

Polepole kafanya nini?

Alikuwa na strategy gani zaidi ya malalamiko ya kawaida ambayo raia yeyote angeweza kulalamika?
 
Mnataka wote mfanane mbinu na mawazo? Mbona hata yule Yesu kristo wapo wanaosema kama alikuwa na nia ya kuwakomboa watu kwanini asingetumia Nguvu zake kukwepa mateso ya waliomsurubisha?, jibu ni kuwa kila mtu na aina yake ya Ukombozi anaouona unafaa.

Ni bora yeye kuliko sisi humu na ID zetu feki kutwa kujifanya watetezi na wajuaji wakati tunaogopa hata kuandamana kuteta haki zetu.

Wanaojidai kumkebehi polepole waulizwe wao hata wakiishi miaka 100 wataacha legacy ipi kwa taifa?, utaona hawatofikia hata robo ya alichokifanya huyo bwana.

Kajitoa sadaka ambayo waoga wa TANZANIA hatuwezi na tunamshangaa, na kuna wale TAKATAKA wanaopendelea kusema hao wanaotetea maandamano kwanini wasirudi nchini, mbona hata huyu wa nchini mnaumia kuwepo?

Ni ngumu sana kumuelewa mtanzania mpumbavu,
 
horses for courses, Amefanya kwa nafasi yake (kujitoa sadaka kikondoo)

Ametekwa na pengine ameuawa/atauawa.

Maneno yako Kiranga ni ya kukosoa, tone yako ni ya kulaumu na kubagaza. Kwa maslahi ya nani na tunapata nini out of this. Hakuna.
Hapana.

Kuukuza strategy si kubagaza.

Ni kuuliza strategy tu.

Na kujitoa sadaka si strategy ya kukomboa nchi.
 
Polepole ndio alitakiwa amuhadithie Kiranga strategy yake kuwa nina mpango moja mbili tatu?

Kuweni serious kidogo basi.
Halafu kutaja strategy kwa aliyokua anayafanya Polepole ingekua ni sawa na kuuza ramani ya vita,
Sio kila kitu huwekwa wazi na muhusika,mengine hua ni siri ili kutimiza lengo secretly.
 
Back
Top Bottom