GE2025 Swali hili la Kiranga kwa Polepole lilipuuzwa: What is Polepole's strategy? Lilifanya Kiranga atukanwe sana

GE2025 Swali hili la Kiranga kwa Polepole lilipuuzwa: What is Polepole's strategy? Lilifanya Kiranga atukanwe sana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Amani iwe nanyi watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU

Ukiachana na maumivu makali sana niliyo nayo lakin swali la kiranga bado linaniumiza kichwa na linanifunza mengi na linanifanya nisimuelewe kabisa polepole

Nakuombea polepole MUNGU MWENYEZI akulinde sana

Nakuombea Tanzania ukomboz wako umewadia

Asanten sana

SAYUNI BOY
Yani Polepole ampe mkimbizi mmoja strategy zake,!? Mkimbizi ambaye Kila kucha anabweka jamiiforum na ID yake fake ila hang'ati akiwa amejificha kwenye nchi za wengine kama mkimbizi, Huyo mkimbizi Hana hiyo moral authority ya kuhoji strategy ya Polepole
 
Alipaswa kuchukua tahadhari zipi ili wewe uone kua kachukua tahadhari?
Alipaswa kuishi nje ya Tz kama wenzie akina MangeKimambi. Lakini unakaa Tz unainanga Serikali, hata Agustino Polepole (kaka yake), akifika bei anakuuza tu
 
Tumezaliwa mara moja tutakufa mara moja kwa hiyo hata ufanye nini ujifiche na I'd fake utakufa hata kugongwa na gari anaembeza Polepole huyo ni mtu mpumbavu ova
 
Kwanini polepole alibaki nchini alijiamini nini? Ili iweje
Sasa wewe ulitaka aende wapi? Kwa nini kila anaiendea kinyume serikali ya ccm lazima akimbie nchi yake? Polepole ni mtanzania, kwao ni tanzania, kwa nini aondoke kwa kuikosoa serikali tu? Kama mtindo huu wa kukimbia kimbia nchi ndio maana serikali haiingii na hofu yeyote ile kutoka kwa wapinzani. Kumbuka nyerere alisema mkimbia nchi ni haini wa nchi.
 
Ni swali la kidhahania, si lazima aseme. Aseme, asisema, swali lipo tu.

Kwa sababu kinachojadikiwa ni hoja, si mtu.

Mfano Fidel Castro alipovamia Cuba na Che Guevara mkakati wao ulikuwa wa kijeshi mpaka wakaichukua nchi.

Mandela na ANC walikuwa na mkakati wa kuwabana makaburu kwa vijwazo vya kinataifa, migono ya ndani, maandamano, mpaka kikaeleweka.

Ndiyo tukauliza, huyu Polepole ana mkakati gani?

Maana kusema serikali tu kila mtu anaweza, lakini then what?

It turns out Polepole si tu hakuwa na mkakati wa kukomboa nchi, hakuwa hata na mkakati wa kujilinda yeye mwenyewe.

Watanzania wengi wanapenda kufanya mambo kwa emotions, bila logic, bila mkakati, bila intentionality.

Polepole wengine walifikiri kavuka maisha hayo, lakini matukio yameonesha yuko palepale tu.
Mkuu unachosema ni kweli, na ndio haswa kinaniwazisha. Gwajima nilijua kakurupuka. Lakini Polepole kakaa kwenye system, nilijua vita yake kaipanga vizuri, hata niliamini ana watu wakubwa wa system nyuma yake.
Lakini baada ya kutekwa ndio naona kafanya errors nyingi ndogo ndogo ambazo kwa mtu wa system kama yeye hakupaswa kufanya.
Kwamba alipanga kuongea tu? alete mageuzi kwa kuongea?
Kwamba angejificha milele?
Kwamba asingeishiwa pesa au mahitaji? maana hakuwa na kazi tena.
Kwamba alisema yote aliyotaka kusema? je wangemkamata kabla hajasema yote?
Mifumo ya Ulinzi, CCTV, choice of hiding place, personal weapons, hivi vyote alizingatia?
Hakuandaa hata tape ya kublackmail watesi wake incase amekamatwa imsaidie?
Nani ana nguvu yupo nyuma yake anaweza kumsaidia kumsemea au kushinikiza aachiwe?
Kwamba kaacha kazi sababu ya harakati ambazo ziko doomed kufeli tangu day 1?
 
Yale matambara ya kijani aliyoweka kama mapazia kwenye chumba alimokuwa anajirekodi ndiyo tahadhari? Be serious
Kasome kiss Cha Afisa Usalama hapo Rwanda Be Andrew Kayegere utaelewa Background SI kitu Cha kubeza hata kidogo.
 
Back
Top Bottom